WAFANYA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA WAZIDI KUKAMATWA
WATU wawili raia wa kigeni wanashikiliwa na polisi mkoani Lindi baada ya kukamatwa wakiwa na kilo 40 za madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye thamani ya shilingi bilioni 2.4, tukio lililotokea Februari 7, mwaka huu.
Miongoni mwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema watu hao, Ture Ally (55) raia wa Uganda na Sano Sadick Abobakary (53) wa Guinea Bissau, walikamatwa katika kizuizi cha Nangurukuru wakitokea Msumbiji kuelekea jijini Dar es Salaam.Polisi walikuwa wameweka mtego baada ya kupewa taarifa na raia wema, dawa hizo zilikuwa zimehifadhiwa katika paketi 40 zilizokuwa na uzito wa kilo moja kila moja na walikuwa na gari lenye namba za usajili UAU 789 na kesi yao ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Lindi.
Binti huyo ambaye bado hajafikishwa mahakamani, alikamatwa akiwa njiani kuelekea Nairobi na Mombasa na Kamanda wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa amewataka wananchi kuzidisha ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu mtu yeyote wanayemhisi kujihusisha na biashara hiyo haramu.
GPL.