Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

JANGA LA UPUNGUFU WA NGUVU NA MATUMIZ YA VIAGRA KWA WANAUME


Inasikitisha sana siku hizi wanaotumia Viagra ni vijana wadogo sana ,wengine hata ni wanafunzi wa vyuo. Na hii si Dar tu, mpaka hata mikoani..nilikua Dodoma nikawa na jamaa yangu mmoja pale anaduka la dawa...ananiambia Viagra ndio inamlipa kuliko dawa zote.

Wateja ni wanafunzi wa vyuo na waheshimiwa. Sijui kwa kweli nini kinalikumba Taifa. Hivi kweli kwa mawazo yako unaweza ikomoa papuchi wewe. Acheni ujinga jamani.
Excellence is not a destination you arrive at… It is the benchmark for your journey. Earvin “Magic” Johnson

MSANII WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA



Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia usiku wa kuamkia jana.
Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba  ambazo  ni Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k.
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

Picha za Trafiki aliyetimuliwa akiwa kavaa kiraia, Ni Sheeedah.


Wezee Nimekutana na Hiyo Picha Instagram, Yule Polisi wa Kike Traffic Watu wamechimba Mpaka Wamepata Picha zake Akiwa Bila sare za Kazini....

Baadhi ya Comment ni Hizi Hapa :

-mwambie alete CV mi ntamwajiri

-Aje kwangu atalelewa kuliko alivyokuwa huko!Contact pls 

-Kajazia Sana hata Ingekuwa Mimi Ningekula Mzigo, hiyo ni ajali kazini

OPEN RELATIONSHIP ni Map3nz! ya hatari sana.




kuna hii aina ya uhusiano wa kimap3nz! iliyopewa jina la open relationshi=mapenzi yasiyokufunga kuwa na Mp3nz!/Wap3nz! wengine hata kama mp3nz! wako akijua wala hamind na wewe ukimuona na demu mwingine wala hakuna tatizo.

Wap3nz! wa namna hii huwa mara nyingi wanakuwa na siri ya uhusiano wao na pengine wanatambulishana kwa wapenzi wao wengine kuwa"huyu ndiyo girlfrend wangu ama huyu ndio boyfriend wangu na hao wanaotambulishwa wasijue kama hawa ni Wap3nz! na si masheji ama mawifi kama wanavyodanganywa".
WENGI WANATAMBULISHWA KWA HAWA WATU NA HAWAJUI NA WANABAKIA Kujua yule ni wifi kumbe mke mwenza ama yule ni shemeji kumbe mume mwenza.

LAKINI KUNA WENGINE KWENYE facebook Nashindwa kuelewa kama wanamaanisha open relatioship ya kweli wanapoandika hivyo status zao kwa luv ama wanafanya direct english swahili translation na kufikiri open relationship=uhusiano usio wa kificho, mana ni ngumu kidogo kuweka wazi kuwa una Wap3nz! tayari lakini haikufungi kuwa na mwingine.

JF.

SHEMEJI ANANITAKA KIMAP#NZI, KADHAMIRIA WEEKEND TUFANYE WAKATI DADA ANASAFIRI.


Toka nilipohamia nyumbani kwa dada yangu, mume wake amekuwa akisumbua sana maisha yangu, kwanza alinitumia meseji na nilidhani ilikuwa ni utani, jana usiku tu, na kwa makusudi ametoka kunishika kalio langu nilipokuwa jikoni napika, hakika nilikasirika sana mpaka nilikataa kula na dada yangu aliniuliza kwa nini naonekana kama nimekasirika? Sikuwa na neno la kumjibu sababu yule mume wa dada alikuwa ananiangalia machoni.

Mchana wa leo alinitumia meseji nyingine akinieleza kwamba dada yangu anategemea kusafiri siku ya Ijumaa na atarudi Jumapili hivyo atakuwa na mimi kwa muda wote na kwa raha zake, hebu fikiria? Je nahitaji kumueleza dada yangu juu ya hili na je atajisikiaje? Sababu nisingependa kuzua matatizo kati yao.

Naomba ushauri -

SAMSUNG yawalipa APPLE $ Bilioni 1 kwa kupeleka Malori 30 yaliyojaa Senti 50


Baada ya Mvutano wa zaidi ya Mwaka, Mahakama iliamua kampuni ya SAMSUNG kutoka Korea ya kusini kuwalipa APPLE zaidi ya Trilioni 1.6 za Kitanzania kama faini inayotokana na Kokopi kwa Teknolojia bila kibali husika.

Cha kufurahisha ni kwamba Mahakama haikulazimisha malipo hayo yafanyike kwa mkupuo au kwa awamu ili mradi hela hizo zitimie. Kutokana na hayo SAMSUNG waliamua kuwachezea rafu ya aina yake APPLE kwa kupeleka Malori 30 ambayo ndani yake yalikuwa yamejaa Coins za senti 50 ili kulipa Faini hiyo.

Walipofika Mlangoni walizuiliwa na walinzi wa hapo lakini baadae kidogo CEO wa APPLE, Tim Cook alipigiwa simu na CEO wa SAMSUNG kumwambia kuwa huo ndio mzigo wao na deni litalipwa kwa namna hiyo.

Mchezo huo Mchafu na wa akili utawapa Gharama kampuni ya APPLE kwani watapoteza muda kuhesabu na kuhakikisha ukamilifu aw Kiasi hicho cha fedha na kujipanga kuzipeleka Bank.

Katika maelezo yake Mwenyekiti  wa SAMSUNG, Lee Kun-hee amesema kwamba kampuni yake haiwezi ikatetereshwa na na "Wajanja wenye Mbinu" ikiwa wanapenda michezo michafu, hata wao wanaiweza.

Ikiwa watataka kuziyeyusha Coin hizo na kutengenezea Computer basi ni juu yao hainihusu, nimeshatekeleza amri na kuwalipa Coins Bilioni 20 zenye thamani ya $ Bilioni Moja.

Ukilala na Mwanamke huyu unakwenda na Maji


Wakuu!
Haya ni maajabu kidogo, leo nimekutana na mwanamke mmoja anatokea Masasi, kuja Tandahimba kwa fundi (mganga wa kienyeji.)

kwa bahati nilifanikiwa kupiga nae stori na akanielezea kisa kilichomfanya aje Tandahimba kumtafuta fundi!

Inshort tatizo lake yeye ni kuwa aliolewa kama miaka 2 hivi iliyopita na katika ndoa yake ilitokea mtafaruku kati yake na mumewe kitu kilichopelekea wakatengana.

Sasa ajabu ni kuwa tokea atengane na huyo mumewe, kila mwanaume anayekutana nae kimwili(kus3x nae) lazma apate homa kali, na akipona tu! Anakuwa siyo rizki tena!
Kesha fanya hivyo na zaidi ya wanaume 4 na wote wamekutwa na tatizo hilo, ndiyo akagundua kuwa tatizo ni yeye na anadhani amelogwa na mume wake wa kwanza!!

Ndiyo mjue wanawake wengine ni hatari, na dawa nyingine ni hatari..

Kuna kulogwa hadi kwenye map3nz!

JF

Isikilize U Heard ya Nov 20 kuhusu msanii Berry White kuchoma hili gari.






Soudy Brown anaamplfy kuhusu msanii Berry White kuchoma gari la mpenzi wake ambae walikua kwenye ugomvi.. stori zaidi ipate kwa kubonyeza play hapa chini…
Berry white 2

Aota maziwa baada ya kuiba Ng'ombe wa Watu


Wakati mwengine huwa nacheka na kushangazwa na kutokana na habari ambazo binafsi zinanifikia, ila ni kazi yangu ya kuzifikisha kwenu na kuwaachia ninyi kuweza kufanya maamuzi ya kuamini au kutoamini.

Jamaa huyu mwenye umri wa miaka 40 kutoka Nherera ndani ya Mhondoro, Zimbabwe gafla maziwa yake yalianza kukua kwa kile kinachoelezwa kuwa aliiba ng'ombe wa mtu mmoja na kisha kuwauza.

Wanakijiji wa sehemu hiyo wanasema kuwa jamaa huyu aliyefahamika kama Acry Chinhivi Shayamano amefanyiwa kitu hiyo mbaya na aliyeaminika kuwa ni mmiliki wa ng'ombe hao.

Nimekolea na P3nz! la Demu wa Rafiki yangu


Nimekolea kwa Aliyekuwa Demu wa Rafiki Yangu. Je Nifanyeje?

Nimejikuta nipo kwenye mapnz na aliyekuwa demu wa rafiki yangu. Rafiki yangu na huyu demu walikuwa kwenye mahusiano katika kipindi cha mwaka mmoja ila wakaja achana.

Kwa sasa huyu rafiki yangu ana demu mwengine na haonekani kuwa na nia ya kutaka kumrudia huyu aliyekuwa wake hapo awali ambaye kwa sasa nimejikuta nikikolea kwake.

Japokuwa ni mkubwa kwangu kwa zaidi ya miezi sita ila ukweli ni kwamba nampenda.

Naomba ushauri nini nifanye....?

Bibi anapokolezwa na Damu changa


Hatuwezi kuficha na kusema kuwa hili ni tukio la kawaida, hata pia hatuwezi sema kwamba eti hawa watakuwa wanacheza tu.

Ila je hii hatuweza sema kuwa hiki ni kitu kizuri na kitamu sana ambacho bibi huyu anaonekana kukifurahia kiasi cha meno yote 32 kuwa nje kiasi hiki....?

P Square watua Dar kwa ajili ya Makamuzi ya Jmosi

<

Wanamuziki wa kundi la P-Square Peter na Paul baada ya kutua jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkrulu ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East Africa Radio na EATV.
 
 Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao.
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea.
Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi ya kesho
(Picha na Mdimuz Blog)

Mke anusurika Kung'olewa Jicho na Mumewe baada ya Kumnyima Unyumba



MWANAMKE mmoja Sada Majaliwa mkazi wa Temeke Mikoroshini jijini Dar, amedai kunusurika kutolewa roho na mumewe Mohamed Rashid hivi karibuni kwa kosa la kunyimwa unyumba.

Akizungumza na mwandishi wetu, Sada alisema siku ya tukio, mumewe alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na  kudai unyumba kwa nguvu, jambo ambalo hakukubaliana nalo na kusababisha kutokea kasheshe kati yao.

“Siku zote nimekuwa nikimpa unyumba kama kawaida, lakini siku hiyo mwenzangu alirudi akiwa amelewa chakari, sikupendezwa na hali yake ndiyo maana sikutaka kushirikiana naye,” alifafanua Sada.

Mke huyo alisema baada ya kukataa kushiriki tendo hilo, mumewe alianza kumkaba shingoni kwa kutumia mikono yake, lakini alipoona haitoshi akachukua khanga na kuendelea kumkaba nayo.

Sada alidai kwamba hali ilikuwa mbaya na alishindwa kujiokoa kirahisi na kulazimika kumng’ata mumewe mkononi ndipo alipojiokoa huku shingo yake ikiwa imechubuka.

“Baada ya kunikaba na khanga shingoni sikuwa na jinsi ilinibidi nimng’ate ndipo aliponiachia na kupata upenyo wa kutoka nje,” alisema.

Sada alidai baada ya tukio hilo yeye na watoto wake walikimbilia kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Rehema Bakari kuomba hifadhi wakati akisubiri mwafaka na mumewe.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo mume wa Sada amekamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
“Mume wake amekatwa leo (Jumatano iliyopita) lakini nitaendelea kumhifadhi mwanamke huyu hadi pale suala lake litakapopata mwafaka,” alisema mwenyekiti huyo wa serikali ya mtaa.

GPL

Kauli ya Mwisho ya Babu Seya na Papii Kocha kabla ya kurudishwa Gerezani



Ni dhahiri kwamba huu ndio mwisho wa harakati za Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi Tanzania mwenye asili ya Congo DRC Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza (Papii kocha) kujinasua kwenye kifungo cha maisha gerezani.

Kwa mara nyingine tena harakati zao za kujitoa kwenye adhabu hiyo zimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Rufani kupigia msumari wa mwisho uliozima harakati zao kujinasua baada ya kutupilia mbali maombi yao ya marejeo ya hukumu ya rufaa yake.

hii ni mara ya tatu kwa wafungwa hawa kugonga mwamba baada ya Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa zao kupinga hukumu ya Mahakama ya hakimu mkazi  kisutu iliyowahukumu kifungo cha maisha.

Wafungwa hawa kupitia kwa Wakili Mabere Marando walikua wakiiomba Mahakama ya Rufani ifanye marejeo ya hukumu yake ya February 11 2010 iliyothibitisha adhabu hiyo waliyohukumiwa na Mahakama ya chini na badala yake iwaachie huru lakini Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake uliotolewa na Majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk ilitupilia mbali maombi hayo hivyo waendelee kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Ni uamuzi ambao uliibua machungu sio tu kwa Wafungwa na ndugu zao lakini hata kwa Wakili wao mwingine Gabriel Mnyele aliesema ‘hakuna namna nyingine ya kuwachomoa kwenye adhabu hii isipokua miujiza’
Ndugu na watu wengine waliohudhuria Mahakamani waliendelea kutokwa na machozi ya huzuni pale Wafungwa hawa walipokua wakipandishwa kwenye gari la Magereza kurudishwa kuendelea kutumikia adhabu yao.

Kauli ya Mahakama baada ya kutupilia mbali maombi yao ni ‘Waomba Marejeo hao hawakuwa na hoja ya msingi kwa sababu hoja zilizotolewa sio tu hazikidhi kuifanya Mahakama irejee hukumu hiyo bali pia zilishatolewa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na kutolewa uamuzi na kwamba waomba Marejeo hawakuweza kubainisha makosa waliyodai yalijitokeza kwenye hukumu iliyowatia hatiani na hawakuweza kueleza ni jinsi gani yalisababisha haki kutotendeka’

Mahakama hiyo imesema ‘kuhusu upande wa mashtaka kushindwa kuwaita Mahakamani mashahidi wanaoonekana kuwa muhimu kuunga mkono ushahidi wa Watoto, tunasema hoja hiyo haina msingi…. suala la shahidi gani aitwe Mahakamani kuthibitisha kesi ya upande wa mashtaka liko mikononi mwa upande wa mashtaka, zaidi ya yote idadi ya Mashahidi sio hoja ya msingi bali kuaminika kwao’
Wakili Mnyele amesema ‘huu ndio mwisho wa mchakato, kulinganisha na hukumu ilivyokua ni kwamba kunahitajika kuwepo na Mahakama ya juu zaidi ya hii, kungekuwepo na Supreme Court ingeweza kusikiliza na kufikia maamuzi ya haki’

Kwa upande wake, Babu Seya wakati akipelekwa na askari kwenye gari la Magereza alitoa kauli ambayo hakuipa ufafanuzi wowote baada ya kuisema kwamba ‘kwa binadamu ni makosa lakini kwa Mungu hakuna makosa’

Papii Kocha nae wakati anapelekwa kupanda gari arudishwe Magereza alisema ‘sasa tunamuachia tu Rais ndie anaweza kutoa uamuzi wa mwisho’

Babu Seya na wanawe watatu walihukumiwa adhabu ya maisha gerezani na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu June 25 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto kumi wa kike wenye umri chini ya miaka 10.

JB afumaniwa na Mke wa Mtu Hotelini Dodoma



LILE sakata la madai kwamba, staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’ amenaswa akiwa na mke wa mtu mjini Dodoma limeingia katika sura tofauti baada ya habari yenyewe kujaa utata.

Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
 “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”
Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.
Staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’.

Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
 “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”



Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.

GPL.

Mchumba Aliyenusirika katika Mauaji ya ilala anena mazito


Christine Newa

Imebainika kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.
Akizungumza nyumbani kwao Ilala Bungoni jana, mmoja wa majeruhi ambaye ndiye aliyekuwa kiini cha shambulizi hilo, Christine Newa alisema si kweli kwamba sababu ya mchumba wake, Gabriel Munisi kuwashambulia na kuwajeruhi kwa risasi yeye na mama yake mzazi, Ellen Eliezer na kumuua mdogo wake wa kike, Alpha Newa ni kutokana na kusaliti uchumba wao.
Awali, ilidaiwa kwamba sababu ya shambulizi hilo ni Christine kumkataa Munisi, (ambaye pia alijiua baada ya kufanya mauaji hayo) na kuchumbiwa na rubani wa ndege, marehemu Francis Shumila ambaye pia alifariki katika tukio hilo... “Kwanza Shumila hakuwa mchumba wangu kama ilivyoelezwa. Alikuwa shemeji yangu, mume wa dada yangu Caroline Newa. Pia hakuwa rubani wa ndege, bali nahodha wa meli.”
Alisema amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Munisi katika kipindi kisichofikia mwaka mmoja lakini sehemu kubwa ya maisha yao ikitawaliwa na misuguano iliyowafikisha polisi mara kadhaa.
Alisema katika kipindi cha uhusiano wao marehemu Munisi alikuwa akimpiga, akimkataza kufanya kazi, kusoma na alikuwa na wivu uliopindukia.
Christine kuona hivyo, aliamua kufanya mipango ya kwenda kusoma katika Visiwa vya Cyprus kimyakimya pasi na kumuaga, jambo ambalo alisema lilimkera mchumba wake huyo na kuweka kisasi.
“Nikiwa huko, Munisi alitafuta mawasiliano hadi akayapata na tukawasiliana na siku niliporejea alikuja kunipokea uwanja wa ndege lakini cha ajabu, alinikataza kwenda nyumbani na badala yake akanipeleka moja kwa moja hadi Mwanza eneo la Kitangiri,” alisema na kuongeza: “Tukiwa njiani kuelekea Mwanza, katika maeneo ya Singida, alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?”
Alisema alimwomba msamaha na kuendelea na safari yao. Anasimulia kwamba baada ya kufika Mwanza, alimpora simu zake zote na kumfungia ndani kwa zaidi ya wiki mbili hadi alipopanda kwenye dirisha na kuomba msaada kwa majirani na kuwapa namba za simu za ndugu zake ili wamsaidie kuwapa taarifa.
Ndugu zake walianza mchakato wa kuwasiliana na polisi hatua iliyofanikisha msichana huyo kurudishwa Dar es Salaam... “Hata hivyo niliondoka na khanga na fulana tu. Vitu vyote niliviacha huko.”
Baada ya kurudi Dar es Salaam, anasema Munisi naye aliamua kumfuata lakini safari hii alifikia katika Hoteli ya MM iliyotenganishwa na ukuta wa nyumba yao na akawa anafuatilia nyendo za familia hiyo.
“Alikuwa ananitumia meseji kwamba amemuona dada Caro, mama na Alpha na wakati mwingine anasema ameniona mimi mpaka nguo tulizovaa, tukaanza kupata na wasiwasi,” alisema.
Wasiwasi huo ulitokana na historia ya maisha yao ya Mwanza na pia tishio ambalo anadai kwamba Munisi aliwahi kulitoa kwamba atahakikisha anaiteketeza familia yote kuanzia Goba anakoishi mama yake (Ellen), Zanzibar anakoishi mdogo wake (marehemu Alpha) na hapo Ilala.
Anasema walikwenda polisi lakini walielezwa kwamba hayo ni masuala madogo ya mapenzi na kwamba yatamalizwa kifamilia.
Siku ya tukio Christine alikuwa akitoka kwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurudi shuleni Cyprus ndipo Munisi alipotokea na kuanza kumrushia Shumila risasi na baadaye Alpha kisha mama na yeye kabla ya kujiua.
Akizungumzia tukio hilo, Caroline alisema mumewe alitabiri kifo chake kabla kwani baada ya kusikia vitisho vya Munisi, alimtoa shaka Christine akimwambia kwamba atamlinda hata ikibidi kupoteza maisha yake, jambo ambalo lilidhihiri.
Alisema mama yake amepata nafuu na ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa na mazishi ya mdogo wake, Alpha ambaye ameacha mtoto mwenye umri wa miezi minane, yamepangwa kufanyika Jumamosi Goba, Dar es Salaam.

Alisema mipango ya mazishi ya mumewe inafanywa huku akidokeza kwamba huenda akasafirishwa kwenda Mombasa.

Angalia Hapa Video ya Single kali KUCHI KUCHI Toka kwa Jodie


Jack wa Maisha Plus naye atumbukia katika Tabia Chafu



MREMBO aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dunstan ‘Jack wa Maisha Plus’ amezua jambo katika mtandao baada ya kutundika picha akiwa anabusiana na mwanamke mwenzake.

Jack ambaye kwa sasa yupo nchini Dubai, aliweka picha hiyo katika mtandao wa Instagram hali ambayo iliwashangaza wadau wengi waliopo kwenye mtandao huo ambapo walimchana kuwa aache vitendo vya kisagaji lakini mwenyewe hakujibu.

Jack baada ya kuweka picha hiyo aliandika maneno haya; ‘mwaaah’ ndipo wadau walipoanza kumshambulia na kumtaka aondoe picha hiyo chafu.

 GPL

Rage Arudi Madarakani Simba


BARAZA la Wadhamini la Klabu ya Simba, limesikia maamuzi yaliyofanywa na kikao cha kamati ya utendaji ya timu hiyo, juu ya kumsimamisha mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage na kusema lenyewe bado linamtambua kiongozi huyo.
Hamis Kilomoni, ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, maamuzi ya kamati ya utendaji ya timu hiyo hayakufuata katiba kikamilifu, hivyo baraza lake linaendelea kumtambua Rage kama mwenyekiti halali wa Simba.

Kilomoni, ambaye ni nyota wa zamani wa timu hiyo, amesema juzi aliitisha kikao cha baraza lake na kukutana na mwenzake Ramesh Patel, ambapo wamegundua kwamba kamati  haikufuata katiba kikamilifu.
Alisema kamati hiyo ya utendaji ilitakiwa kuyachukua maamuzi yake na kuyawasilisha katika baraza la wadhamini au lile la wazee, ambayo yote yanaongozwa na yeye.

Hata hivyo, Kilomoni alibabaika wakati akitoa maelezo yake baada ya kuulizwa inakuwaje wadhamini ambao kazi yao ni kuangalia mali za klabu, waingilie uamuzi wa kiutendaji!

“Kweli hatujaingilia, lakini tunachotaka ni kuwakutanisha baada ya Rage kutua kesho (leo) usiku,” alisema na alipoulizwa inakuwaje wametengua uamuzi wa kamati ya utendaji na kuendelea kumtambua Rage, alisema:
“Sasa sijui unavyofikiri ila sisi tunataka kulimaliza hili suala, unajua tumekutana mimi na Ramesh Patel ambao ndiyo wadhamini, mmoja wetu anaishi Uarabuni na tusingeweza kushirikisha baraza la wazee kwa kuwa halipo.

“Maamuzi waliyoyafanya vijana wetu tunayaona kama yana kasoro, katiba haiwaruhusu kuchukua maamuzi ya aina hiyo, ni kama wamefanya maamuzi kwa jazba kubwa, jambo ambalo tunaona siyo sahihi.”
Kilomoni alipoulizwa ni kipengele kipi cha katiba kinawaruhusu kutotambua maamuzi ya kamati ya utendaji, alijiuma:

“Aah mi sikijui, labda nirudi na kufungua katiba nitafute tena lakini kikubwa tunataka kusuluhisha.”
Kuhusiana na kurejea kwa Rage, Kilomoni alisema hatambui kama atarejea na matarumbeta na kupokewa na wanachama.
“Sijui lolote, hajaniambia kama anataka kufanya hivyo. Lakini pia sijui lolote kuhusiana na mkutano wa Jumapili ambao Rage inasemekana atauitisha, nimesikia tu lakini sijui,” alisema.

Awali, ilielezwa kuwa, baada ya Rage kurejea na kupokewa kwa mbwembwe, atafanya mkutano keshokutwa Jumapili na kuwatimua wajumbe wote wa kamati ya utendaji ambao walimsimamisha na kuitisha mkutano Desemba Mosi ambao utatoa uamuzi wa mwisho arudi madarakani au ndiyo ‘apigwe chini kimoja’.

Awali, katika hali iliyoonekana ni ya kushangaza, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, alikuwa amepanga kuzungumza katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Msimbazi, Kariakoo jijini Dar, lakini akaukimbia, ndipo waandishi walipoelezwa waende Kinondoni kwa mzee Kilomoni kwa ajili ya mkutano huo.

Kuhusiana na mgogoro huo wa Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema limepokea barua kuhusiana na kusimamishwa kwa Rage na nafasi yake kuchukuliwa na Mzee Kinesi.

“Tumepokea barua na sasa tunasubiri suala hilo tutalipeleka kwenye kamati ya sheria,” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura.

Hata hivyo, hakuna kamati yoyote hadi sasa tangu uongozi mpya uingie madarakani chini ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambaye juzi alisema watakutana kesho na kuziunda upya.

Siku moja baada ya kusimamishwa na kamati ya utendaji kwa madai ya ubadhirifu, Rage akiwa nchini Sudan kwenda Marekani, aliamua kuahirisha safari hiyo, mara moja na ameamua kupanda ndege kurejea nchini ambapo atatua leo jioni.
Imeelezwa Rage amepanga kupokewa na wanachama wanaomuunga mkono ambao watakwenda naye kwa maandamano hadi makao makuu ya klabu ambako atafanya mkutano.

Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Swedi Nkwabi, alisema: “Sisi tunaamini tulichoamua ni sahihi, kama mzee Kilomoni amesema tungeweza kumuonya, kweli yuko sahihi lakini katiba inaturuhusu kuchagua pia kama kumuonya au tunaona kumsimamisha ni sahihi, pia hakuna tatizo.”

TANESCO KUPANDISHA GHARAMA ZA UMEME


 Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeomba kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 67.87 ikiwa ni kutoka Sh197.8 kwa Unit mpaka Sh332.06.
Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba, alipokuwa akiwasilisha maombi ya shirika hilo mbele ya Wadau wa Umeme na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).
Alisema kwa sasa uzalishaji wa umeme utokanao na nguvu za maji ni asilimia 13, utokanao na gesi ni asilimia 42 na utokanao na mitambo ya mafuta ni asilimia 45.
“Kutokana na kuongezeka kwa gharama za kutoa huduma, wastani wa bei iliyopo ya Sh197.8 kwa uniti, hailingani na wastani wa Sh332.06 kwa unit inayotakiwa kukidhi mahitaji ya sasa,” alisema Mramba na kuongeza:
“Hii ni pungufu kwa kiasi cha Sh134.25 kwa uniti, ongezeko la bei la asilimia 67.87 litafidia upungufu huo,” alisema Mramba.
Alisema, asilimia ya mapato yanayotumika kulipia gharama za umeme utokanao na mitambo ya dharura na ile ya binafsi ni asilimia 85. “Ikiwa ombi la ongezeko la bei ya umeme halitaridhiwa, shirika litashindwa kumudu gharama za uendeshaji na hivyo kutokidhi mahitaji makubwa ya umeme nchini na kutoa huduma zenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema Mramba.
Alisema madhara mengine yatokanayo na kutoongezwa kwa bei hiyo ni shirika hilo kutokidhi mikataba iliyoingiwa jambo alilosema litasababisha mgogoro ya kimikataba.
Mramba alieleza pia kuwa, hali hiyo italifanya shirika hilo kushindwa kulipa mikopo yake benki na kuathiri uwezo wake wa kuwekeza kupitia mikopo mipya.
Aliongeza kuwa, katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 matumizi ya umeme yamekuwa yakiongezeka wakati kiwango cha mvua kikiwa chini ya wastani hali iliyosababisha Tanesco kutumia zaidi umeme unaozalishwa kwa mafuta.
“Katika kipindi hiki kiwango cha gesi asili hakikukidhi mahitaji ya nishati kwa sababu ya ufinyu wa miundombinu ya gesi iliyopo. Upungufu huu ulisababisha mgawo wa umeme mwaka 2010 na 2011,” alisema na kuongeza:
“Athari ya mgawo wa umeme katika taifa ni kubwa, kulingana na utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia, hasara kwenye uchumi wa taifa ya kutokuwapo kwa umeme kutokana na mgawo ni wastani wa dola za Marekani 1.1 kwa kila uniti,”.
Katika hatua nyingine, Mramba alisema kutokana na gharama za uzalishaji kupanda, hasara ndani ya shirika hilo imeongezeka kutoka Sh43.43 bilioni mwaka 2011 hadi Sh178.45 bilioni mwaka 2012.

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga