Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

BREAKING NEWS :MEZ B AFARIKI DUNIA


Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake amefariki Dunia. Mez B alikuwa akiuguliwa na homa ya mapafu [Pneumonia] na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa siku ya tatu toka anatumia dawa hizo. 



Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe drip ila hali yake ikawa mbaya zaidi, wakati wanampeleka hospitalini alifia walipofika mapokezi. Jirana amelezea haya. 

Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen

BAADA YA KUONEKANA PICHA ZA UTUP# ZA NAY AKIWA NA KIMWANA, WADAU WAMPA UJUMBE HUU.


 
KWAKO mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’. Mambo vipi? Mishe zinasemaje? Binafsi mimi ni mzima wa afya, maisha yanasonga mbele kwa kasi ya ajabu. Tunapambana!Nimekukumbuka leo kwa barua maana kitambo kidogo hatujaonana. Nakupongeza kwa nyimbo zako maana hata wale waliosema ulibebwa na Diamond katika wimbo wa Muziki Gani, sasa hivi wanajutia kauli zao.
Wanaona walikosea maana umefyatua nyimbo zako mwenyewe na unaendelea kukimbiza mitaani.
Madhumuni ya barua hii ni kutaka kukueleza kwamba wewe ni staa hivyo unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kila mtu katika jamii. Hutakiwi kuteleza hata kidogo. Ukiwa wewe ndiyo kinara wa majanga, utatolewa mfano kwamba hufai kuigwa kutokana na matendo yako maovu.

Kila mmoja anatambua uwezo wako, anatambua hatua ambayo umefikia kimuziki. Watu wanatambua kwamba una mchumba ambaye una mikakati ya kufika naye mbali kwa maana ya ndoa Mungu akipenda.
Kinachoshangaza ni kwamba, inakuwaje unaonekana katika pozi za kimahaba na mwanamke mwingine? Picha zenyewe zinatia kinyaa?
Mwishoni mwa wiki iliyopita gumzo katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni wewe na picha zako za utup# na mwanamke huyo ambaye hakuwa mchumba wako.Ndugu yangu, picha zile hazikuwa nzuri kwako. Zimekudhalilisha na hata kukuletea ugomvi kwa mchumba wako.
Kwa nini ulikubali kupiga picha za namna ile? Zilikuwa za nini? Ulikuwa na malengo gani? Hata kama mlikuwa katika ‘shooting’ ya wimbo kwa nini ulikubali kupigwa picha katika hatua ile?
Tena bora zingevujishwa na mtu mwingine, wewe mwenyewe unatajwa kuwa ndiye chanzo cha kusambaa kwa picha hizo kupitia mitandao yako ya kijamii, hivi kwenye kichwa chako uliwaza kabla ya kufanya?
Unapaswa kujiheshimu hata kama ni video ya wimbo, naamini kwa desturi zetu, kamwe huwezi kuruhusiwa kurusha video ya namna hiyo hewani. Tamaduni zetu haziruhusu, unasubiri nani akuzuie kufanya hivyo wakati wewe kama kioo cha jamii unapaswa kuwa mfano?
Una watoto sasa, ulimwengu wa sasa si ule wa zamani. Picha zako za utupu zinachapishwa magazetini, zitasambaa kwenye mitandao mbalimbali na wanao pia watajionea bila wasiwasi. Watajifunza nini kutoka kwa baba? Jibu najua unalo na haliwezi kuwa zuri kwa mtu muungwana.
Ulimwengu wa sasa, ukifanya vituko vya namna hiyo, rekodi zake zinabaki kwenye mitandao. Vizazi na vizazi vitakuja kuona hayo uliyoyafanya juzi. Badilika kaka!Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa, kwa leo naishia hapa, naamini utafanyia kazi mawazo yangu na kubadilika.
Wasalaam,

WABONGO WANAWAPA ULAJI SANA WA SOUTH" AY


Yessaya ‘AY' akipozi.
Stori: Shani Ramadhani
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene
Yessaya ‘AY’ amefunguka kuwa maprodyuza
wengi waliopo Afrika Kusini ‘Sauz’
wanapata faida kubwa sana kutoka nchi za
Afrika hasa Tanzania kupitia muziki.
Akichonga na Over The Weekend, AY alisema
wasanii walio wengi kutoka Bongo
wamekubaliana
na gharama zao ndiyo maana wanakwenda
kurekodi huko kuanzia ‘audio’ mpaka video.
“Sauz sasa hivi imekuwa kama moyo wa
muziki kwa Wabongo kutokana na kila
mmoja kukimbilia huko kwa sababu tu kuna
waandaaji wengi wa muziki.
Wanawanufaisha sana, natamani na sisi
siku moja Wasauz wakimbilie Bongo
kurekodi,” alisema hj

RAY C KUMSAIDIA DAZ BABA KUPONA "UTEJA"


Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya. 

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo Daz Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia dozi ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.

Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Ray C, alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz ila akaomba asizungumzie walipofikia kwa sasa.


KWELI BODY GUARD WA DIAMOND NI NOUMAH, ANGALIA MBWEMBWE ZAKE HAPA.


Kwa tetesi tunazosikia huyu jamaa ndo mlinzi binafsi wa wasanii wa hapa Tanzania anayelipwa ghali zaidi. kuanzia mshahara na marurupu mengine kiasi kwamba anaishi kama majuu vile. Si haba kama shukrani yake kuendelea kukitunza kibarua chake kwa kuji keep well fit kila mara.

Angalia baadhi ya picha zake hapo chini ikiwa kikazi zaidi:-




ALI KIBA AKIRI KUWA NA BEEF NA DIAMOND PLATINUMZ, AFUNGUKA.


Hatimaye staa wa Bongofleva Ali Kiba amekiri kuwa yuko katika bifu na mwanamuziki mwenzie Diamond Platnumz kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Kauli hiyo ya Ali Kiba inapingana na ile ya hivi karibuni iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati za bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisisitiza kuwa wanamuziki hao hawana tofauti zozote na kwamba ni watu tu ndio wanakuza suala hilo.
Hata hivyo, juzi Ali Kiba aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli kuna ugomvi baina yao, huku akisisitiza kwamba tofauti yao ilianza mwaka 2012. Wakati Ali Kiba akifunguka kuhusu bifu hilo hali imekuwa tofauti kwa Diamond ambapo amekaririwa mara kadhaa kuwa hana tofauti yeyote na mwanamuzi huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na kuunganisha Kundi la Kigoma All Stars. Akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali katika mahojiano maalumu, mwanamuziki huyo pia alielezea mambo mengi kuhusu muziki wake na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;
Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?
Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga muda mrefu …Labda watu wahisi kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo wake (alisema bila kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta katika wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.
Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo ule, ila ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri tufanye wimbo mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady Jay Dee.
Swali: Umeshawahi kuwa karibu na Diamond?
Ali Kiba: Hapana yeye ndiyo alishawahi kuwa na ukaribu na mimi.
Swali: Unaweza kufanya kolabo na Diamond?
Ali Kiba: Ngoja nikwambie ukweli, sidhani kama ninaweza kuja kufanya kolabo na Diamond, ila nikipata wimbo ambao nadhani kwamba anastahili kuwapo, kiukweli nitamshirikisha lakini kama hastahili haitawezekana.
Kwa sababu kila wimbo unajielezea, kwa mfano kama mtu anataka kufanya Zouk akimtafuta Stara Thomas itawezekana kwani hayo ndiyo mambo yake, kwa hiyo kama nikitaka kufanya naye wimbo ambao nitaona kwamba unafaa nitamfuata na nitamweleza.


Swali: Utofauti kati yako na Diamond ni upi?
Ali Kiba: Mimi naimba muziki mzuri na nina ‘hit song’, naye Diamond anaimba ‘hit song’, unaposema mimi sina hit song wakati mimi nina nyimbo nyingi kushinda yeye unakuwa unakosea, tangu nimeanza kuimba ni nyimbo mbili tu hazijawahi kuwa hit ikiwamo ‘My Everything’ na ‘Mali Yangu’ lakini nyingine zote zilivuma tangu nianze kufanya muziki.
Swali: Inasemekana katika Tamasha la TigoMusic kuna hirizi zilionekana Uwanja wa Leaders na wewe na Diamond mnatuhumiwa kuhusika, unalizungumziaje?
Ali Kiba: Yaani Mungu mmoja sina imani hiyo kabisa na mimi naamini Mungu na mambo ya hirizi na mimi ni tofauti. Nadhani watu wanasema hivyo kwa sababu wanadhani kwamba kuna bifu. Binafsi sina bifu na msanii yeyote labda kama wanaweza kuwa na bifu na mimi binafsi simchukii msanii yeyote na sina bifu na yeyote.
Swali: Video yako ya Mwana imezungumziwa na mashabiki kuwa haikuwa na uhalisia. Pia ilikuwa ya kawaida sana, wewe binafsi unalichukuliaje?
Ali Kiba: Video ilivyokuwa ndivyo ilipangwa iwe kwa sababu kila mtu alikuwa amejenga picha itakuwaje kwa hiyo ililazimika kufanya vile kwa kuwa watu walishapanga mpaka gharama kwa kuwa nilikaa muda mrefu pasipo kufanya. Ningefanya kitu ambacho watu walikifikiria kiukweli ingekuwa karaha, nilichozingatia mimi ni kuimba vizuri na kuonyesha fikra za wimbo husika.
Swali: Vipi uliandaa ‘skripti’ ya video au aliamua GodFather kuifanya vile ilivyotengenezwa?
Kiba: Tulikuwa na ‘script’ yetu pia waongozaji wa video walikuwa na yao ambayo walitupatia. Hivyo tukakubaliana nao kwa sababu tulitaka kuleta utofauti na kila kitu kikakaa sawa.
Swali: Ni kweli kwamba una mpango wa kufanya kolabo na Chris Brown?
Ali Kiba: Uwezekano wa kufanya upo kwa sababu kila kitu ni mipango kwa hiyo naweza kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa na mashabiki watarajie kufanya hivyo.
Swali: Kwa nini haujafanya video ya Kimasomaso na ulisema video ya Mwana ingefanyika Dar es Salaam kwa nini ulitengenezea Afrika Kusini?
Ali Kiba: Video ya ‘Kimasomaso’ ilishindikana kutokana na muda ulikuwa hautoshi, nilijikuta niko katika mambo mengi sana kwani nilikuwa nimeegemea katika video ya Mwana kwa hiyo nilipokuja kugeuka ikawa ni vigumu.
Nilisema kwamba nyingine ningefanya nje ya hapa lakini kwa ‘Mwana’ sijaelewa kwanini nifanye hapa, tofauti na hiyo nyimbo haikuwa na maana ya Dar es Salaam, maana yake ni mwanamke na mwanamume sikuona sababu ya kufanyia hapa jijini.
Ukitumia neno la Dar es Salaam ni kwa sababu ni jiji lenye changamoto kwa hiyo unapozungumzia hilo ina maana kwamba ni Joharnesburg, Nairobi, Kampala, London majiji ambayo yana changamoto mfano video ya Macmuga nilifanyia Marekani.
Source, Mwananchi.

FAMILIA YA RAPPER STEREO YATEKETEA KWA AJALI YA MOTO


Mama mdogo, Baba Mdogo,kaka yake Mjomba na watoto wa Kaka yake Rapper Stereo wamepoteza Maisha kwenye ajali ya moto iliyotokea leo maeneo ya Ukonga Banana jijini Dar Es Salaam
Hii ndiyo nyumba iliyoteketea kwam moto na kusababisha vifo vya mama mdogo,baba mdogo,kaka,mjomba na watoto wa kaka wa kaka yake rapper Stereo

Taarifa hii ilithibitishwa na watu wake wa karibu akiwemo Nikki Mbishi na Songa
"Nimefiwa nababa mdogo(last born wa marehemu baba yangu)mama mdogo,kaka,uncle, na watoto wa kaka yangu,wameungua na moto usiku wa kuamkia leo''Nikki amenukuu ujumbe aliotumiwa leo na Stereo
Bado haijafahamika chanzo cha ajali ya moto huo jitihada za kumtafuta Stereo ziligonga mwamba kutokana na simu yake kutokuwa hewani
Swahili One inampa pole kwa msiba huo

NICK MBISH ATANGAZA KUACHA MUZIKI



Rapper Nikki Mbishi leo ametangaza kuwa ameacha muziki.

Rapper huyo ameelezea uamuzi wake wa kuachana na muziki kutokana na kutokunufaika chochote na kwamba hawezi kuendelea kuwa mtumwa mwa kiwanda cha muziki.
“I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry,” ametweet rappe huyo. “Nitaziachia tracks zangu zote ambazo hazijatoka for free then SITOINGIA TENA STUDIO kufanya wimbo(MUZIKI BASI).”
“The Industry is designed to frustrate the cats with high degrees of talents and intelligence. Ngwea,Langa,Geez mlale pema wanangu. I will remain as a music fan…and u guys need to find me some hip hop heads to listen to…asanteni,” ameongeza.
“Bora kuwa JAMBAZI kuliko MWANAMUZIKI. Tusije kushikiana bunduki bure maana milango ya kutoka kimaisha ni mingi na muziki ni burudani na biashara sio vita. Industry full of stupid and Illiterate but rich and famous. Mpaka lini tutauza UNGA kwa kivuli cha kuwa WASANII?”





RAY C AJIPANGA KURUDI NA ALBUM



Ujio Mpya wa Ray C Kudondosha Alabum

WAKATI asilimia kubwa ya wasanii wa Bongo Fleva wakiachana na mpango wa kutoa albamu, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amerudi rasmi katika muziki huo na wimbo wake mpya wa ‘Mshum Mshum’ huku akitamba kudondosha albamu.

Ray C alibainisha kuwa albamu yake itakuwa na nyimbo nane, ikiwa amemchukua mwaka mmoja na nusu kuiandaa mpaka kuikamilisha mwishoni mwa mwaka huu.

“Albamu yangu ina nyimbo nane na imechukua mwaka mmoja na nusu kuimalizia, najua mmesubiri sana na wengine walidhani sitarejea tena kwenye muziki, haya sasa bidada karudi tena kwa nguvu zote na Mwenyezi Mungu kabariki wimbo wangu unafanya vizuri na nimepokea pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki,” alisema Ray C.

Ray C aliyesifika kwa kuzungusha kiuno chake, alisema pongezi anazozipokea zinampa moyo wa kuzidi kufanya kazi nzuri zaidi.

“Eeh Mola niepushe na husda za binadamu, nifungulie milango yenye neema na baraka zote,” alisema Ray C.


KESI YA MADAWA ILIVYOHARIBU MIPANGO MIZURI YA CHID BENZ


Rapper Chidi Benz anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya, amesema kesi hiyo imeathiri kufanyika kwa video ya wimbo wake ‘Mpaka Kuchee’ aliyowashirikisha Diamond na AY.

Chidi alikuwa akiongea na Bongo5 jana kwenye uzinduzi wa video ya Wakazi ‘Wanawake wa Dar’.

“Video inakuja, bado sijaanza kufanya mazungumzo na AY wala Diamond ambao nipo nao kwenye hiyo project,” alisema. Video itafanyika hivi soon, haya matatizo ndo yameichewesha hii project.”

Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa tena December 1. Diamond na AY waliahidi kugharamia video hiyo.

Credit Bongo5

BLUE "KAMA SIO NGOMA YA "PESA" GAME INGEKUWA BASI


Akizungumza kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, rapper huyo alidai kuwa kama ngoma yake ‘Pesa’ ingebuma, angeachana kabisa na muziki na kuzamia Ulaya.
“Pesa kama Pesa ilikuwa ni project yangu ya mwisho,” alisema Kabayser. “Nilikuwa nimeshakata tamaa. Vitu vingi vilikuwa vinanisumbua, nilikuwa naplan kidogo niwakimbie watanzania nikatulie Uingereza. Nyumba yangu ilikuwa ipo kwenye finishing na itahitajika kama milioni 25 nimalize au 30 labda, nitaipata wapi hiyo hela, ikiwa mimi kazi yangu ni muziki? Ndioa Mungu akanisaidia nikatoa lile jiwe Pesa. Kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu ikawa ni balaa,” aliongeza.
“Sasa baada ya kupata ile pesa ikabidi nichague nimalizie nyumba yangu au nitoe video watu wanijue kama huyu ni Mr Blue! Kwahiyo hela yangu yote nawashukuru Serengeti Fiesta naomba niseme wazi kabisa ni watu ambao wamenisaidia hilo tatizo. Kwasababu hela hiyo yote niliipata kwenye Fiesta.”
Kuhusu video ya Pesa, Blue alidai kuwa Adam Juma alishoot video ya Pesa bure, bila kumpa chochote.
“Adam Juma from nowhere, ni mtu ambaye sikuwahi kufikiria nitafanya naye video. Nilishajaribu kutaka kufanya naye lakini mipango ikawa haikamiliki. Alinipigia simu mwenyewe namshukuru sana Adam Juma na Mungu akusaidie kwa kunipa video bure kabisa! Yaani video kila kitu bureee kabisa. Mimi nasema kuishi na watu kwa upendo ndo zimefanya hivyo ninaweza kusema ni zawadi.”
Credit: Bongo5.com

DIAMOND PLATNUMZ, AKIFANYA YAKE IRINGA TOWN.


Hivi ndivyo jinsi Msanii Diamond Platnumz alivyoweza kukonga nyoyo za mashabiki wa Iringa Town alipoenda kupiga show. Mbali na maskendo yake na Projects zake lakini Mashabiki lukuki walifurika Uwanjani.

JOKATE ALAMBA SHAVU


Baada ya Salama Jabir kupata shavu la kuwa na show kwenye kituo cha runinga cha Maisha Magic, sasa ni zamu ya Jokate Mwegelo. Mtangazaji huyo anatarajiwa kuongeza show yake ya tatu katika TV (baada ya The One Show ya TV1 na Top 10 Most ya Channel O), itakayoanza kuonekana kupitia Maisha Magic, December mwaka huu.

Jokate atashirikiana na mtangazaji maarufu wa Uganda, Gaetano Kagwa kuendesha kipindi hicho kiitwacho Beat the Challenge.
Beat the Challenge ni kipindi kitachokuwa kikihusisha mashindano ya familia 12 (baba, mama na watoto wao wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 17) wataokuwa wakihusika kwenye kazi mbalimbali na kuulizwa maswali kuhusu uelewa wa masuala mbalimbali.

Show hiyo itaanza kuonekana kupitia Maisha Magic (DSTV CHANNEL 161(, Jumamosi ya December 13, saa 2 na nusu usiku. Usaili utafanyika Nairobi November 22, Supersport Studios, Tanzania ni siku hiyo hiyo New Africa Hotel Dar es Salaam na Kampala utafanyika Silver Springs Hotel Kampala,kuanzia saa tatu asubuhi.

MIMI SI BIKIRA MARIA" LADY JAY DEE


Supastaa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee akipozi.

Kutoka moyoni! Wakati kukiwa na maneno mengi juu ya madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na prizenta maarufu Bongo wa Redio E-FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’, supastaa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee amefunguka kuwa naye si mkamilifu kwani siyo Yesu wala Bikira Maria.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wikiendi iliyopita Jide aliamua kuvunja ukimya kufuatia maswali ya mashabiki wake lukuki waliotaka afunguke kinachoendelea katika maisha yake.


“Watu wanategemea niwe kama Yesu au Bikira Maria? Siwezi, mimi ni mwanadamu tu. Hakuna aliye mkamilifu. Niacheni niishi maisha yangu bila stresi. Mwingine yeyote pia aishi maisha yake. Kila mmoja anatakiwa awe huru,” aliandika Jide.ted

PATA MUDA KUTAZAMA MAKAMUZI YA DIMPOZ KWA POZ NDANI YA SWEEDEN


Mkali wa bongo fleva, Ommy Dimpoz kama kawaida amewapagawisha mashabiki wa muziki nchini sweden ambapo alitoa burudani ya nguvu stockholm nchini sweden usiku wa kuamkia juzi

ALI KIBA, NYOTA INAYORUDI KWA KASI BONGO FLAVA.



Asilimia kubwa ya wapenda burudani Afrika Mashariki kwa sasa wanazungumzia kuhusu ujio wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Kiba, maarufu kama Alikiba.
Baadhi ya watu wamekuwa wakimlinganisha na mwanamuziki nyota kwa sasa Diamond Platnumz, ambaye naye kwa sasa yupo katika nafasi ya juu kimataifa kama ilivyokuwa kwa Alikiba miaka mitatu iliyopita.
Si kwamba ndiyo anaingia katika muziki, kwa watu wanaojua historia ya bongo fleva wanakumbuka kwamba kijana alikuwa tishio, kwani amekuwapo kwenye gemu tangu mwaka 2004 na kufanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimtambulisha uliojulikana kama ‘Cinderella’.
Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2004, alianza kujituma katika muziki na kufanikiwa kuandika wimbo wake wa kwanza, ‘Maria’. Mwaka huohuo Alikiba alianza kutengeneza albamu yake ya kwanza. Ilipofika mwaka 2005, alipata ofa ya kwenda kuchezea soka la kulipwa nchini Uganda, lakini baadaye aliachana na mpira ili kuendeleza kipaji chake cha muziki.
Mwaka 2007 alifanikiwa kuachia albamu iliyopewa jina la ‘Cinderela’, sambamba na kuachia wimbo huo redioni, ambao ulivuma na kusababisha albam hiyo kuuzika zaidi sokoni. Albamu hiyo ilikuwa ni kati ya albamu bora na iliyouza zaidi mwaka 2007 Afrika Mashariki.
Tangu hapo akaanza kupokea mialiko mingi kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi. Aliifanya Afrika Mashariki kumjua kwa muda mfupi kupitia vibao kadhaa vilivyokuwepo katika albamu hiyo kama MacMuga, Nakshi Mrembo, Njiwa na Mali Yangu.
2008 Alikiba aliachia albamu ya pili ‘Alikiba 4 Real’ na wimbo wa kwanza kuachia ulikuwa ‘Usiniseme’ na wakati huu alikuwa ameshatangaza jina lake Afrika Mashariki na kwingineko.
Albamu hiyo ilimfanya aanze kuaminika zaidi, mwaka huohuo akateuliwa na kushinda tuzo za Kilimanjaro Music Awards kupitia wimbo wake wa Cinderella.
Aliendelea kutafutwa kwa ajili ya kusakata kabumbu ambapo mwaka 2009, alipokea maombi kwa ajili ya kuichezea timu ya African Lyon ya Tanzania lakini alikataa na kuamua kuingia kwenye mitindo ambako hakukumchukulia muda mwingi.
Akutana na R Kelly
Ilipofika mwaka 2010 ndipo alipopata dili la One 8 na kufanikiwa kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa akiwamo R Kelly na wengine saba kutoka Afrika. Alipokutana na R Kelly alimsifu kwamba ana sauti nzuri na ya kipekee, hivyo kupendekeza aanze kuimba katika singo ya pamoja ‘Hands Across the World’. Kupitia wimbo huo, mtandao maarufu wa kimuziki duniani Billboard walilitangaza kundi la One 8 kama “Best Bet of 2011” kupitia orodha ya nyimbo zao bora duniani.
Mwaka huohuo Alikiba aliteuliwa na kushinda tuzo ya BEFFTA London Awards kama ‘Best International Artists’ (ACT) na kumshinda mwanamuziki 2 Face Idibia. Pia alifanikiwa kurudi na tuzo ya Sexiest Male Artist.
Historia yake
Alikiba alizaliwa Iringa Novemba 26, 1986 kutoka kwa mama yake Tombwe Njere na Saleh Omari. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wane katika familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba.
Muziki ni kati ya vitu ambavyo zimekuwa vikipendwa na mwanamuziki huyu tangu utoto wake.

Mwananchi.

CHEKI VIDEO "SHITOMBE" YA MSANII Y-TONY



CHID BENZI AFUNGUKA KUHUSU KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA



Imekua stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.

Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.

Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.
Kuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay >>> ‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake… tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji, tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema nakuona uko poa afya yako iko poa’
‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’

Kuhusu kukamatwa Aiport na dawa za kulevya Benz amesema >>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’
‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’

‘Sio kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe’

‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.


javascript://

NAY APATA MTOTO WA KIUME NA SIWEMA


Rapper Nay Wa Mitego na mchumba wake Siwema wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume tarehe 28/10/2014 ambaye ni siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa Ney Wa Mitego.

This is Why Ndoa ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu Itadumu


Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz aka Dangote ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri katika music industry ndani na nje ya Tzee, yote ni kujituma kwake kwa kutoa hit songs za nguvu kama ‘Moyo Wangu’, ‘Ukimuona’, ‘Mbagala’, ‘Number One’ and so many songz zimempelekea kufika hapo halipo, mapenzi ya Dangote na Wema Sepetu aka Madam Wema yalianza pale jina la Diamond lilipoanza ku-make headline kwenye media kutokana na ngoma zake nyingi kukubalika, since that day mapenzi yao yalishamili kwa kasi sana ingawa walikuwa wana mvutano wa kutoaminiana na kusababisha Diamond Platnumz kuachana na Wema Sepetu na kumchukua Peniel Mungilwa aka Penny, but they could not last long mapenzi yakarudi tena kwa Wema Sepetu yote kutokana na Diamond kumuona Madam Wema ni msaada kwake, na kuna tetesi kuwa Wema Sepetu ananyota kali sana ya mafanikio kiasi cha kumfanya Dangote kuona umuhimu wa kufunga ndoa, na hivi ndivyo vitu vitano vinavyofanya ndoa ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu kudumu kwa muda mrefu kama ndoa hiyo ikitokea.
Kutosikiliza maneno ya watu
tumeona ndoa nyingi sana za mastaa zinavunjika not only Tzee even abroad mfano kwa Bob Junior na Halima, Ezden na Dida yote ni kusikiliza sana maneno ya watu kuliko hisia zao wenyewe.
Diamond-Platnumz-59
Kusaidiana
Tukiangalia kwa Jay Z na Beyonce wanasaidiana sana kwenye kazi yao ili wazidi kuendelea ku-make mkwanja, so kwa Dangote na Wema wakiwa wanasaidiana watadumu na kufika mbali sana katika ndoa yao.
Super-couples-jay-z-beyonce-Diamond-Platnumz-Wema-Sepetu
Elimu
ukweli utabaki kuwa kweli Diamond Platnumz hana elimu ya kutosha kumzidi Wema Sepetu ila  ana mkwanja than Wema kitu kinachowafanya wazidi kujifunza kutoka kwa kila mmoja.
rp_diamond-wema.jpg
Kutambuana kitabia
kitu kitakachowafanya wazidi kudumu kwenye ndoa yao kila mmoja kumtambua mwenza wake coz wameshaumizana sana, kujivuna kwa sana na sasa watakua wanajua ni kitu gani wanapaswa wasifanye ili kutoumizana.
Diamond-Platnumz-62
Wote ni mastaa
Hii itawasaidia sana katika kuendeleza mshikamano wao katika ndoa kwa kujilinda kutokana na hadhi waliyonayo right now.
Wema-Sepetu-Diamond-Platnumz-Sasa-copyright-www-vibe-co-tz
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga