Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

ALIYEKUWA MENEJA WA DIAMOND PLATNUMZ ANENA MAZITO KUHUSU MSNII HUYO


Papa Misifa ( wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Cassim Mganga
Meneja wa zamani wa Diamond Platnumz, Msafiri Misifa maarufu kama Papa Misifa, amesema wasanii wengi wanashindwa kuendelea kutokana na kushindwa kuhifadhi wanachokipata.
Papa Misifa aliyewahi pia kuwa meneja wa Dully Sykes na Cassim Mganga, ameiambia Bongo5 kuwa Diamond ni msanii pekee aliyeweza kufuata mafunzo yake na ndio maana anaendelea kufanikiwa mpaka sasa.
“Tatizo kubwa wasanii sana wanapopata riziki wanashindwa kujipangilia. Na mafunzo mengi niliyompa Diamond ndo maana mpaka leo anajua kujipangilia mpaka pale alipofika. Wasanii wanashindwa kupangilia pesa zao. Tatizo wanapopata pesa wanabadilika. Ukitaka kujua tabia ya mwanadamu ngoja apate pesa ndo utajua tabia yake,” amesisitiza.
“Wasanii wengi hawalengi kufanya vitu vya maendeleo, wanalenga kufanya starehe kwenye baa. Ndio maana watu wanasema wanamuziki wa zamani wamefulia ni kweli kwa sababu hawakujipanga. Hawakutambua kesho yao, wewe unafikiri kwanini Diamond anaiogopa kesho yake? Ni kutokana na maisha yalivyo ukipata nafasi itumie ipasavyo.”

MC AMKERA WAZIRI FANELA KATIKA SHEREHE YA KUMPONGEZA LUIZA MBUTU


Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mkangara (kushoto) akiwa na Luiza Mbutu.
 
MSHEHERESHAJI wa onyesho la Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kumpongeza mwimbaji kiongozi Luiza Mbutu kutimiza miaka 16 ya kuifanyia kazi mfululizo bila kuhama, Sakina Lyoka, Jumamosi iliyopita alimkera mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mkangara baada ya kukosea kutamka vizuri cheo chake. 
 
Mtangazaji huyo wa televisheni, wakati akimkaribisha, alimtambulisha kama Waziri wa Utamaduni, kitu ambacho kilimkera kiasi cha kumnyang’anya kipaza sauti ili kumsahihisha.
“Jamani mimi naitwa Fenela Mkangara, ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na siyo Waziri wa Utamaduni kama alivyonitambulisha huyu Mc,” alisema Waziri huyo ambaye baadaye alimpongeza Luiza kwa kudumu kwa muda wote bila kuhama na kuonyesha nidhamu kazini.

KWELI BODY GUARD WA DIAMOND NI NOUMAH, ANGALIA MBWEMBWE ZAKE HAPA.


Kwa tetesi tunazosikia huyu jamaa ndo mlinzi binafsi wa wasanii wa hapa Tanzania anayelipwa ghali zaidi. kuanzia mshahara na marurupu mengine kiasi kwamba anaishi kama majuu vile. Si haba kama shukrani yake kuendelea kukitunza kibarua chake kwa kuji keep well fit kila mara.

Angalia baadhi ya picha zake hapo chini ikiwa kikazi zaidi:-




MIAKA 10 YA MUZIKI KWA D'BANJ, ASINDIKIZWA NA AMBER ROSE.


D'Banj akihojiwa.
D'Banj akimnong'oneza jambo Amber Rose.
Amber Rose na D'Banj katika…
D'Banj akihojiwa.
D'Banj akimnong'oneza jambo Amber Rose.
Amber Rose na D'Banj katika pozi.
D'Banj akifurahia jambo na Amber wakati wa sherehe hizo.
MWANAMUZIKI mahiri wa Nigeria, D'banj jana amesherehekea kuadhimisha miaka 10 katika muziki ambapo sherehe hizo ziliongozwa na mwigizaji na mwanamitindo maarufu kutoka nchini Marekani, Amber Rose.
Video ya mahojiano ya D'Banj na HipTV kuhusu maadhimisho hayo na kwa nini alimchagua Amber Rose kuongoza sherehe.



Mastaa mbalimbali wakiwemo Ice Prince, Kayswitch, Seyi Law, Orezi, Toke Makinwa na wengineo walihudhuria sherehe hizo zilizofanyika Ocean View jijini Lagos, Nigeria jana.

NICK MBISH ATANGAZA KUACHA MUZIKI



Rapper Nikki Mbishi leo ametangaza kuwa ameacha muziki.

Rapper huyo ameelezea uamuzi wake wa kuachana na muziki kutokana na kutokunufaika chochote na kwamba hawezi kuendelea kuwa mtumwa mwa kiwanda cha muziki.
“I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry,” ametweet rappe huyo. “Nitaziachia tracks zangu zote ambazo hazijatoka for free then SITOINGIA TENA STUDIO kufanya wimbo(MUZIKI BASI).”
“The Industry is designed to frustrate the cats with high degrees of talents and intelligence. Ngwea,Langa,Geez mlale pema wanangu. I will remain as a music fan…and u guys need to find me some hip hop heads to listen to…asanteni,” ameongeza.
“Bora kuwa JAMBAZI kuliko MWANAMUZIKI. Tusije kushikiana bunduki bure maana milango ya kutoka kimaisha ni mingi na muziki ni burudani na biashara sio vita. Industry full of stupid and Illiterate but rich and famous. Mpaka lini tutauza UNGA kwa kivuli cha kuwa WASANII?”





P SQUARE, WAMPOTEZA BABA YAO



Mapacha kutoka nchini Nigeria Peter Okoye&Paul Okoye P- Square pamoja na kaka yao Jude Okoye,Jumatatu ya Nov 24 wamempoteza mzazi aliyebakia ambaye ni baba yao mzazi hii ni miaka miwili tangu afariki mama yao.

tovuyi ya www.Naij.com imesema kuwa Mr.Okoye alikua akisumbuliwa na maumivu ya Goti baada ya kufanyiwa upasuaji ingawa hali iliripotiwa kuendelea vizuri.
psqdad

MKALI WA KUCHEZA NA MAPIKIPIKI TOKA SOUTH ATUA DAR




MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia pikipiki Bian Capper kutoka nchini Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.

Akizungumza jana kabla kuonesha umahiri huo mchezaji wa pikipiki ambaye ni raia wa Afrika Kusini anayefanya ziara katika nchi za Afrika kwa udhamini wa kinywaji cha Redbull atakuwa nchini kwa ziara za ya maonesho ya kuonesha namna ya kucheza na pikipiki kwa siku tatu.

Onyesho la kwanza lilianza jana kwenye viwanja vya Coco beach , leo Jumapili atakuwa Mlimani City na kesho Jumatatu atakuwa katika eneo la Ubungo Tanesco ambako litakuwa onyesho lake la mwisho.

Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.


Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.

“Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .

Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote ni ya wazi.

KWA NINI MAKAMUZI YA MWANA FA JMOSI YALIFANA HUKO TANGA


Tunajua kuhusu umahiri wake kwenye uandishi wa mashairi pamoja na kumiliki stage, amedumu kwenye game tangu siku ya kwanza na bado anabakia kuwa bora kila siku ndio maana siku ya Jumamosi Oktoba 31, rapa mkongwe, Hamis Corleone Mwinjuma a.k.a Mwana FA aliacha historia ya aina yake Tanga kwenye ile show ya nguvu iliyoandaliwa na Vodacom.
Kabla ya kufanya show hiyo iliyopewa jina la ‘Mcheza Kwao Hutuzwa’ iliyofanyika katika ukumbi wa La Casachika, taarifa kutoka kwenye blog ya Issa Michuzi zimesema Mwana FA alitembelea kituo cha yatima cha Diana kilichopo Tanga na kukabidhi zawadi ya jezi kwa niaba ya kampuni simu ya Vodacom Tanzania.
Mwana FA Tanga
Mwana FA akikabidhi zawadi ya Jezi kwa Niaba ya kampuni ya Vodacom Tanzania kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Diana, Tanga.
Mbali na hilo, msanii huyo alikabidhi zawadi kwa mshindi wa simu ya Vodafone Smart alipotembelea duka la Vodacom lililopo barabara ya tatu, Tanga.
Mwana FA II
Mwana FA akipiga ‘Selfie’ na mshindi wa Vodafone Smart, Kika Martin Joseph baada ya kumkabidhi zawadi ya simu hiyo kwa niaba ya kampuni ya Vodacom Tanzania.

RONALDO AZIDI KUKIMBIZA, ASHIKA NAMBA MOJA KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI NA WENZA WANAOVUTIA ZAIDI, ANGALIA 9 WALIOSALIA.


Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na mpenzi wake ambaye pia ni mwanamitindo, Irina Shayk, wamechaguliwa kuwa kapo yenye mvuto zaidi miongoni mwa wachezaji wa mpira wa miguu na wap#nzi wao, hii ikiwa ni mbele ya David na Victoria Beckham.

Ronaldo na patna wake walipata 18% ya kura zote kwenye utafiti uliofanywa na mtandao wa BetNegotiator.com.

Shuka chini upate listi kamili na picha zao....

Top 10 ya kapo zenye mvuto kwa wachezaji soka

1. Cristiano Ronaldo and Irina Shayk – 18 %

2. David Beckham and Victoria Beckham - 14 %

3. Lionel Messi and Antonella Roccuzzo – 11 %

 4. Steven Gerrard and Alex Gerrard – 9 %

5. Gerard Pique and Shakira – 8 %

6. Frank Lampard and Christine Bleakley – 7 %

7. Iker Casillas and Sara Carbonero – 6 %

8. Wayne Bridge and Frankie Sandford – 5 %

9. Gareth Bale and Emma Rhys-Jones – 4 %

10. Peter Crouch and Abbey Clancy – 3 %
DC.

ETI HIZI NDO NYWELE ZA ASILI ZA NICK MINAJ, MCHEKI HAPA.


Rapa huyu wa kike hapo jana kupitia ukurasa wake wa Instagram alionyesha nywele zake za asili zilizoonekana kuwa ni ndefu (utaziona nywele hizo hapo chini) na ni kweli kwamba ni nywele zake Nicki Minaj.

Mcheki zaidi kwenye picha hapo chini...

Unaonaje zimempendeza sana au....?

DC.

SNURA ALIA NA WABAYA WAKE, WANAOTAMANI AANGUKE.


STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Snura Mushi.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli wowote.

DR CHENI APANIA KUIRUDISHA KAOLE SANAA GROUP.


MWENYEKITI Msaidizi wa Bongo Movie Unity, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amesema amekumbuka na kutamani kurudisha Kundi la Sanaa ya Maigizo la Kaole ‘Kaole Sanaa Group’ liwe na nguvu kama zamani.
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’.
Dk. Cheni alisema japo kundi hilo limeonekana kupoteza mvuto wake wa awali, lakini anaamini wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu kwa sasa wametoka katika kundi hilo maarufu.
Hata hivyo, pamoja na kupotea kwa kundi hilo, Dk. Cheni anatamani sana kulirejesha kwenye ulingo wa sanaa na kwamba kuna mikakati anayoiandaa ili kukamilisha azimia hiyo.
“Naitamani Kaole ya zamani, nahisi kama kuna vionjo vinakosekana siku hizi. Wasanii wengi wenye majina makubwa kwa sasa wametoka kwenye kundi hilo, lakini nitajitahidi kulirudisha, naamini nitafanikiwa,” alisema Dk. Cheni.

BAADA YA KUJIINGIZA KIAINA NA SIASA, WANA BONGO MOVIES WAMTAKA STEVE NYERERE AJIUZULU.


Hali si shwari katika klabu ya wasanii wa filamu za Kibongo, Bongo Movie Unity ikidaiwa kuwa baadhi ya ‘memba’ wake wanashinikiza mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzulu.
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Habari zilizoifikia Stori Extra wikiendi iliyopita zilidai kuwa, baadhi ya wasanii wa klabu hiyo akiwemo mwenyekiti huyo walilamba mshiko kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa CCM mkoani Mbeya ili wamfanyie kampeni katika uchaguzi ujao jambo ambalo wenzao walilipinga vikali kwa kuwa wao hawajihusishi na siasa bali wasanii na jamii.
Alipotafutwa Steve kujibu tuhuma hizo hakupatikana lakini katibu wake, William Mtitu alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.
GPL.

MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA




Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu ) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!

CHEKI DIAMOND ALIVYOPAGAWISHA MABINTI WA KENYA HAPA, ANGALIA PICHA ZAIDI YA 20 HUMU.

 
 
 Dancer wakiongozwa na Moze iyobo,wakafungua pazia la burudani

 Weka mbalii na watotto















Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga