Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

UNDANI WA KIFO CHA ASKARI ALIEKATWA MAPANGA


Marehemu, Koplo Joseph Isaac Swai (27) enzi
za uhai wake.
KILA nafsi itaonja mauti! Maneno ya mwisho
ya Koplo Joseph Isaac Swai (27) aliyeuawa
kwa kucharangwa mapanga na Tisi Sirili
Mallya (29) katika zoezi la kumwokoa mtoto
Valerian Tisi (miezi nane) asichinjwe,
yanazidi kuzua simanzi, Uwazi limenasa
mkononi.Katikati ya wiki iliyopita, eneo la
Chang’ombe mjini hapa, Koplo Swai
aliyekuwa akitumia namba ya uajiri wa
polisi G. 7168 alikatwakatwa mapanga
sehemu mbalimbali za mwili na Mallya kisa
ni afande huyo kwenda nyumbani kwa
mtuhumiwa huyo na kumtaka asimuue
mwanaye ambaye alikuwa katika hatua za
mwisho za kumchinja akiwa
amemning’iniza.
Mtuhumiwa saa chache kabla ya kukata
roho.
YA SIKU TATU KABLA
Akizungumza na Uwazi kwenye msiba wa
Koplo Swai mjini hapa, rafiki mmoja wa
karibu huku akiomba jina lake lisitajwe
gazetini kwa sababu yeye si msemaji wa
familia, alisema:
“Bado naumia sana, unajua siku tatu kabla
ya hili tukio, marehemu aliniambia hajisikii
sawasawa. Nilimuuliza kama anaumwa
akasema hapana, ana matatizo ya kifedha
akasema si sababu, ila hajielewielewi tu.
“Mimi nilijua ni hali ya mwili, kuna wakati
unakuwa mzito wakati mwingine mwepesi
lakini baada ya kuuawa sasa ndiyo nimejua
kwa nini afande Swai alikuwa akisema
hajisikii sawasawa.”
ALISEMA AMEWAMISI NDUGU ZAKE
Rafiki huyo alisema siku ya tukio, muda
mchache, Swai alimpigia simu na
kumwambia anatamani kwenda kwao
(Kilimanjaro) kusalimia ndugu zake, anahisi
kuwamisi sana. Pia aliniambia alikuwa
studio moja ya redio mjini Dodoma (Dodoma
FM Radio) ndiyo amerejea.”
AKATA SIMU BAADA YA KUITWA
Akizungumzia namna tukio la afande huyo
kukatwakatwa mapanga hadi kifo, rafiki
huyo ambaye naye ni polisi, alisema:
“Wakati tukizungumza kwa simu, ghafla
akasema atanipigia baadaye kuna mtu
anapiga simu. Sikuwa na maswali juu ya hilo
wala sikushtuka mpaka nilipokuja kusikia
kuwa, amekumbwa na mauti kwa njia hiyo
ya kikatili.”
IGP Mangu akiuaga wwili wa marehemu,
Koplo Joseph Isaac Swai wakati wa mazishi.
ALICHOELEZEWA RAFIKI HUYO
Kwa mujibu wa rafiki huyo, Swai alipigiwa
simu na Mtendaji wa Mtaa wa Chang’ombe,
Oliver Balthazar akimwambia kuna mzazi
(Mallya) anamtesa mwanaye na huenda
angemuua kwani tayari alishamning’iniza
kichwa chini na panga liko
mkononi.“Niliambiwa mtendaji huyo
alimpigia Swai akiamini ni polisi hivyo
angeweza kunusuru uhai wa mtoto huyo
ambaye alikuwa akilia kwa sauti ya juu.”
ALIGOMA KWENDA
Ilizidi kudaiwa kuwa, baada ya afande huyo
kuambiwa taarifa za baba kutaka kumchinja
mwanaye, aligoma akisema, ‘siwezi kwenda,
siku hizi raia wanaua sana polisi.’
Baada ya sekunde kadhaa, inadaiwa Swai
akasema: “Oke, poa nitakwenda maana ni
majukumu yangu.”
ALIONGOZANA NA WATU WAWILI
Afande Swali alitoka nyumbani kwake
mpaka kwenye ofisi ya mtendaji huyo na
kutoka naye. Aliongozana na mtendaji na
mtu mwingine ambaye anashughulika na
kitengo cha kuhudumia watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.
Njiani, habari zinasema, afande Swai
alikuwa akishangaa ni baba wa aina gani
mwenye dhamira ya kumshika mtoto wake
na kumtesa na kutoa kauli za kumchinja.
Inadaiwa alisema:
“Hivi huyo baba ni mzima kweli? Mwanao
wa kumzaa umtese, useme utamchinja! Kwa
kosa gani kubwa?”
HALI YA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA
Ikaendelea kuelezwa kwamba, Koplo Swai
alipofika nyumbani hapo alimkuta Mallya
bado anamtesa mtoto wake na safari hii
mtoto alikuwa halii tena.
Inaelezwa kuwa, Swai aligonga mlango na
kujitambulisha lakini mtuhumiwa
alipofungua mlango alionekana
amemning’iniza mtoto wake kichwa chini,
miguu juu huku akisema anamchinja.
“Swai alimsihi Mallya kuachia panga chini
akitumia lugha ya upendo lakini Mallya
akasema lazima amchinje. Ndipo Swai akawa
anamsogelea lengo lake lilikuwa ni
kumrukia mtuhumiwa huyo kwa
kumkumbatia ili amnyang’aye panga.”
KAMA SI MGUU WA KUSHOTO
“Wakati anamsogelea, Swai alipanua mikono
tayari kwa kumrukia na kumkumbatia.
Lakini mikono ikiwa bado hewani, mguu wa
kushoto uliteleza hivyo safari ya kumfikia
Mallya ikaishia hapo, maskini jamaa
akaenda chini.
“Pengine kwa hasira za kuona afande huyo
alitaka kuingilia dhamira yake, Mallya
alimtupa mtoto chini na kuanza
kumcharanga mapanga koplo huyo,”
kilisema chanzo kingine.
ALIPIGA MAGOTI ASIUAWE
Habari nyingine zinasema, wakati Mallya
ameshapeleka mapanga mwilini, Swai
alipiga magoti na kuomba asimuue kwa vile
alikuwa ana mipango ya ndoa
(haikufafanuliwa), lakini mtuhumiwa huyo
hakumsikiliza.
MTENDAJI, YULE MTU MWINGINE
Inaelezwa kwamba, baada ya kuona Mallya
anamcharanga mapanga Swai bila huruma,
yule mtendaji na yule mtu mwingine
aliyekuwa naye walitimua mbio mbali huku
wakianza kupiga kelele za kuomba msaada.
MAMA AMKWAPUA MTOTO
Huku Mallya akizidi kumcharanga mapanga
afande huyo, mama wa mtoto alimkwapua
mwanaye aliyekuwa chini na kukimbia naye
ambapo mpaka sasa amefichwa
kusikojulikana.
MAVAZI SIKU YA MAUAJI
Siku hiyo, Mallya ambaye ni maji ya kunde
alivaa suruali ya ‘jinsi’ rangi ya bluu, fulana
rangi ya bluu iliyoiva na kapelo nyeupe.
KUHUSU MTUHUMIWA
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma, SACP David Misime, mtuhumiwa
Mallya aliuawa na wananchi wenye hasira
kali usiku wa Jumatano iliyopita, saa tano
akiwa na panga alilofanyia mauaji ya afande
huyo.
Kamanda Misime alisema baada ya Mallya
kutekeleza mauaji hayo alikimbilia
mafichoni, lakini ilipofika saa tano raia
walimuona maeneo ya Mtimkavu Maili Mbili
akiwa na panga alilotumia kumuua Koplo
Joseph huku nguo zake zikiwa zimetapakaa
damu.
KUMBUKUMBU MBAYA
Kamanda Misime alisema katika
kumbukumbu za kipolisi, mwaka 2006,
Mallya alifungwa miaka mitatu jela kwa kosa
la kujeruhi. Mwaka 2009 alifungwa tena,
miezi sita kwa kosa la kutishia kuua.
SWAI AZIKWA
Mwili wa marehemu Swali ulisafirishwa
kwao Moshi, Kilimanjaro, Februari 5 na
mazishi kufanyika Februari 7, mwaka huu.
Mungu ailaze pema peponi, roho ya
marehemu. Amina.

AJALI YA MOTO ALIVYOTEKETEZA NDUGU WA FAMILIA MOJA AKIWEMOAFISA MSTAAFU WA JWTZ

Watu sita wa familia moja akiwamo Kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), wamekufa papo hapo baada ya kuteketezwa kwa moto  jijini Dar es Salaam.

Janga hilo la moto limetokea jana saa 10:30 alfajiri katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, wilayani Ilala.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kuwa moto huo ulizuka ghafla katika nyumba inayomilikiwa na mstaafu huyo wa Jeshi, David Mpira anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 na 60.

Alisema wengine waliokufa katika ajali hiyo ni mke wa marehemu, Selina Yegela anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50 na 55, ambaye pia ni mstaafu wa iliyokuwa Kampuni ya Kuhudumia Ndege (DAHACO), sasa Swissport.

Aidha, moto huo pia umesababisha vifo vya watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 30 ambao ni, Lucas Mpira na Samwel Yegela.
  
Kamanda Nzuki alisema wajukuu wa marehemu nao wamekufa katika ajali hiyo, ambao ni Selina Emmanuel (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu na Pauline Emmanuel (3), mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya Tumaini iliyopo Kitunda.

“Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, tunaendelea na uchunguzi na tunashirikiana na Shirika la Umeme (Tanesco) ili kubaini chanzo kilichosababisha moto huo,” alisema Nzuki.

Maiti wamehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na uchunguzi bado unaendelea.

FAMILIA YA RAPPER STEREO YATEKETEA KWA AJALI YA MOTO


Mama mdogo, Baba Mdogo,kaka yake Mjomba na watoto wa Kaka yake Rapper Stereo wamepoteza Maisha kwenye ajali ya moto iliyotokea leo maeneo ya Ukonga Banana jijini Dar Es Salaam
Hii ndiyo nyumba iliyoteketea kwam moto na kusababisha vifo vya mama mdogo,baba mdogo,kaka,mjomba na watoto wa kaka wa kaka yake rapper Stereo

Taarifa hii ilithibitishwa na watu wake wa karibu akiwemo Nikki Mbishi na Songa
"Nimefiwa nababa mdogo(last born wa marehemu baba yangu)mama mdogo,kaka,uncle, na watoto wa kaka yangu,wameungua na moto usiku wa kuamkia leo''Nikki amenukuu ujumbe aliotumiwa leo na Stereo
Bado haijafahamika chanzo cha ajali ya moto huo jitihada za kumtafuta Stereo ziligonga mwamba kutokana na simu yake kutokuwa hewani
Swahili One inampa pole kwa msiba huo

WIVU WA MAPENZ WAMPONZA DEREVA BODABODA.



MH! ‘Haga gangi’ (haya mengine)!  Simon Manase (22) ambaye ni dereva wa bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Nguyami, wilayani Gairo mkoani hapa amecharangwa mapanga mwilini na kukatwa mkono wa kulia na mtu aliyetajwa kwa jina la Frank akidai kumfumania na mkewe vichakani.
Kijana Simon Manase (22) aliyecharangwa mapanga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu vichakani.
Ishu hiyo inadaiwa kujiri usiku mnene wa Oktoba 31, mwaka huu kwenye Kijiji cha Nembo mpakani mwa Gairo na Kilosa katika muziki wa mitaani maarufu kwa jina la ‘kigodoro’.Mwandishi wetu alipiga gia hadi kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kuzungumza na mashuhuda, viongozi wa kata, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Berega na Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila.
“Siku ya tukio tulikuwa kwenye shereha ya mwenzetu, mwanae amevunja ungo hivyo nyumbani kwake aliweka muziki wa kigodoro, cha ajabu ilipofika saa sita usiku DJ wa muziki, Alex Munga alitutangazia kwamba kuna watu wanapigana mapanga baada ya kufumaniana kwenye kichaka.
Simon Manase akiuguza majeraha katika Hospitalini ya Berega mkoani Morogoro.
“Tulikimbilia kule. Kufika tukamkuta Frank akimcharanga mapanga Simon akidai amemfumania na mkewe ,”alisema shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Joseph.Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nembo, Musa Bruno alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye kijiji chake.
“Ni kweli, siku hiyo, mimi na msaidizi wangu, Daudi Kisonela na mgambo wa kijiji tulifika eneo la tukio na kushuhudia Simon akivuja damu mwilini huku mkono wake wa kulia ukining’inia nusu hadi mfupa wa ndani ukionekana baada ya kupigwa mapanga na Frank akidai kamfumania na mkewe,” alisema mtendaji huyo.
Akaendelea: “Tuliwaweka kikao, tulimhoji mke akasema mumewe alikurupuka kumcharanga mapanga mtuhumiwa kwani si kweli.
Majeraha ya usoni ya panga alilopigwa Simon Manase.
“Kwa kauli ya mama huyo tulimtia hatiani Frank, tukamkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Dumila, cha ajabu wakati sisi tukitafuta usafiri, huku nyuma mtendaji wa kata alimuachia huru Frank huku akitukabidhi panga lenye damu kama ushahidi.”Akizungumza kwa tabu na mwandishi wetu katika wodi ya wanaume Hospital ya Misheni ya Berega, Gairo, Simon alisema:
”Siku ya tukio nilifika kwenye kigodoro kwa lengo la kusaka abiria, mtu mmoja aliniambia nimkodishe pikipiki aendeshe mwenyewe, kuna watu anataka kwenda kuwafuata baada ya makubaliano ya bei nikamkabidhi pikipiki yangu na mimi nikamsubiri palepale.
Majeraha ya kichwani na begani aliyopata Simon Manase.
“Ilipotimu saa 6 nikaona jamaa harudi, nikaamua kuondoka nikiamini nitakutana naye njiani. Nilipofika mbali kidogo nikamuona Frank akiwa na panga mkononi huku akinishutumu kwamba natembea na mkewe, nilijaribu kubisha, akarusha panga la kichwa katika hatua ya kujihami nililipanchi na mkono ambapo alinikata mkono.
“Mkewe naye alikuwepo, alipojibu si kweli alimpiga,”alisema kijana huyo.
Juhui za mwandishi wetu kutaka kuzungumza na Frank zilikwama kufuatia mtuhumiwa huyo kutimua mbio akiogopa chombo cha habari.
Mganga mkuu wa hospitali aliyolazwa Simon, Alfred Chiponda alithibitisha kumpokea mgongwa huyo.
Mkuu wa kituo cha polisi, afande James Charles alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema vijana wake wanamsaka  Frank.

BASI LAUA SABA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI



Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
Basi hilo likiwa limepinduka.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.
ZAIDI ya watu saba wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi la Super Aljabir linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mahenge mkoani Morogoro kugongana na treni maeneo ya Kiberege karibu na Ifakara, Morogoro jioni hii.
Ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likijaribu kuwahi kuvuka reli kabla ya treni kupita.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga