Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

MAIMARTHA AWAPONDA MAJIMAMA WANAOTOKA NA SERENGETI BOYS.




Mtangazaji ambaye pia ni mjasiriamali, Maimartha Jesse amewaponda mastaa wa Bongo Muvi wanaotoka kimapenz na vijana wadogo ‘Serengeti Boys’ akidai kuwa wanajichoresha.
Mtangazaji ambaye pia ni mjasiriamali, Maimartha Jesse.
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Mai alisema anawashangaa baadhi ya mastaa hao kutoona aibu kutangaza kuwa wanatoka na Serengeti Boy huku wakionekana maeneo mbalimbali wakiponda raha.
“Mimi mpaka naogopa na nawaonea huruma kwani hali ni mbaya jamani, watoto wadogo wanatoka na wasanii waliowazidi sana kiumri, yani imekuwa ni kama fasheni sasa, huku ni kujichoresha,” alisema Mai.

Gumzo kuhusu Sakata la Mzee Majuto Kuoa kwa Siri Dar!!!!

-->


Chande Abdallah na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, kuna taarifa kwamba gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ almaarufu mzee Majuto amefunga ndoa ya siri ndani ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Tukio hilo limetokea Julai 8, mwaka huu pande za Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo mzee Majuto alifunga ndoa na msichana mbichi aitwaye Rehema Omary.
Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.
Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.
Muoaji akaongozana na wakwe na mashehe kwenda Msikiti wa Aqswa uliopo jirani ambapo ndoa hiyo ilifungwa kisha wakarudi nyumbani ambako cherekochereko ziliendelea.
Paparazi wetu alifanikiwa kujipenyeza na kuonekana kama mmoja wa ndugu na kushuhudia mzee Majuto akikabidhiwa mkewe.
Baada ya robo saa, mzee Majuto na mkewe walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuingia kwenye gari hilo aina ya Noah.
Paparazi wetu alipojaribu ‘kufotoa’ picha kadhaa, alisababisha kuzuka kwa  kizaazaa kwa wanandugu waliomlazimisha kuzifuta picha hizo ambapo alitii.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu walijaribu kuzungumza na mzee Majuto kwa simu lakini kazi haikuwa nyepesi kwani simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Alilipopigiwa simu mpambe wa bwana harusi, Barafu, alisema hana la kusema na kusisitiza atafutwe mzee Majuto.
Mwandishi wetu alirudi Mbagala kwa mama wa biharusi ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa atafutwe mzee Majuto.
Siku hiyohiyo mzee Majuto alipokea simu na kuulizwa kama ni kweli amefunga ndoa na msichana aitwaye Rehema.
Katika hali ya kushangaza, mzee Majuto alicheka sana na kudai kwamba utafiti wake umekakilika. Alipohojiwa ni utafiti gani alisema:
“Nilikuwa nafanya utafiti wa kutaka kuigiza filamu ya ndoa ya siri ndiyo maana nikaenda kule Mbagala lakini sasa nimeamini kwamba hakuna ndoa ya siri,” alisema mzee huyo huku akikwepa kukubali.
Habari zinasema kwamba mzee Majuto anakwepa kukubali kwamba amefunga ndoa kwa kumhofia mkewe wa kwanza ambaye amemuacha jijini Tanga.

Source: GPL

Kajala Atimkia South Africa, Wadau Wamohofia na Madawa, Mwenyewe Asema ni kupunguza Stress Tu!!!


Imelda Mtema
MWIGIZAJI Bongo, Kajala Masanja ambaye miezi michache iliyopita alichomoka nyuma ya nondo za Segerea kwa dhamana, ametimkia nchini Afrika Kusini kupunguza mawazo.
Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, Kajala alitupia picha zake mbalimbali katika mtandao wa Instagram zikimuonyesha akiwa nchini humo na kusindikiza na ujumbe wa maandishi uliosomeka kuwa amekwenda kwa ajili ya kubadilisha hali ya hewa kwani toka akumbwe na matatizo, hajapata mtoko wa kupumzisha akili.
“Nimekuja kubadilisha hali ya hewa  maana nimetoka kwenye matatizo, sijapata kabisa muda mzuri wa kuipumzisha akili yangu hivyo nimeona bora nije huku kupumzika kidogo kisha nitarejea nyumbani,” alisema Kajala.

Source: GPL

Za mwizi, 40.!!! Kibaka achezea kipigo huko Kawe, ni baada ya kuruka geti.


Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.…
Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.
Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi waliochoshwa na wizi.
...Akiendelea kusulubiwa kabla ya kupelekwa polisi.
Baada ya kulainika akawa anapelekwa polisi.
Kutokana na kipigo jamaa huyo alianguka hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa.

MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Source:GPL

Rafiki Wa Sharo Milionea Adaiwa Kudhulumu Mali za Marehemu

-->


MALI zilizoachwa na aliyekuwa staa wa vichekesho Bongo, marehemu Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Milionea’ zinadaiwa kudhulumiwa na rafiki yake wa karibu aliyejulikana kwa jina moja la Suma, Risasi Jumamosi lina  mkanda wote.


MADAI
Chanzo chetu kilichoongea na gazeti hili Julai 25, mwaka huu kilisema Suma anadaiwa kudhulumu mali za Sharo kufuatia kupewa madaraka ya kufuatilia na kuuza baadhi ya vitu bila fedha kumfikia mama wa marehemu, Zainabu Mkieti.

MAMA WA SHARO AFUNGUKA
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Alhamisi iliyopita, mama huyo alikiri kuonekana kwa njama za Suma kudhulumu mali hizo likiwemo gari aina ya Opa lenye namba za usajili T 879 CAR na shilingi milioni 1. 2 za seti ya sofa alizonunua marehemu siku chache kabla ya kifo.

AZUNGUMZIA GARI
“Kweli nahitaji msaada ili nifanikishe kupata mali za mwanangu kwani kuna mambo hayaeleweki, kikubwa ni gari ambalo baada ya arobaini tulimpa Suma akaliuze kwa shilingi milioni kumi na moja na anipe fedha hizo lakini hadi sasa sijaona hata shilingi mia. Arobaini ya Sharo ilikuwa Januari 2013.

FEDHA ZA MASOFA
“Ukiachilia mbali gari, kuna fedha za masofa shilingi milioni moja na laki mbili sijazipata hadi leo, Suma aliahidi kunipa baada ya kuuza masofa hayo kwa dada yake na nimeshajaribu kuzungumza naye lakini hakuna majibu ya ukweli.
“Kabla ya Tuzo za Kili Music, Juni, mwaka huu, mimi nilikuja Dar na nikaongea na Suma na mama yake kuhusu fedha hizo, nilipomuuliza kuhusu gari, Suma akasema hataliuza na badala yake baada ya siku mbili angenitumia fedha lakini hadi leo hii simpati kwenye simu.

FEDHA ZILIKUWA ZITUMIKE KWA UJENZI
“Nakosa njia rahisi ya kuzipata fedha hizo maana huyu Suma naona kama mjanja, nilikuwa nataka kuanza ujenzi  wa nyumba kwenye kiwanja alichokiacha marehemu lakini naona kama muda unakwenda,” alisema mama mzazi wa Sharo.

MAJIBU YA SUMA
Suma baada ya kupatikana kwenye simu yake ya kiganjani na kusomewa mashitaka hayo, alidai ameshaongea na mama Sharo lakini alisafiri na ni kweli alikuwa hapatikani kwenye simu.
“Mbona nimeshaongea na mama na mambo tumeyaweka safi, ujue nilikuwa South Africa (Afrika Kusini) nina kama wiki tatu tangu nirudi na kusema kweli sijawasiliana na mama Sharo ila tutamalizana tu mambo yakiwa vizuri,” alisema Suma.

KUMBUKUMBU
Sharo Milionea alifariki dunia kwa ajali ya barabarani Novemba 19, 2012 iliyotokea kwenye Kijiji cha Songa Maguzoni, Muheza Tanga akiwa ndani ya gari aina ya Harrier lenye namba za usajili T 378 BVR likitokea Dar es Salaam kwenda Tanga.
Alizikwa Novemba 23 kijijini kwao, Lusanga, Muheza, Tanga.

Source: GPL

Mwanafunzi Ashikiwa Uchawi, Akutwa na zana kibao za uchawi huku akiwa na Nguo ya Ndani Tu!!!


Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, duniani kuna uchawi! Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Pasco (21) ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Samaritan iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara amekutwa getini kwa kaka’ke, Edward Raphael akiwa amefungwa kamba na matunguri.
Denti akiwa amaefungwa kamba
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni huko Yombo-Buza jijini Dar na kuibua sekeseke la aina yake kutokana na mazagazaga ya kichawi aliyokutwa nayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Pasco alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni huku akiwa na nguo ya ndani pekee.
Habari zilieleza kuwa pia kijana huyo alikuwa amepakwa unga na kuandikwa maandishi ya Kiarabu mwilini huku kiunoni akiwa na shanga, hali iliyowashangaza wengi.
Polisi akiwa eneo la tukio
Akizungumza na wanahabari wetu juu ya tukio hilo, kaka wa kijana huyo alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, wiki mbili zilizopita ambapo aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake lakini alipofungua geti alishangaa kumuona mtu akiwa amelala akiwa hajitambui.
Alisema baada ya tukio hilo, alirudi ndani haraka na kumwita mpangaji wake ili akashuhudie alichokiona.

Mazagazaga aliyo kutwa nayo
Alisimulia kuwa baada ya mpangaji huyo kuamka, waliamua kwenda polisi lakini wakiwa huko, mkewe aliamua kwenda kumchunguza mtu huyo kwa makini usoni ambapo aligundua kuwa ni shemeji yake, jambo ambalo lilizidi kuwachanganya watu.
Alisema aliporudi alikuta umati mkubwa wa watu umemzunguka Pasco.
Wakazi wa eneo hilo wakishangaa

Kaka mtu alisema kuwa alitimba na askari ambao walimfungua kamba na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza lakini wakiwa njiani, kijana huyo alikuwa akiongea maneno ya ajabu kama vile mtu mwenye majini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina la Mube, Joseph Paja alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema naye alikuwa miongoni mwa mashuhuda.
Alisema kuwa alipofika, alikuta kijana huyo aliyewahi kuishi mtaani hapo kwa kipindi kirefu akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hali ambayo ilimshangaza kila mtu.
Mchungaji wa Kanisa la Church of World, Steven Paul ambaye naye alishuhudia tukio hilo, alisema kuwa baada ya ndugu kuamua kumpeleka polisi aliambatana nao hadi kituoni lakini walipofika, askari walimtema kwa kigezo kuwa hakuwa na kesi ya kufunguliwa, wakashauri apelekwe hospitali.
Ilielezwa kuwa zoezi la kumpeleka hospitali lilifanyika lakini walipofika huko, madaktari walimkataa kwa kigezo kuwa hawakuona ugonjwa wowote, jambo lililosababisha hofu kutanda.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji huyo alisema kutokana na kote huko kushindikana, aliamua kumchukua kijana huyo na kuishi naye nyumbani kwake kwa lengo la kumfanyia maombi.
Baada ya kumchukua, alianza dozi ya maombezi ya nguvu ambapo hivi sasa anaendelea vizuri.
Katika mahojiano na waandishi wetu, Pasco alisema hajui kilichotokea hadi akajikuta amefika Dar, tena getini kwa kaka yake akiwa uchi.
Alisimulia kuwa siku hiyo, alienda benki kutuma ada ya shule na baada ya hapo, alirudi nyumbani kwa bibi yake na kumkuta akiandaa ugali ambapo alikula kidogo kwani alikuwa akihisi maumivu makali ya kichwa.
Baada ya kushindwa kula vizuri, bibi yake alimtaka ale chungwa ambapo alichukua moja na kwenda nalo chumbani, akachukua panga kisha kulikata vipande viwili lakini alipoanza kula, kabla ya kumaliza kipande kimoja alihisi usingizi mzito ambapo alikuja kushtukia akiwa sehemu tofauti yaani getini kwa kaka yake akiwa amezingirwa na watu kibao.
Alieleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na mauzauza ya kichawi ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kaka yake amhamishie Rorya mkoani Mara ambako alienda kuanza kidato cha pili wakati huku Dar alikuwa ameshafika kidato cha nne.

Chanzo: GPL

Mwanaume Akatwa Miguu baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu



Na Mwandishi Wetu, Kilosa
ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said  Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.


Mke wa mtu sumu: Said  Iddi akiwa chini baada ya kukatwa miguu na Ali Omar.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Julai 15, mwaka huu wakati Said na mama Ali walipokuwa ndani ya nyumba ya Ali iliyopo kijijini hapo.
MANENO YA SHUHUDA
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri.
“Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.
Chini ya ulinzi: Mwenye mali, Ali Omar (kati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kumkata Said.
Aliongeza kudai kuwa, Said ni msimamizi wa mashamba ya Ali kijijini hapo na kwamba God ni mtoto wa mwenye nyumba ambayo Ali amepanga kijijini hapo.
MPANGO WA FUMANIZI
Habari zinapasha kuwa mara baada ya mnyetishaji kutoa taarifa za usaliti huo, Ali alimtafuta  ‘baunsa’ ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja na wakaweka mtego kwa kujificha karibu na nyumba hiyo ambayo Said angeingia ili kuivunja amri ya sita ya Mungu.
Umbea kazi: Kijana aitwaye God (kulia) aliyetoa taarifa kwa Ali naye akiwa chini ya ulinzi.
Katika kufanikisha mtego huo, mmbeya huyo alipewa jukumu la kuhakikisha nyendo za Said na mama Ali siku hiyo zinarekodiwa mpaka kuingia ndani ya nyumba hiyo na kumtaarifu Ali ambaye siku hiyo alimuaga mkewe kwamba amesafiri.

SAID ATINGA NYUMBANI KWA ALI
Habari zinasema mtoboa siri huyo alimwambia Said kuwa Ali amesafiri na ndipo jamaa akafunga safari kwenda kwa mama Ali kwa nia ya kujivinjari licha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukifikia katikati.
Mwanamke hutulii?: Mke wa Ali Omar naye akipelekwa polisi baada ya tukio hilo.
Habari zinadai mara baada ya kufika kwa Ali, Said aliingia ndani ya nyumba bila kujua kwamba mwenye mke alikuwa amejificha jirani akisubiri mtego unase.
Inasemekana Said akiwa ndani, Ali na baunsa wake waliibuka kwa kutaarifiwa na God na kumnasa jamaa huyo huku akidai ni mgoni wake. Alimuuliza maswali kadhaa, yakiwemo haya:
“Umekuja kufanya nini ndani ya nyumba yangu? Kwa nini umekaa na mke wangu?”
Habari zinasema Said alijibu hakuona ubaya kwa kuwa yeye ni mwangalizi wa mashamba ya mwanaume huyo hivyo anaweza kuingia ndani kwake wakati wowote.
Said  Iddi akiwa amezungukwa na wananchi baada ya kukatwa miguu.
MWENYE MKE ATIBUKA NA MAJIBU, AMWAGA DAMU
Jibu hilo lilidaiwa kumtibua Ali na ndipo yeye na baunsa wake wapomfunga kamba miguuni Said na kuanza kumkata kwa panga mguu mmoja kisha kuugeukia wa pili.
Said alipiga mayowe yaliyowafanya wanakijiji kukimbilia eneo la tukio kwa lengo la kujua kulikoni ambapo walimkuta Said akiwa anavuja damu na sehemu ya nyuma ya miguu ikiwa nyanga’nyang’a.
Said akipelekwa kwenye difenda.
MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA
Ali, God na baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee kumwagika. Said alikuwa akilia sana.
“Wanakijiji walichukizwa sana na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkong’oto kwa lengo la kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali afikishwe kwenye kituo cha polisi,” alisema shuhuda.
...Akiingizwa ndani ya difenda.
MKE, MUME, MMBEYA WAFIKISHWA POLISI
Polisi wa Kituo cha Dumila waliitwa na kumchukua Said, Ali na God kwa kutumia gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 750 AAJ. Mke wa Ali yeye alipelekwa polisi kwa pikipiki.
Walipofika kituoni, Said alipewa fomu ya matibabu ya polisi (PF 3) na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa matibabu.
“Pale hospitali Said alishonwa miguu yote lakini madaktari wakaamua ahamishiwe katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi,” alisema shuhuda huyo.
Bwana Said akiwa ndani ya difenda.
ANAWEZA ASITEMBEE TENA
Akaongeza: Daktari mmoja alisema haamini kama jamaa (Said) atatembea tena kwa sababu zana iliyotumika kumkata ilifika hadi kwenye mishipa ya nyuma ambayo ndiyo humfanya binadamu aweze kusimama na kutembea.
Said akishonwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
BAUNSA ASAKWA
Afisa mmoja wa polisi kituoni hapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema wanaendelea kumsaka baunsa aliyeshirikiana na Ali kumkata miguu Said.
...Said akizidi kupatiwa huduma.




 SOURCE: GPL

Said, Billionea Aliyemwagiwa Tindikali Usoni, Mfahamu kwa Undani zaidi.



Gladness Mallya na Shakoor Jongo
MSHTUKO mkubwa ulijiri Jumamosi iliyopita, ikiwa ni baada ya kusambaa kwa habari za kumwagiwa tindikali, mfanyabiashara mwenye ‘levo’ ya ubilionea, Said Said Mohammed, 42, ambaye ndiye mmiliki na Mkurugenzi Mkuu wa Home Shopping Centre.
Nje ya jengo la Msasani Mall ambapo Said Said Mohammed alimwagiwa tindikali. Katika jengo hili kuna maduka ya mfanyabiashara huyo.
Said ambaye kwa utambulisho mwingine anajulikana kama Said Mohammed Saad, alimwagiwa tindikali Ijumaa iliyopita, saa 2 usiku, lakini habari zake zikavuma Jumamosi, hivyo kuibua taharuki ya aina yake.
Kuhusu nani alimmwagia tindikali hiyo, sababu ya kutendwa unyama huo, yupi mhusika mkuu wa ukatili wenyewe na malengo ya uharamia, kwa jumla, hayo ni maswali yanayoendelea kuitesa familia yake, watu wa karibu pamoja na Jeshi la Polisi Tanzania.
Taarifa za kipolisi zinathibitisha kwamba alimwagiwa tindikali akiwa anazungumza na mfanyakazi wake wa duka lake lililopo kwenye Jengo la Msasani City Mall kisha akakimbizwa Hospitali ya Ami Wellness Centre, iliyopo Masaki, Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa ndege ya kukodi ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60.

SAID NI NANI?
Ni Mtanzania mwenye asili ya Bara la Asia. Inadaiwa kwamba ndugu zake wengi wana asili ya nchi za Yemen na Saudi Arabia.
Ndiye mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Center. Kampuni hiyo ina maduka mengi Dar es Salaam na katika mikoa kadhaa ambayo yanahusika zaidi na uuzaji wa vitu vya nyumbani na ofisini.
Anatajwa kuwa tajiri mwenye uwezo zaidi katika jumuiya ya wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo, kifedha na ushawishi.
Inadaiwa kwamba wafanyabiashara wengi wenye maduka yao Kariakoo, humtegemea yeye kuingiza mizigo nchini, kutokea nje ya nchi hususan China.
Anamiliki nyumba kadhaa za ghorofa Kariakoo, yapo madai kwamba anamiliki nyumba sita.
Baadhi ya majengo ambayo anahusishwa nayo, la kwanza lina ghorofa saba, lipo Mitaa ya Swahili na Msimbazi, la pili lina ghorofa sita, lipo Kongo na Aggrey, tatu ni la ghorofa nne, lipo Barabara ya Uhuru na kadhalika.
Duka lingine analomiliki mfanyabiashara huyo.
NI MTU WA KUTOA MISAADA
Said kupitia kampuni yake ya Home Shopping Centre, aligeuka nyota ya jaha kwa familia 655, zilizokumbwa na mafuriko eneo la Jangwani, Desemba 2011 kisha kuhamishia Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa moyo wake mwema, Said aliidhinisha kila familia ipewe seti kamili ya vyombo vya nyumbani pamoja na taa zinazowaka kwa kutumia nishati ya mwanga wa jua.
Misaada hiyo, ilikabidhiwa na mkurugenzi mwingine wa Home Shopping Centre, Ghalib Said Mohammed ambaye ni mdogo wa Said. Misaada hiyo, ilipokelewa na Rais Jakaya Kikwete, Januari mwaka jana.

AJENGA SHULE MABWEPANDE
Said hakuishia hapo, baada ya misaada ya vyombo na taa za nishati ya mwanga wa jua, alifanya jambo jema zaidi kwa kujenga shule ya msingi, madarasa yote pamoja na ofisi za walimu, vilivyojengwa kwa ufadhili wa Home Shopping Centre.
Machi mwaka huu, shule hiyo ilizinduliwa na Rais Kikwete ambaye alikiri kwamba ujenzi wake utarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwenye eneo hilo.

ALICHOKISEMA KAMANDA WA POLISI KUHUSU ISHU YA TINDIKALI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, Yusuf Mrefu, alisema kuwa uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio la Said kumwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu.
Mrefu alisema, Said alikuwa akizungumza na mfanyakazi wake nje ya duka lake kwenye Jengo la Msasani Mall kisha akatokea kijana mrefu mwembamba ambaye alimmwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali.
Kamanda huyo wa polisi aliongeza kwamba mfanyakazi huyo wa Said, Hassan Ahmad, naye alijeruhiwa kidogo katika purukushani hiyo lakini alipopelekwa Hospitali ya Ami Wellness Centre, alitibiwa na kuruhusiwa.

KINACHOELEZWA KUHUSU MFANYAKAZI HUYO
Iadaiwa kuwa Hassan, alipata majeraha baada ya kuanguka, wakati akimfukuza jamaa huyo ambaye alimmwagia tindikali Said.

HOSPITALINI AMI WELLNESS
Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Ami Wellness, aliliambia gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini kwamba baada ya Said kufikishwa pale, ilichukua kama nusu saa, akachukuliwa kupelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tayari kwa safari ya kwenda Afrika Kusini.
“Hali yake ilikuwa mbaya, lile jicho moja limeathirika sana, kwa kweli sijui kama litaweza kuona tena. Ila moja litakuwa salama, ukizingatia amepelekwa katika hospitali yenye ubora zaidi. Yule mfanyakazi wake aliumia kidogo tu, alitibiwa na kuruhusiwa siku ileile,” alisema muuguzi huyo.
Kuhusu jina la hospitali aliyopelekwa, alisema: “Hakukuwa na utaratibu wa kuandika rufaa, alichukuliwa tu kupelekwa Afrika Kusini na sasa naamini anaendelea na matibabu vizuri. Ila inasikitisha sana, naamini wahusika walitaka kumfanya awe kipofu.”

NI UMAFIA
Kwa mujibu wa taswira ya tukio lenyewe, kitendo alichofanyiwa ni umafia na mambo kadhaa yanafaa kumulikwa kwa undani. Mambo hayo ni;
Said ana uadui na nani? Aliyemmwagia alijuaje kama yupo pale? Kwa nini tindikali machoni?
Ni wazi Said anao maadui ndiyo maana kitu kile kimetendeka. Bila shaka aliyemmwagia aliambiwa na mtu, huyo anafaa kupatikana. Bila kupindisha ukweli ni kwamba mmwagaji alikusudia kumfanya Said awe kipofu.
Polisi wanatakiwa kuchunguza nyendo za Said, kuona ana uhasama na akina nani katika biashara au hata kwenye mambo ya kijamii. Kadhalika, ichunguze mawasiliano ya watu wa karibu na Said, atajulikana mtoa taarifa, hivyo kumpata mhusika wa ukatili pamoja sababu ya unyama wenyewe.

SKENDO ZA SAID
Said ameshawahi kuripotiwa na vyombo vya habari katika kashfa mbalimbali, gazeti moja liliwahi kuandika matoleo kadhaa, likimtaja kama mfanyabiashara hatari kwa nchi ya Tanzania.
Vilevile, alishawahi kuripotiwa kumfanyia unyama, kijana mmoja raia wa Lebanon ambaye alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yake.

CHANZO: GPL

ASKARI WA KUTULIZA GHASIA (FFU) WAPINDUKA, MMOJA AFARIKI, WAKIENDA KUTEMBEZA KICHAPO MOSHI


ASKARI mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoani Kilimanjaro, Fidelis Mwaliyatabu, amefariki dunia papo hapo na wengine tisa akiwamo Mkuu wa Kikosi hicho kujeruhiwa vibaya baada ya gari lao kupinduka katika kijiji cha Kilingi, wilaya ya Siha, wakati wakienda kuzima vurugu za wananchi.
Ajali hiyo ilitokea wakati kikosi hicho kikielekea katika kijiji cha Karansi kwa ajili ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga wenzao waliokamatwa usiku wa manane baada ya kuvamia mashamba mali ya Shirika la Roho Mtakatifu-Kilasara.
Taarifa kutoka kijijini humo zilieleza kwamba wanakijiji waliamua…
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa kazini. (Picha na Maktaba Yetu)
ASKARI mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoani Kilimanjaro, Fidelis Mwaliyatabu, amefariki dunia papo hapo na wengine tisa akiwamo Mkuu wa Kikosi hicho kujeruhiwa vibaya baada ya gari lao kupinduka katika kijiji cha Kilingi, wilaya ya Siha, wakati wakienda kuzima vurugu za wananchi.
Ajali hiyo ilitokea wakati kikosi hicho kikielekea katika kijiji cha Karansi kwa ajili ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga wenzao waliokamatwa usiku wa manane baada ya kuvamia mashamba mali ya Shirika la Roho Mtakatifu-Kilasara.
Taarifa kutoka kijijini humo zilieleza kwamba wanakijiji waliamua kuandamana baada ya wenzao watano kukamatwa na Jeshi la Polisi nyakati za usiku kwa mahojiano kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kushawishi wanakijiji wenzao kuvamia maeneo ya Shule ya Kilasara na kusababisha hasara kubwa kwa shule hiyo.
Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao, wanakijiji waliamua kuaandamana hadi katika kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao hali ilisababisha jeshi hilo kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya, jambo ambalo lilishindikana kutokana na wingi wa watu walikuwa wanaandamana.
Inadaiwa kuwa wananchi hao walijikusanya na walianza kuandamana kuanzia majira ya saa 7 usiku kuelekea kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao walikuwa wanashikiliwa.
Wananchi wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni John Sokoine, Abeli Solomoni, Christopher Solomon na aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Julius. Wote walikamatwa usiku wa kuamkia jana.
Mnamo Juni 11, mwaka huu majira ya mchana wananchi wa kijiji hicho walivamia eneo lenye ukubwa wa hekta mbili na kufyeka mazao mbalimbali yaliyokuwa shambani hapo kwa madai kuwa wamiliki wa shule hiyo wamechukua eneo hilo kinyume cha taratibu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu, Kanda ya Afrika, Padri Jerome Okama, aliushutumu uongozi wa kijiji hicho kwa kuvifumbia macho vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi wakati wakitambua kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 8.9 linamilikiwa na shirika hilo kihalali.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka wilayani humo jana jioni, alisema askari hao walipata ajali hiyo majira ya saa 6.45 mchana katika kijiji cha Kilingi nje kidogo ya mji wa Sanya Juu.
Alisema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na wengine wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu ya Kibong'oto ilioyopo wilayani Siha na kwamba watano kati yao hali zao ni mbaya.
Alitaja gari la Polisi lililopinduka na kuua kuwa ni Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2070 lililokuwa likiendeshwa na Sajenti Herman Dancan. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kuacha njia na kupinduka.
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Mkuu wa FFU mkoani hapa, ASP Nonino, Renatus Misigalo, Alfonce Joseph, Koplo Elifuraha Lenare, Peter Albert, Bashiri Yusuph, George Mwakyusa na Gaspar Mwapunda.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kibong'oto.
CHANZO: NIPASHE & GPL

Wema Sepetu Hatiani, Heunda akaenda Jela Safari Hii.






Na Waandishi Wetu

KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.

Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.…
Na Waandishi Wetu
KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.
Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.
Kabla ya  kupandishwa  kwa ‘pilato’,  staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.

ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.
MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.
WEMA AGEUKA MBOGO, ALALA SELO
Baada askari kumfikia staa huyo, walimtaka kwenda naye kituo cha polisi kwa kutumia difenda walilofika nalo ambapo Wema alipinga na kugeuka mbogo kwa kudai kwamba hawezi kupanda difenda kutokana na hadhi yake.



Pamoja na askari kutaka kumpandisha kwa nguvu, staa huyo alipinga na ikakubaliwa apande gari lake aina ya Audi Q7 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari.
Safari ikaishia Kituo cha Polisi cha Kawe ambako staa huyo aliandikisha maelezo na baada ya zoezi hilo akatupwa selo.

WEMA HAUOZI
Kama lilivyo jina lake, wema hauozi, staa huyo alipata dhamana saa 5 za usiku baada ya kudhaminiwa na msanii  mwenzake wa filamu, Kajala Masanja.
Kajala aliwahi kutolewa katika mdomo wa jela na Wema siku za nyuma baada ya kukutwa na hatia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar alipotakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 13 au kwenda jela, Wema alimlipia kiasi hicho cha fedha.
WAPAMBE FULL SHANGWE
Wapambe wa Wema waliokuwa wamejazana nje ya kituo hicho cha polisi, walilipuka kwa shangwe baada ya bosi wao kuchomolewa kutoka selo. Staa huyo aliondoka na gari lake lililokuwa likiendeshwa na meneja wa kampuni yake aitwaye Petit Man.

ATEMBEZWA KWA MIGUU
Julai 17, asubuhi Wema alirudi kituoni hapo na kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kusomewa mashitaka yake.
Katika hatua ya kushangaza, staa huyo alitembezwa kwa miguu umbali wa mita 200 kutoka kituo cha polisi hadi Mahakama ya Mwanzo ya Kawe.
APANDISHWA KIZIMBANI
Wema alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mh. Hakimu, Bernice Ikanda na kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Kayumbu.
Mbele ya hakimu, Wema alikana mashitaka na hakimu aliiahirisha kesi hiyo mpaka Julai 31, mwaka huu.

IKO SIKU WEMA ATAFUNGWA GEREZANI
Kumbukumbu kutoka kwenye makabrasha yetu zinaonesha kuwa, mrembo huyo ni mtu wa majanga, mara kwa mara amekuwa akifikishwa polisi na mahakamani kutokana na ugomvi.
ALIVUNJA KIOO CHA GARI LA KANUMBA
Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja. Hata hivyo, Kanumba aliifuta kesi hiyo.

ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alikamatwa na Polisi wa Oysterbay jijini Dar na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob Junior’.
Katika kesi hiyo, Hakimu Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi 40,000 ambapo alilipa fedha hizo.
ALIMTUSI REHEMA FABIAN
Aidha, mara baada ya Wema kuachiwa huru mahakamani hapo alikamatwa tena na polisi kwa kile kilichodaiwa kumtusi Miss Kiswahili 2008, Rehema Fabian. Wema alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa maelezo zaidi.

ALIMTUKANA MSANII
Aidha, Wema amewahi kulala kituo cha Polisi Oysterbay, Dar akiwa na mashoga zake, Kajala na Dida kwa madai ya kumshambulia mwigizaji mmoja wa Bongo, kwenye pati iliyofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar. Kesi hiyo iliisha kwa mazungumzo nje ya polisi. 

Imeandikwa na Musa Mateja, Mwaija Salum, Makongoro Oging’ na Shakoor Jongo.
SOURCE: GPL.

Unamkumbuka Rehema?!!, Sasa anakula bata na Mtoto wa Balozi Huko China!!


Na Hamida Hassan
MLIMBWENDE aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa Nigeria nchini China aliyemtaja kwa jina moja la Allen anayetaka kufunga naye ndoa.
Rehema akijiachia na mtoto wa Balozi wa Nigeria nchini China aitwaye Allen.
Akichati na Risasi Mchanganyiko, kwa njia ya mtandao, Rehema alikiri kuwa na mwanaume huyo ambaye ni mtu mzima na kweli ni mtoto wa balozi huyo.
Rehema akiwa na Allen.
“Nimechoshwa na masharobaro hivyo nimeamua kutulia na mwanaume huyo kwa sababu nimempenda na yeye anaonekana kunipenda,” aliandika Rehema.
...Wakizidi kujinafasi.
Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.
...Pozi la kamera.
“Tumepanga kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya ndoa, hivyo nitarajieni huko muda si mrefu,” aliandika Rehema na kuongeza kwamba atafanya bonge la sherehe.

Source: GPL
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga