Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

JOYCE KIRIA AKWAA DENI LA MIL 500 BAADA YA KUTOA SIRI YA MBUNGE WA ZANZIBAR


Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.

Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi

MAKAH@BA MWANZA WAVAMIWA NA OFM WAKIWA WANAJIUZA


Issa mnally/Mchanganyiko
Baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna maeneo jijini Mwanza yanatisha kwa biashara ya ngono, Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivi karibuni imetua na kufanikiwa kufumua dangaro maarufu.

Makahaba hao wakiwa katika mawindo yao ya kila siku. Awali, dawati la OFM lilipokea sms kutoka kwa msomaji wake aliyeomba hifadhi ya jina lake iliyosomeka hivi: “Jamani nyie tunawaaminia kwa kufichua maovu, tumeona kazi nyingi nzuri mlizofanya Dar sasa tunaomba mje huku Mwanza maana kuna maeneo kama vile Liberty, Market Street, Deluxe na Villa Park, Kirumba yanatisha kwa uchangudoa.” 
Baada ya kupokea meseji hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita kamanda wa OFM akiwa na wenzake walitingia jijini humo na katika zungukazunguka yao, walifanikiwa kunasa eneo maalum linalosifika kwa biashara hiyo haramu.
Ilikuwaje?
...Wakisubilia wateja.Mishale ya saa 8 usiku mapaparazi wetu walitonywa juu wa kuwepo mabinti waliojikusanya katika maeneo ya Liberty (Mwanza mjini) huku wakitumia nyumba moja iliyopo karibu na hapo kufanyia ufuska wao. 
Bila kuchelewa, timu ya OFM ilifika na kuwakuta mabinti hao wakiwemo wake za watu wakiwa wamevaa kihasara ikionekana wazi walikuwa ‘sokoni’.
Kufuatia hali hiyo, maparazi wetu walianza kuwafotoa picha kitendo kilichowafanya watimue mbio kuelekea kusikojulikana.
Kamanda wa OFM akitua jijini Mwanza. Hata hivyo, baada ya timuatimua hiyo, inadaiwa wengi waligundua kuwa OFM wako Mwanza na wengi waliokuwa wakifanya ufuska eneo hilo walihama wakihofia kunaswa. 
Uchunguzi uliofanwa na gazeti hili umebaini kuwa, kama ilivyo maeneo mengine, Mwanza pia wapo wake za watu na wanafunzi ambao nyakati za usiku huingia viwanja na kujiuza ili kupata pesa za kujikimu.OFM inaahidi kuendelea kufichua maovu mkoani humu ili kuhakikisha maadili yanachukua mkondo wake.


HEBU MUONE LADY JAY DEE ENZI ZA KU RAP


Kweli maisha ni safari ndefu, mkali Jide wa enzi hizoo, kipindi anachana, alikuwa bonge la msela. cheki picha kali nyingine hapo chini.

SHILOLE AWAWAKIA WALIOMPONDA KWA KUWA KICHWA WAZI MSIBANI KWA MEZ B



Nawaangalia tu wote mnaonisnich kama ww unajiua ni snich jitoe tu coz hata mm sina time na ww! Tusilazimishane kuwa kama ww mm ni mm na ww ni ww so naona au coz mm ni shilole nisingeenda msiban pia mngechamba oooh wasanii hamjaliani sasa mm nimekwenda lakin bado oooh nywele
 sijafunika! Plzzz tusiingiliane mbona hamna jema nyinyi loh! Mnikome nafanya kile ambacho naweza kufanya kwa wakati huo so tuheshimiane (tusi) tena nyie ambao mnasema ooooooo hujafunga kitamba kichwani hata misiban hamjaww kwenda 

HATIMAYE MILLARD AYO AMILIKI STUDIO YAKE YA RADIO


Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini
hii na baadae watu wangu francis_ayo na abdul8819 wa pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa. 

HAYA SASA, HIZO NDO SIFA ZA MWANAUME ANAEMTAKA JAY DEE


SIFA ZA MWANAUME AMTAKAE LADY JAYDEE KWA SASA Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa? JIBU :Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona ),Asiwe
tegemezi.Hata kama sio tajiri lakini asinitegemee.Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar,Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale.Nikikohoa tu awepo hapo Kwa mtazamo wako unaweza kupata Mwamke au Mwanaume asiye na mapungufu?

BARUA YA JACK AKIWA GEREZANI, ALIA NA USALITI WA P3NZI LAKE KWA JUX, DIAMOND NA ZARI NA SKENDO ZA MASTAA WA BONGO



Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.

Modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’.
BARUA KUTOKA CHINA
Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani map3nzi hayachagui hasa kama ana furaha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike map3nzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika Jack.
DIAMOND, ZARI
Mbali na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo alionesha kushtushwa na p3nzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh! Wala hawatadumu maana map3nzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond Platnumz) atahamia South.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakiwa kwenye pozi.
KAJALA Vs WEMA
Pia video queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan (ya Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la Wema na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies walishazoeleka kugombana na kupatana.
Bifu hilo ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK) huku akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa wako hivyo kila muda, kawaida yao.”
JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malov3e na s3xy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.
Juma Khalid ‘Jux’, akiwa na mp3nzi wake Vanessa Mdee.
“Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack.
Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapema hivyo hatakaa jela miaka yote sita.

BAADA KUKOSA MUME, MISS DODOMA AAMUA KUOKOKA


Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans amemrudia Mungu kwa maana ya kuokoka kwa kile alichodai kutotimia kwa malengo aliyojiwekea.Akizungumza na mwanahabari wetu, Eva alisema tangu akiwa mdogo, alijiwekea kiapo kuwa endapo atashindwa kumpata mume mwema, basi atafanya kazi ya kumtumikia Mungu.
Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans akiwa kanisani.
“Nakumbuka mapito yangu yote tangu nikiwa mdogo mpaka nikaingia kwenye masuala ya urembo nilijiwekea nadhiri ikifika muda mambo yangu hayajakamilika, itanibidi nimrudie Mungu wangu.
“Baada ya kupitia urembo nilichumbiwa, hapohapo nikaanza kuhudhuria mikutano mbalimbali ya neno la Mungu, siku moja Nabii akitoa neno, nilimsikia akisema kuna binti mmoja hapa anataka kuolewa apite mbele haraka sana, basi nikapita mbele na nilipofika pale alianza kuniombea na baadaye alianza kuniuliza maswali.
“Akaniambia mwanaume anayetaka kunioa hana sifa za kuwa mume bora na kama nabisha nimchunguze, basi nikamchunguza na kugundua kuwa hakuwa na sifa.“Basi nilivyojua tu nikaamua nisitishe mipango ya ndoa zikiwa zimesalia wiki mbili tu ili ndoa ifungwe, nashukuru Mungu nilieleweka, na kuanzia hapo nikaamua kuokoka kabisa, ninaomba sana Mwenyezi Mungu aniletee mume mwema,” alisema mrembo huyo.
Eva alifunguka kuwa katika mashindano ya urembo kuna uchafu mwingi hivyo akawashauri wasichana walioko huko kumrudia Mungu.

WAREMBO WALIOZAA NA NAY WAMALIZA TOFAUTI ZAO, WAONEKANA KAMA WAKE WENZA ESCAPE ONE.


Mabinti wawili waliozaa na msanii wa muziki, Emmanuel Elbarik ‘Nay wa Mitego’, Siwema na Skyna Ally ambao awali ilidaiwa walikuwa na bifu zito, sasa wameamua kuwa mashosti.Ijumaa hivi karibuni liliwanasa wawili hao kwenye Ukumbi wa Escape One, Msasani jijini Dar wakiwa beneti kama mtu na mke mwenza na lilipotaka kuzungumza nao wote walichenga na kutaka waachwe.
Mrembo aliyezaa na msanii wa muziki, Emmanuel Elbarik ‘Nay wa Mitego’ Siwema.
Hata hivyo, mmoja wa marafiki aliyekuwa ameongozana nao aliyeomba hifadhi ya jina lake alimwambia mwandishi wetu kuwa, baada ya wawili hao kuwa na bifu kwa muda mrefu, waliamua kukaa chini na kumaliza tofauti zao kwani kilichotokea tayari kimeshatokea.
Skyna Ally.
“Sasa hivi ni mashosti ile mbaya, sehemu mbalimbali wamekuwa wakienda pamoja, yaani ni kama vile wamekubali kuwa wake wenza licha ya kwamba anayekaa na Nay ni Siwema,” kilieleza chanzo hicho.

BANDAWE BADO ANAMKUBALI ROSE NDAUKA, JAPO WAMESHA ACHANA.


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ambaye sasa anatamba na wimbo wake wa Tucheze amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa tangu atengane na mzazi mwenziye, Rose Ndauka bado hajatokea wa kumtetemesha.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe.
Akizungumza na Ijumaa juzikati, Malick alisema kuwa huko nyuma alipomuona Rose alimtetemesha na kuamua kuingia mzimamzima mpaka kufikia hatua ya kupata naye mtoto lakini mpaka sasa hajatokea kama yeye.

Rose Ndauka.
“Unajua mambo yanapotokea lazima kukubaliana nayo na huwezi kulazimisha. Tangu uhusiano wetu usambaratike, hajatokea kama Rose,” alisema Malick.

DANCER WA DIAMOND AKUBALI KIAINA KUHUSIKA NA UJAUZITO WA AUNTY EZEKIEL


Kuanzia magazeti, mitandaoni mpaka kwenye redio… kwenye mtiririko wa stori za mastaa wa Tanzania zilizoongelewa au kuandikwa sana ndani ya wiki 6 zilizopita, hii ya mwigizaji Aunty Ezekiel kuwa na ujauzito na dancer wa Diamond Platnumz aitwae Mose Iyobo imo kwenye orodha. 
Wawili hawa walitajwa kuwa mapenzini kitambo na hata ujauzito wa Aunty iliandikwa kwamba baba kijacho ni Mose japo Aunty mwenyewe alikanusha.
Nakumbuka alisema ‘kuhusu taarifa za mimi kupewa ujauzito na Mose Iyobo, hizo taarifa mwenyewe nasoma kwenye magazeti nasikia kwenye Radio kama unavyosema lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani‘ 

Pamoja na kukanusha huko, wawili hawa wameendelea kuchukua nafasi kwenye vichwa vya habari kutokana na post zao wenyewe kwenye page za instagram wanazomiliki ambapo wiki mbili zilizopita Mose aliweka hii picha hapa chini huku Aunty akiwa juu yake kitandani na kuandika ‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila……..?

VIDEO YA WASANII TUNDA NA STANI WAKIFANYA MAP3NZI YAVUJA....


Aibu! Mrembo anayeuza nyago (video queen) kwenye video kibao za wasanii wa Bongo Fleva, Tunda Sabasitana na mchekeshaji maarufu Bongo, Stan Bakora wamepiga picha za ng0n0 kisha kusambaa hadi kulifikia deski la Ijumaa Wikienda. 

Mrembo anayeuza nyago (video queen) kwenye video kibao za wasanii wa Bongo Fleva, Tunda Sabasitana na mchekeshaji maarufu Bongo, Stan Bakora wakijiachia.
Picha hizo chafu zilitua mezani kwetu wikiendi iliyopita ikiwa ni siku mahususi kwa wapendanao.
Picha hizo zinawaonesha wawili hao wakiwa kwenye ‘bedi’ huku wakifanya yao.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Stan na Tunda, wawili hao wemekuwa kwenye ‘malovee’ siku nyingi na kupiga picha za ngono kwao si ishu maana wote hawana mshipa wa aibu kwa kuwa ni wasanii.

Ilisemekana kwamba tangu Stan aanze kuigiza amekuwa akifanya mambo ya aibu tofauti na jinsi anavyoonekana.
 
Source: GPL

KAJALA ANASWA NA KIDUME CHINA. KUMBE HAJAFULIA KIHIVYO EEH.


Yap! Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘K’ anadaiwa kufumwa na mwanaume nchini China huku akisusiwa sherehe ya bethidei yake, Ijumaa Wikienda limeinyaka.

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘K’.Kwa mujibu wa kachero wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) aliyepiga kambi Hong Kong, China, mwishoni mwa wiki iliyopita Kajala alionekana na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Meddy kwenye pati hiyo ambayo eti inasemekana ilihudhuriwa na watu watatu.
Ilisemekana kwamba Kajala amejibu mapigo kwa kujinyakulia kijana kwa ajili ya kumkosha moyo na kumsafisha na skendo za waume za watu.Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Kajala kwa njia ya simu hakuwa hewani na hata alipotumiwa ujumbe kwa WhatsApp hakujihu.hakujib

SHILOLE AAMBULIA KICHAMBO KIKALI BAADA YA KUANIKA MAPAJA YAKE HIVI


 Shilole Alipost Picha hiyo hapo juuu na Kuandika Maneno haya "Baada ya Kutoka TBC tv Taifa! Now nipo Mlimani Tv Live "
Jisomee Watu walivyomchamba hapa chini:

MAMA KANUMBA ANA LAANA, NDO MAANA ANAFILISIKA


   Stori: Laurent Samatta
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amemchana mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kuwa anateswa na laana na ndiyo maana hafanikiwi.

Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba. Mzee huyo alisema mama Kanumba ameshindwa kufanikiwa katika mambo mengi likiwemo suala la kuendeleza ofisi ya marehemu kutokana na kushindwa kumshirikisha yeye kama baba na ndiyo maana amepata laana.“Tatizo ni papara ya mwezangu ya kutaka mali ndiyo mambo yanayotokea na kamwe hataweza kufanikiwa kwa sababu baraka za mtoto zinatoka kwa mama na baba na hiyo laana itazidi kummaliza sababu hakunishirikisha,” alisema. 
Mama Kanumba Flora Mtegoa. Alipotafutwa mama Kanumba kuhusiana tuhuma hizo, alisema:
“Huyo mzee yeye ndiyo ana laana, nimeshamzoea, hana jipya amekalia majungu. Mimi sina laana, nakaa kwenye nyumba ya maana na si kama yeye anaeishi kwenye nyumba ya udongo.

YULE JAMAA ANAYEWATAKA WASICHANA KINGUVU MTANDAONI HUYU HAPA, APATA KICHAMBO CHA MWAKA


"Huyu kiumbe nimemchoka ndio wale niliokua nawalalamikia kila siku... Nishaongea kiistarabu nimechoka, matus! yote nimetukana yupo tu nikibloc k linafungua account mpya
... Jaman hiv kuna viumbe wamezaliwa kuwakera wenzao nakuwaharibia siku... Nakuchukia wewe furushi nakuchukia kama ninavomchukia shetan.. Nataman ningekukamata hakyamungu naapa hats panga ningekukata.. Khaaaaaaa hiv ungebahatika kua angalau hata hawara yangu ww mbwa cungepanda ungo untafute nilipo uniroge.. Nahasira jaman I hate this nguruwe..lugha ya mwisho ww nguruwe hii ni last worning kitachofuata ushawah ona wajinga wenzio wanavoeditiwa.. Okey go ahead"
MSUMBUFU
 

SKENDO NZIMA YA STARA THOMAS KUFUMANIWA NA MUMEWE HII HAPA



Staa wa Bongo Fleva, Stara Thomas akiwa na mumewe.
Stori: Deogratius Mongela na Chande  
HAYA ni madai mazito! Kwamba, staa wa Bongo Fleva ambaye juzi kati alinusa kwenye gospo ‘ikamshinda', Stara Thomas anadaiwa kufumaniwa na mumewe, Raumu Ally mpaka kufikishana polisi, Risasi Jumamosi halipitwagi na ‘ubuyu’. 
Kwa mujibu wa shuhuda wa kuaminika, tukio hili lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa familia hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam.

FUMANIZI LILIVYOTOKEA
Akilisimulia Risasi Jumamosi baada ya kuulizwa kama kweli fumanizi lilikuwepo, mume wa Stara alifunguka hivi: “Ni kweli ilitokea. Siku ya fumanizi nilikuwa nimesafiri, lakini nikarudi ghafla bila kumpa taarifa mke wangu.
“Nilikuwa nyumbani, yeye hakuwepo. Saa 9:00 usiku ndiyo nilimwona Stara akirejea tena akiwa amelewa. Aliletwa na gari mpaka nje ya nyumba.” 
NDANI YA GARI KWA NUSU SAA
“Lile gari lilisimama zaidi ya nusu nje bila kushuka mtu ndipo nikaamua kulifuata. Stara aliponiona akamwambia dereva ambaye najua ni jamaa yake, aondoe gari kwani mimi ni mume wake nitampiga.
“Nilizuia wasitoke, yule jamaa akarudi nyuma na kuniparuza kwenye mguu na tairi, nikadondoka. Niliposimama nikaokota jiwe na kulirushia gari nikavunja kioo cha mbele.” 
STARA, JAMAA POLISI
Mume huyo anaendelea kusimulia: “Baada ya hapo Stara aliondoka na yule jamaa mpaka Kituo cha Polisi Tabata ambapo walinishtaki. Niliitwa polisi kwa madai ya uharibifu wa kioo.
“Kwa vile nilikuwa nasafiri kwenda nje ya nchi (ni dereva wa malori) niliona mambo yaishie pale kituoni, nilikwenda nikachukuliwa maelezo kisha nikalipa shilingi laki saba (700,000).”
Mume wa Stara Thomas Raumu Ally. DALILI ZA KUVUNJIKA KWA HESHIMA
Habari zaidi zilidai kwamba, wawili hao wamekuwa kwenye ugomvi wa mara kwa mara.
Imeelezwa kwamba, ugomvi wao ulianza pale Raumu aliposhindwa kulipa ada ya shilingi laki tano ya mtoto wa Stara (jina tunalo) huku madai ya mchepuko nayo yakisambaa hali iliyokuwa ikishusha heshima ya familia. 
TUJIUNGE NA RAUMU 
Akifafanua kuwepo kwa sakata hilo pamoja na chanzo kizima, Raumu alisema kuwa Stara amekuwa akimfanyia vituko na mambo ya ajabu tangu aliposimamishwa kazi kwenye kampuni aliyokuwa akifanyia awali (jina kapuni) baada ya kutokea matatizo. “Mimi ni dereva wa malori, nakwenda Lusaka (Zambia) na Congo (DR), nimekuwa na mgogoro na Stara baada ya kusimamishwa kazi. Unajua ukiwa huna kazi hata fedha huna. Alitaka nimlipie ada ya laki tano mtoto wake lakini nikawa sina, ikawa maneno.” 
KUMBE KUNA MENGINE ZAIDI
“Huwezi kuamini ndugu zangu wamenitenga mimi kwa sababu wakati naanza kuishi na Stara nilibadili dini yangu ya Kiislam na kumfuata yeye kwenye ulokole (wakati huo) halafu leo hii ananiletea mambo ya ajabu! Stara amuogope Mungu.” 
WALIKUTANA HIVI 
Akizungumzia historia fupi ya uhusiano wao, Raumu alisema walikutana kwa mara ya kwanza, Stara alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Mzizima, Dar, miaka ya 90.
Stara Thomas. MAP3NZI MOTOMOTO
Map3nzi yao yalikuwa motomoto lakini baadaye walipotezana kisha kuja kuonana tena miaka ya hivi karibuni huku kila mmoja akiwa na maisha yake.
Kutokana na namna walivyopendana kupita kiasi kipindi cha awali, wawili hao walirejesha uhusiano ambapo mwanaume huyo alihamia nyumbani kwa Stara, Tabata baada ya staa huyo kuachana na mumewe wa ndoa aliyezaa naye watoto wawili. 
STARA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Stara ili kujibu tuhuma hizo ambapo alipopatikana mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Haloo Stara…
Stara: Haloo.
Mwandishi: Unamfahamu Raumu?
Stara: Kwanza wewe nani? 
Mwandishi: Mimi ni mwandishi wa Global Publishers.
Stara: Ndiyo namjua Raumu. 
Mwandishi: Ni nani kwako? 
Stara: Ukitaka kujua kuhusu Raumu, njoo nyumbani tuongee.
Mwandishi: Nataka unijibu kuhusiana na tuhuma za yeye kukufumania.
Stara: Njoo nyumbani wewe na Raumu tuongee tuyamalize huku.
Hata hivyo, mwandishi wetu alitinga nyumbani kwa staa huyo lakini hakumpata hadi gazeti hili linakwenda mitamboni.

RAY C AJITAMBA NA NYOTA YAKE.


kupitia account yake ya insta...Ray C azid kuwaacha midomo wazi mashabik zake.. hiki ndicho ameandika... nanukuu... Haka kademu kaliumiza wengi na hako kakiuno dah kalikuwa homa ya jiji na ndio maana kakarushiwa pepo la madawa maana kalikuwa kanasumbua sana kimuziki na kimvuto!ndio maana hakuna hata msanii mwinzie aliempa hata pole mwee!tatizo kanyota kake ndo kalimletea majanga maana kanyota kake kalin"gara sana ndio maana kakapewa mtihani mgumu ili
kaadhirike na pengine kapotee kabisa lakini kana bahati mungu nae alikapenda sana na ndio sababu kamepewa nafasi nyingine ya kuishi na kutimiza mallengo yake!tatizo wabaya wake wana hasira ile mbaya kwanini kamerudi tena?kwanini kabishi kufa kama paka?

kwanini kamerudi tena kwenye muzikj?kwanini hakajafa!!!kwanini ziko nyiiiiiiiingi?????kwanini kaliokolewa na mkubwa wa nchi????kwanini Rais alikasaidia????mxuiiiiiiiiiii KWANINI NYIIIIIIINGI?MWEEEEE BAHATI YA MWEZIO USIILALIE MLANGO WAZI!NDO HIVYO TENA NDO ISHAKUWA!!!!WE KAA UJIULIZE KWANINI KWANINI!!!!WAKATI UNALISUBIRI JIBU MWENZIO NIKO MBALI TAYARI!ZE PROBLEM IS ZE NYOTA!!!!!Ndo jibu labda!Kwanini my foot! je, wewe unalo lakusema? karibu 

KAJALA APAKWA VIBAYA INSTA, KAFULIA MBAYA, SOMA HAPA YALIYOMWAGWA KUHUSU YEYE.


Kajala Kwenye News Tena Katika Pita pita zangu Instagram nimekutana na huu Ubuyu kutoka kwa Dougiesmasta akimponda Kajala na Kuandika haya Hapa Chini:
"Hehehehehehehe kama nilivyo sema mbea kazia yake ni kufikisha habari....na habari ndio hiii watu mpoooooooooo kutukanwa sitaki lkn umbe wa mujini ndio huu eeti ndugu yetu billionea kajala wa masanja sasa hiv amekuwa apeche alolo aka alosto kafulia fuli fuli...hatari hapana chezea lakzima utajiuliza kwan bwana Ck yuko WAP...aibu mjin CK ajifungia ndani anamadeni kila kona ya dunia....ck wa kuuza vitu vyake vya ndani inatia huruma billionea kajala wa kutembelea NOAH wakat mbezi ya kimala NOAH dala dala uwiiii....
 
kajala tulikwambia lkn hapa mjini ukifulia hakuna atakae kutaka yuko wapi yule big daddy alokuwa anajifanya anakupenda kumshinda mamako mzazi wote wamekukimbia kajala wewe sio wakujifungia ndani bilionea shauzi kumwaga pesa sasa hiv unazijutia..yani wenzio wananunua magali wewe unauza hatari hii...hiv KAY YAKEE wewe kwann kila mwanaumr utakae kuwa nae lazima aishie jela maskin CK yani kama namuona anavyoenda kunyea debe mpooo CK kazi ndo basi wazee TAKUKURU wamfikisha mahakamani kwa wizi wa pesa za serikali...
 
mungu sio fundi juma tusema ukiwa huna pesa utampa ny... mungu wako wewe ndio wawote kajala ulifurahi Sana Wema alipo pokonywa gali kipo WAP huyo bwana alokuwa anakutia jeuri sasa hiv kabaki yeye na tumbo lake...KAY VIP China mbona hatuoni tena safari zimeingia mchanga au hahahahahaha jamn jmn msipende kuchezea pesa zikiisha utaanza kukumbuka unao wadai wote
NAENDELEA UMBUYU MREFU" By Dougiesmasta

PAMOJA NA KUCHANGIWA KUJENGEWA NYUMBA NA BWANA'KE, MAMA AMKANA MCHUMBA WA LULU.


Kufuatia kauli yake ya hivi karibuni kuwa nyumba anayomiliki ilitokana na mchango wa bwana’ke (hakumtaja jina), mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ameibuka na kumkataa mwanaume huyo.


Mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.
Kwa mujibu wa Lulu, nyumba hiyo iliyopo Kimara jijini Dar ameijenga kwa kusaidiana na bwana’ke kwa mtindo wa pasu kwa pasu (kuchangia nusu kwa nusu).Alisema kuwa anamshukuru Mungu kwani hadi hapo ilipofikia ikiwa inakaribia kumalizika ameijenga kwa nguvu zake na mwanaume wake huyo.

“Yeah! Nimejenga kwa msaada wa mwanaume wangu, tunasaidiana nusu kwa nusu,” alinukuliwa Lulu.
Pamoja na mbwembwe zote hizo za staa huyo kwa jamaa yake huyo, mama mzazi wa Lulu ameliambia Amani kwamba hamtambui mwanaume huyo kwani hajawahi kwenda kujitambulisha kwake pamoja na kwamba kahusika kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.
Alifunguka: “Sijawahi kutambulishwa na Lulu kama ana mchumba.
“Kwa hiyo awe amemsaidia au hajamsaidia, mimi simtambui.
“Ingekuwa Lulu amewahi kumtambulisha kwangu kuwa huyo ndiye mchumba wake hapo sawa lakini hakuna kitu kama hicho.

“Halafu naomba utambue kwamba Lulu hawezi kumtambulisha bwana’ke au boy friend wake kwangu, siyo heshima labda awe mchumba. Hapo kidogo afadhali lakini mtu tu mtu, hakuna kitu kama hicho.
Kabla ya Lulu kueleza ukweli juu ya ujenzi wa nyumba hiyo, awali kulikuwa na madai kwamba alihongwa na mheshimiwa mmoja (jina tunalo) huku wote wakikanusha kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo, kitendo cha Lulu kumiliki mjengo huo kimempa heshima kubwa tofauti na mastaa wenzake wa kike ambao wamekuwa wakiishia kupangiwa nyumba na kuhongwa magari yasiyo na kadi kisha kunyang’anywa na kurudia maisha ya kawaida uswahilini.




Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga