Kuanzia  magazeti, mitandaoni mpaka kwenye redio… kwenye mtiririko wa stori za  mastaa wa Tanzania zilizoongelewa au kuandikwa sana ndani ya wiki 6  zilizopita, hii ya mwigizaji Aunty Ezekiel kuwa na ujauzito na dancer wa  Diamond Platnumz aitwae Mose Iyobo imo kwenye orodha. 
Wawili  hawa walitajwa kuwa mapenzini kitambo na hata ujauzito wa Aunty  iliandikwa kwamba baba kijacho ni Mose japo Aunty mwenyewe alikanusha.
Nakumbuka  alisema ‘kuhusu taarifa za mimi kupewa ujauzito na Mose Iyobo, hizo  taarifa mwenyewe nasoma kwenye magazeti nasikia kwenye Radio kama  unavyosema lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani‘ 
Pamoja na  kukanusha huko, wawili hawa wameendelea kuchukua nafasi kwenye vichwa  vya habari kutokana na post zao wenyewe kwenye page za instagram  wanazomiliki ambapo wiki mbili zilizopita Mose aliweka hii picha hapa  chini huku Aunty akiwa juu yake kitandani na kuandika ‘Nzi kufa kwenye  kidonda sio ufala ila……..?
