Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

NI ZAMU YA OMMY DIMPOZ KUFAIDI KWA AVRIL


As haters hate, it is undeniable that Avril and Ommy Dimpoz have some serious chemistry as far as music is concerned,  a fact that has escalated them to position one this week's mdundo charts. Here is how your favorite jams have fared the past week.

PICHA 3 KALI TOKA KWA JACQUELINE WOLPER


Msanii wa Bongo Movie Jacqueline Wolper ame share na fans wake Picha 3 kali za kinyumbani nyumbani. cheki nyingine hapo chini.





PICHA YA LEO: AGNESS MASOGANGE NA BALAA LAKE KWA WATAZAMAJI


Kama ilivyoo Kawaida yake, Mwana dada Agness Masogange ametupia picha hizo za kimitego katika page yake ya Instagram, Jionee Mwenyewe.




RAY C AMEZIDI KUKAA MAPAJA WAZI




Imekuwa ni kawaida now days wadada hasa maarufu kujipiga picha za mikao ya ki hasara hasara, sasa hebu jione mwenye picha 3 tofauti zikimwonesh Msanii Ray C akiwa Mapaja Wazi, ndo Style au? Angalia Picha nyingin hao chini:-





RAY C FOUNDATION YAULA, WAFADHILI WAKUBWA WAWILI WAJITOKEZA


 
Ray c akifunguka: Coz Am Happy!Nimepata habari nzuri sana nadhani muda si mrefu mambo yatakuwa mazuri tena ssanakwikwikwik Haleluya!Ray C Foundation imepata wafadhili wawili wakubwa sana kwani wamefurahishwa na shughuli tunazofanya za kuhamasisha na kuelimisha vijana kuhusu athari za utumiaji madawa ya kulevya!tuna project kubwa sana inaandaliwa ili tuweze 
kuwasaidia vijana wa mikoa yote ya Tanzania hasa mikoa iliyoathirika zaid kam Arusha!Tanga na kisiwa cha Zanzibar pamoja na MorogorO.Mungu ni mwema sana kwangu!Amen Amen tunaandaa insta page ya Ray C Foundation ili muone shughuli na projects mbalimbali za Foundation yetu!Tuna mpango wa kuanzisha kipindi cha Tv kitakachoonyesha jinsi gani madawa yalivyoathiri nchi yetu!vijana wetu familia nk........More to Come!Nimeamua kuweka akili yangu yote kwenye Foundation yangu. 

WEMA BADO ANAMPENDA DIAMOND PLATNUMZ, AWEKA VIDEO YA JAMAA AKIWA KIFUA WAZI NA KUSEMA HAYA....



Leo mwanadada wema sepetu amezidi kuudhihirishia ulimwengu wa fans wake kuwa kijana raisi wa wasafi aka Diamond Platnumz ndio mahabuba wake baada ya kupost video ya mwanamuziki huyo akiwa kitandani kifua wazi kabisaaa huku akiandika “In da middle of his writing session…jus had to distrub him a little”. Mmmh hatari sana!

NANENEPA KIMASOGANGE" NISHA


Mwingizaji wa filamu mwenye vituko, Salma Jabu ‘Nisha’ alibandika picha yake matandaoni ikimuonyesha jinsi alivyo mnono kwa sasa na kuandika haya;
"Dah mbona km sijielewi au sio mm??? Ok nimekumbuka chips za mpemba zinafanya kazi dah!!!sa mbona nanenepa kimasogangee masogange mhhhh si kwa kibuno hiko loool.. niacheni nijiambie mwnyw maana mtakua hamnambii."

Usikose filamu mpya ya mkali huyu, inayokwenda kwajina la SHIDA amabayo siku ya kesho inaingia sokoni.

WEMA SEPETU NA OMMY DIMPOZ NI FULL KUPIKIANA NA KUPAKUA




Wakati mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa macho na kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimap3nzi na mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao.
Japo kuwa Ommy alielezakuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini hii imezidiii.

Mbali na kuonekana wawili hawa kuwa pamoja sehemu mablimbali za starehe toka Ommy atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa  Wema ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao wanamahusiano zaidi ya USHKAJI.
 
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambae na folloers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula.
“Dat moment anapokuja home and umepika chakula alafu analeta pozi at first then unashangaa anaenda sahani mbili.... Talk About Good Food Made Real Good”- Wema aliandika mara baada ya kutupia picha hiyo.
 
Japo kuwa hadi sasa mwanadada Wema Sepetu ajajitokeza kukataa au kukubali juu ya yeye kuwa na mahusiano na Ommy lakini idadi kubwa ya wampambe wake mitandaoni na ifagilia sana hii “Couple”.

PICS NYINGINE KALI ZA LEO TOKA KWA JOKATE, ETI WAZEE WANASEMA ZINAMTOA NYOKA PANGONI


Mrembo Jokate Ameshare nasi Picha zake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram ..
Toa Maksi zako out of 10

PICHA YA LEO, UWOYA NA TATOO KIFUANI.


Pata muda muda kuangalia picha ambayo mkali wa Bongo Movies, Irine Uwoya amei share katka Social Media.

SHILOLE AWAWAKIA WALIOMPONDA KWA KUWA KICHWA WAZI MSIBANI KWA MEZ B



Nawaangalia tu wote mnaonisnich kama ww unajiua ni snich jitoe tu coz hata mm sina time na ww! Tusilazimishane kuwa kama ww mm ni mm na ww ni ww so naona au coz mm ni shilole nisingeenda msiban pia mngechamba oooh wasanii hamjaliani sasa mm nimekwenda lakin bado oooh nywele
 sijafunika! Plzzz tusiingiliane mbona hamna jema nyinyi loh! Mnikome nafanya kile ambacho naweza kufanya kwa wakati huo so tuheshimiane (tusi) tena nyie ambao mnasema ooooooo hujafunga kitamba kichwani hata misiban hamjaww kwenda 

HATIMAYE MILLARD AYO AMILIKI STUDIO YAKE YA RADIO


Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini
hii na baadae watu wangu francis_ayo na abdul8819 wa pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa. 

KUMBE DIMPOZ NI KUWADI WA KIGOGO ANAE MMILIKI WEMA SEPETU KWA SASA.


HABARI ya mjini ni kwamba, lile p3nzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akiwa na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo awe mp3nzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye ndiye anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.
“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma.
“Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye chanzo cha Wema kummwaga Diamond, alimpotezea kwa sababu ya maslahi zaidi, hata kwenye bethidei ya Wema mwaka jana, kigogo huyo ndiye aliyegharamia vitu kibao hadi kusababisha Diamond ahoji,” kilisema chanzo chetu.
Jitihada za kumsaka kigogo huyo ili azungumzie ishu hiyo hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Dimpoz na kusomewa tuhuma hizo, alijibu:“Watu watambue kuwa uhusiano wangu na Wema upo kwa ajili ya ‘project’ zangu, niacheni please niinjoi maisha yangu kuhusu huyo kigogo muulizeni vizuri Wema mwenyewe,” alisema Dimpoz.
Mwanahabari wetu alipomvutia waya Wema, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“Ujue sasa hivi mimi sitaki malumbano na mtu, najua kila mtu siku hizi anaongea kila anachojisikia, naomba niachwe na maisha yangu, unayoyasema hayana maana,  wanasema kwa sababu hakuna anayemjua mp3nzi wangu wa sasa sina muda wa kubishana.”
Hivi karibuni, wakiwa Sauz, Wema na Dimpoz, picha zao wakiwa kimahaba zilivuja mitandaoni hivyo kuibuka gumzo kuwa huenda kwa sasa nao wanatoka.

JACQUELINE PENTEZEL, HANA MPANGO WA KURUDI TENA NDOANI


BAADA ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, Gadna Dibibi, mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa tena.
Mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’.
Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake.
“Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,” alisema Jack.
Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika map3nzi.

ANGALIA DIAMOND ALIVYOMKAMATA "KALIO" ZARI THE BOSS LADY, NDO HABARI YA MUJINI.


Diamond Platinumz amedhihirisha ile research ya Uswaz iliyosema kwamba now days wanaume wanahusudu sana Makalio, na ikafika kipindi hawatajali how and where watayafanyia yao makalio hayo, jionee mwenyewe hiyo pic jinsi Diamond Platnumz alimvomkamata Kalio Mp3nz wake, Zari the Boss Lady...

BARUA YA JACK AKIWA GEREZANI, ALIA NA USALITI WA P3NZI LAKE KWA JUX, DIAMOND NA ZARI NA SKENDO ZA MASTAA WA BONGO



Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.

Modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’.
BARUA KUTOKA CHINA
Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani map3nzi hayachagui hasa kama ana furaha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike map3nzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika Jack.
DIAMOND, ZARI
Mbali na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo alionesha kushtushwa na p3nzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh! Wala hawatadumu maana map3nzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond Platnumz) atahamia South.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakiwa kwenye pozi.
KAJALA Vs WEMA
Pia video queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan (ya Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la Wema na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies walishazoeleka kugombana na kupatana.
Bifu hilo ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK) huku akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa wako hivyo kila muda, kawaida yao.”
JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malov3e na s3xy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.
Juma Khalid ‘Jux’, akiwa na mp3nzi wake Vanessa Mdee.
“Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack.
Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapema hivyo hatakaa jela miaka yote sita.

JB ALIA NA JK, MAANA WATAKUFA MASKINI.


NGULI wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao, anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashungulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.
Nguli wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’.
JB alitoa ombi  kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale wanapopeleka filamu zao sokoni.
“Rais wetu alitoa kauli kuwa anawashungulikia wale wote wanaohusika na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie,” alisema JB.

DIAMOND AELEZA KWANINI ALISHINDWA KUFIKA MSIBANI KWA BABA YAKE DULLY SYKES



Diamond Platnumz ni miongoni mwa
marafiki wa karibu wa msanii Dully Sykes
ambaye weekend iliyopita alimpoteza baba
yake mzazi Ebby Sykes, lakini hakuweza
kuhudhuria msiba huo kutokana na sababu
ambazo amezitoa leo.
Diamond ambaye wakati msiba huo
unatokea alikuwa Zanzibar na mp3nzi wake
Zari, ameelezea sababu zilizomfanya
kushindwa kuhudhuria mazishi.
“Watu waliniona niko zanzibar lakini
walikuwa hawajui nimeenda kufanya nini,”
Diamond
ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM.
“Usiangalie kila unachokiona Instagram
ukajua mtu labda kwasababu alikuwa


anafanya starehe. Niko katika kipindi
ambacho sio kizuri kwangu mimi na familia
yangu kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi
kuvizungumza lakini, na siwezi kuviweka
kwenye media ndo maana watu wengine
wanaweza kuniona nacheka lakini […
kwanza mama yangu anaumwa na anaumwa
sana sijawahi kulizungumza hili ndo
nalizungumza hapa, hapa ninapoongea na
wewe yupo India, kuna vitu vingi
vinaendelea, siwezi kusema nilikuwa
Zanzibar nafanya nini, inawezekana ikawa
ndo sababu iliyonifanya mpaka mimi
nikachelewa kwenda kwenye msiba, lakini
inawezekana labda mimi ndio nilikuwa mtu
wa kwanza kutoa pole katika social networks
zangu mimi.”
“Unajua wakati mwingine ni vizuri kwenda
kuzika lakini inawezekana mtu akawa
ameenda kuzika lakini mi nikawa sijaenda
kuzika nikawa nimefanya kitu cha maana
kuliko wale walioenda kuzika kwasababu
huwezi kujua nilifanya kitu gani. Nilisikia
niliambiwa watu walikuwa wanongea sijui
Diamond hajafika lakini naamini kuna watu
wengi hawakufika na kila mtu hakufika kwa
sababu fulani. Dully mi ni kama kaka yangu
kabisa ni mtu ambaye amenisaidia vitu vingi
sana isingewezekana kabisa niko ninanafasi
nishindwe kwenda kwenye msiba.”
“Ukiacha tu Dully mwenyewe kwanza mtu
aliyefariki ni kama mzee wangu, na mtu
ambaye amefanya kitu kikubwa katika sanaa
hii ya muziki na mimi nimefika hapa yeye
pia ana mchango wake, so haikuwa rahisi eti
mimi nisiende tu nikiwa sina sababu,
kulikuwa na sababu na ndio maana.”
Alimaliza Diamond.

ZARI APONDWA KWA KUPENDA KUMUIGA IGA WEMA SEPETU


Cheni na pete alizojinunuliwa Wema Sepetu siku za Nyuma
Baada ya Zari Kupost Picha Akionyesha Pete na Cheni ya Dhahabu aliyonunuliwa na Mp3nzi wake Diamond Kama zawadi huko Instagram limezuka jambo mashabiki wa Wema wakisema Anamwiga mtu wao kila anachofanya …Jisomee hapa huyu ni Shabiki mkubwa wa Wema Amendika hivi :
Mtaawapili

“Bibi zaituni acha tabia zako za copy na kupaste sio kila anachofanya wema na lazima ufanye utaumbuka bure…..nyie team nyoko nyoko ebu tafuteni kitu cha kufanya au mwambeni huyo bosslady awape kazi ya kufua ile sidiria kauka ni kuvae mfyuuuuu.hivi nyie mnajuwa kama wema anapenda gold sana na anazo nyingi mno.alipokuwa ck alipelekwa dubai kununuwa gold tu Google utaona .kama mtakumbuka vizuri wema na domo walikuwa china walinunua gold za gram 50 kila mtu

BREAKING NEWS :MEZ B AFARIKI DUNIA


Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake amefariki Dunia. Mez B alikuwa akiuguliwa na homa ya mapafu [Pneumonia] na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa siku ya tatu toka anatumia dawa hizo. 



Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe drip ila hali yake ikawa mbaya zaidi, wakati wanampeleka hospitalini alifia walipofika mapokezi. Jirana amelezea haya. 

Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga