Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » DIAMOND AELEZA KWANINI ALISHINDWA KUFIKA MSIBANI KWA BABA YAKE DULLY SYKES



Diamond Platnumz ni miongoni mwa
marafiki wa karibu wa msanii Dully Sykes
ambaye weekend iliyopita alimpoteza baba
yake mzazi Ebby Sykes, lakini hakuweza
kuhudhuria msiba huo kutokana na sababu
ambazo amezitoa leo.
Diamond ambaye wakati msiba huo
unatokea alikuwa Zanzibar na mp3nzi wake
Zari, ameelezea sababu zilizomfanya
kushindwa kuhudhuria mazishi.
“Watu waliniona niko zanzibar lakini
walikuwa hawajui nimeenda kufanya nini,”
Diamond
ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM.
“Usiangalie kila unachokiona Instagram
ukajua mtu labda kwasababu alikuwa


anafanya starehe. Niko katika kipindi
ambacho sio kizuri kwangu mimi na familia
yangu kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi
kuvizungumza lakini, na siwezi kuviweka
kwenye media ndo maana watu wengine
wanaweza kuniona nacheka lakini […
kwanza mama yangu anaumwa na anaumwa
sana sijawahi kulizungumza hili ndo
nalizungumza hapa, hapa ninapoongea na
wewe yupo India, kuna vitu vingi
vinaendelea, siwezi kusema nilikuwa
Zanzibar nafanya nini, inawezekana ikawa
ndo sababu iliyonifanya mpaka mimi
nikachelewa kwenda kwenye msiba, lakini
inawezekana labda mimi ndio nilikuwa mtu
wa kwanza kutoa pole katika social networks
zangu mimi.”
“Unajua wakati mwingine ni vizuri kwenda
kuzika lakini inawezekana mtu akawa
ameenda kuzika lakini mi nikawa sijaenda
kuzika nikawa nimefanya kitu cha maana
kuliko wale walioenda kuzika kwasababu
huwezi kujua nilifanya kitu gani. Nilisikia
niliambiwa watu walikuwa wanongea sijui
Diamond hajafika lakini naamini kuna watu
wengi hawakufika na kila mtu hakufika kwa
sababu fulani. Dully mi ni kama kaka yangu
kabisa ni mtu ambaye amenisaidia vitu vingi
sana isingewezekana kabisa niko ninanafasi
nishindwe kwenda kwenye msiba.”
“Ukiacha tu Dully mwenyewe kwanza mtu
aliyefariki ni kama mzee wangu, na mtu
ambaye amefanya kitu kikubwa katika sanaa
hii ya muziki na mimi nimefika hapa yeye
pia ana mchango wake, so haikuwa rahisi eti
mimi nisiende tu nikiwa sina sababu,
kulikuwa na sababu na ndio maana.”
Alimaliza Diamond.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga