Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

DANCER WA DIAMOND AKUBALI KIAINA KUHUSIKA NA UJAUZITO WA AUNTY EZEKIEL


Kuanzia magazeti, mitandaoni mpaka kwenye redio… kwenye mtiririko wa stori za mastaa wa Tanzania zilizoongelewa au kuandikwa sana ndani ya wiki 6 zilizopita, hii ya mwigizaji Aunty Ezekiel kuwa na ujauzito na dancer wa Diamond Platnumz aitwae Mose Iyobo imo kwenye orodha. 
Wawili hawa walitajwa kuwa mapenzini kitambo na hata ujauzito wa Aunty iliandikwa kwamba baba kijacho ni Mose japo Aunty mwenyewe alikanusha.
Nakumbuka alisema ‘kuhusu taarifa za mimi kupewa ujauzito na Mose Iyobo, hizo taarifa mwenyewe nasoma kwenye magazeti nasikia kwenye Radio kama unavyosema lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani‘ 

Pamoja na kukanusha huko, wawili hawa wameendelea kuchukua nafasi kwenye vichwa vya habari kutokana na post zao wenyewe kwenye page za instagram wanazomiliki ambapo wiki mbili zilizopita Mose aliweka hii picha hapa chini huku Aunty akiwa juu yake kitandani na kuandika ‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila……..?

MIMBA YA AUNTY EZEKIEL NA SAKATA LA WAZIRI NYALANDU KUWA BABA


Hatimaye Waziri wa MaliAsili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mke wake Faraja Kotta wamejibu tetesi zilizowahi kuandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa waziri huyo alikuwa na uhusiano wa kimap3nzi na muigizaji wa filamu, Aunty Ezekiel.
Magazeti hayo yaliandikwa kuwa Nyalandu na Aunty walikutana nchini Marekani kwenye hafla ya ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Nyalandu amedai kuwa hilo ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwakuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.

“Unajua mpaka nikaanza kucheka,” alisema Nyalandu. 
“Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina deal kabisa. 
Pili hata kwa anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza, unaona wanaliamplify, story ambayo haipo wanaipeleka,” aliongeza.
“Mimi nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunty Ezekiel katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndo hiyo hiyo siku nimemuona, nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.
Tumekutana naye yeye akiwa mwalikwa pamoja na madj wengine wa Bongo Flava katika tukio lenye watu wengi watanzania katika nchi ya America. 
Mimi nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwahiyo kwanza katika hiyo situation ya kuwa America atakuwa aliniona kwa saa moja katika ule mkutano lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye.
Kuna wasichana wengi sana ambao nilishakula nao dinner, tunakutana nao kwenye chai, yaani hao tu ndio ingebidi waseme. Lakini huyu binti hata namba yake ya simu sijawahi kuwa nayo hata hapa ninapozungumza,” alisisitiza.“Kwanza waliandika kwenye gazeti moja nafikiri ni Jamhuri – lile gazeti ambalo limeniandika mpaka wino umewaishia, yaani wamekosa cha kuandika. Wakasema kwamba ‘Waziri Nyalandu atumia mamilioni ya fedha za serikali na Aunty Ezekiel akiwa Marekani’.
Ikaja kama sensational story. Tukarijibu kiserikali kwamba sio kweli kwasababu yeye alikuwa na safari yake, mimi na safari yangu na haikuwa na uhusiano, ubalozi wa Marekani wakatoa statement. 
Lakini baada ya wiki tatu hasa baada ya kutangaza nia ya kwamba itakapofika saa nategemea kuchukua fomu ya chama cha mapinduzi kugombea uongozi wa nchi yetu, nina matumaini makubwa kwamba saa ya kufanya mabadiliko ya aina fulani ya kiuongozi imefika, saa ya kuiongoza nchi hii kwa wakati tulionao imefika na nina matumaini makubwa tutaungana na watanzania wenzangu kufanya jambo la mbele, sasa ile ndio ikaibua vitu vingine.”
“Wakasema ‘huyo Nyalandu sasa huyo dada Aunty Ezekiel ana mimba’ kwahiyo wakasema ana mimba ya mheshimiwa Nyalandu.
Ukweli ni kwamba siku hizi suala la mimba ilikuwa ni zamani unaweza ukasingiziwa. Siku hizi mimba kuna kitu kinaitwa DNA, hata ukichukua tu damu ya kwako na ya kwake sasa hivi unaweza ukaonesha ni kweli au sio kweli. Hakunaga uongo kama huo siku hizi.”
Nyalandu alilisitiza kuhusu kujenga jamii inayosema ukweli na sio kutunga uongo kitu ambacho ni dhambi itakayokufuata mwenyewe.
Awali mke wake, Faraja alidai kuwa habari hiyo haikumsumbua kwakuwa anamwamini mume wake na kwamba sio habari ya kwanza ya aina hiyo kuisikia.
Faraja aliyewahi kuwa Miss Tanzania alidai kuwa ndoa yao haikutetereka kwa kiasi chochote kufuatia uzushi huo.
“Hazikuleta utofauti wowote,” alisema Faraja. “Uzuri sijui niseme nimekuwa sugu. Maneno mengi yameshasemwa kuhusu uhusiano wetu, kuhusu ndoa yetu, kuhusu map3nzi yetu. Lakini katika huo muda wote tukajifunza kwamba uaminifu na upendo ni kitu muhimu sana.
Mkipendana, mkiaminiana maisha hayatoweza kuwatatiza. Na hata kama nikisikia neno kwa mfano leo hii au hata kesho kwangu mimi kwanza natambua kwamba yeye ni kiongozi wa kitaifa, kiongozi wa nchi yetu na ni kiongozi wa familia yangu kwahiyo jambo likisemwa, mara nyingi sana narudi nyuma na kumwangalia yeye kwa mimi ninavyomfahamu , mimi kama mke wake na naamini kwamba mimi namfahamu vilivyo pengine labda katika wanawake ukiacha mama yake mzazi, mimi hapa ndio ninamfahamu sana kuliko wanawake wote.”
“Kwahiyo yaani hainisumbui na ninamfahamu, ninamuamini, ninamheshimu na ninampenda sana.

MTOTO KUMPA FARAJA AUNTY EZEKIEL


Mkali wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
MKALI wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel
amefunguka kuwa pamoja na kupoteza
wazazi wake miaka kadhaa nyuma pindi
akiwa mdogo, anaamini mtoto
atakayejifungua atamfuta machozi ya muda
mrefu ya kuwapoteza wazazi wake.
Aunty alifunguka ishu hiyo kwa upole,
ambapo alisema kifo cha wazazi wake
kilimfanya kulelewa na bibi yake pamoja na
shangazi.
“Kutokuwa na wazazi ni pigo kubwa kwangu,
lakini hata hivyo naamini kwamba
mwanangu atakuwa na furaha ambayo
nilikuwa naipata kutoka kwa wazazi wangu,
atakuwa ni zaidi ya rafiki au ndugu, ndiye
atakayenifuta machozi ya kufiwa,” alisema
Aunty.

WEMA NA AUNTY EZEKIEL WAFUMWA WAKICHEKA JUU YA KABURI LA MAN NGWEA



INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!

Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.

Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.

ENEO LA TUKIO

Tukio hilo lililonaswa zimazima na kamera za Risasi Jumatano, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro.

ILIVYOKUWA

Aunt ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya ‘kruu’ ya Wema, akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu, Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.

CHA AJABU SASA

Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!

Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo, nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-

WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO

Ni dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka. Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.

Wakati Wema akionesha ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.

WEMA AJIELEZA KWA RISASI

Baada ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu, paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu ya kaburi la staa huyo.Wema: “Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”

KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?

Awali, mastaa hao na wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma.Wakiwa wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo miongoni mwa mambo waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi la Ngwea na kuangusha dua fupi.

Hata hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo la Wema na watu wake hatimaye walifanya dua fupi ya kumuombea malazi mema Albert Mangweha.

KUMBUKUMBU MUHIMU

Mangweha alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6 2013

Powered by Blogger.

KADINDA NA AUNT EZEKIEL KULIKONI?



MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda na mwigizaji Aunt Ezekiel wamenaswa chobingo wakiwa katika pozi tata.Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Klabu ya 71, Tegeta-Kibaoni jijini Dar kulipokuwa na shoo ya kuukaribisha mwaka iliyoandaliwa na Kampuni ya Endless Fame.


“Mh jamani huyu Aunt si ana mume? Halafu si ana kibuzi chake kingine? Huyu Martin naye imekuwaje tena,” alisikika jamaa mmoja ukumbini humo.

Alipoulizwa Aunt kuhusu tukio hilo, alisema wamekumbatiana kirafiki tu na si
wapenz

AUNTY EZEKIEL AMWAGA CHOZI LOCATION


DIVA wa Filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel hivi karibuni alijikuta akiangua kilio alipokuwa eneo la kuigiza ‘location’ pande za Kijichi jijini Dar baada ya kusumbuliwa na jino ambapo alishindwa kuvumilia maumivu.

Akizungumza  na Amani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Aviation, Aunty alisema kuwa  alijikuta uvumilivu unamshinda na kuangua kilio kwani kila alipojaribu kufanya kazi alishindwa.

“Huwezi amini sikupenda hata kuongea na watu, jino naliheshimu sana kwani maumivu yake kama hayajakufika unaweza kuona mtu  anajifanyisha,” alisema Aunty.

Baada ya tukio hilo, Aunty aliyekuwa amejichimbia kwenye kambi ya William Mtitu amesitisha zoezi la kupiga picha hadi hali yake itakapokuwa nzuri.

TETESI: WEMA NA AUNTY EZEKIEL WANASAGAN@?


Kwa tathimin ya haraka tutasema ni wana show l0ve kati yao hawa wasanii wetu, though Gossip iliyotapakaa kitaa ni kwamba wawili hawa wana cheza ile michezo yetu isiyofaa ya kidigitali.

AUNTY EZEKIEL NA SKENDO YA CHENI YA MILIONI 6




NYOTA wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel ameingia matatani na maafande wa Kituo cha Polisi Pangani, Ilala jijini Dar akidaiwa kutokomea na cheni ya Shabani Limo yenye thamani ya shilingi milioni 6.
Nyota wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel akiwa Bongo.
Kwa mujibu wa chanzo, mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa Shabani na kuazima cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya muda jambo ambalo hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri kwenda Marekani kutangaza utalii wa ndani.
Baada ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema.
Ilidaiwa kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani.
Jumatano iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.
Aunty Ezekiel akiwa Marekani alipokwenda kutangaza utalii wa ndani.
“Ni kweli hapa kuna hiyo kesi na ilianzia Oysterbay japo hatuwezi kuitolea maelezo ya kina kwa vile jambo lenyewe limekaa kimapenzi zaidi,” alisema askari mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Shabani alipotafutwa kwa njia ya simu na kuulizwa juu ya taarifa hizo alisema alimuazima Aunty cheni hiyo ambapo naye alimpa shoga yake.
Aunty alipopatikana na kuulizwa alikana kumfahamu Shabani na kudai hana taarifa zozote za kuwepo kwa ishu hiyo.“Mh! Huo ni uzushi, hakuna kitu kama hicho na wala hizo taarifa sizifahamu, huyo mwanaume simjui ndiyo kwanza namsikia kwako,”alisema Aunty.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga