Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

SASA NI PROJECT YA YUSUPH MLELA NA ESHA BUHETI

 
“Nawatakia safari njema ndugu zangu mungu awatangulie kwa kila jambo najua mungu ndio anayepanga kuna mengi ila hili limeanza kwenu na milango mnaifungua wazi msiwe kama wangine wenye kucheka machoni uku moyo umekunjama. Hahahahaha.alianza Wastara . Mona . Sasa zamu yenu Mlela na Esha mkatuwakilishe vyema . USA . CHAO pamoja wasaniii wadogo  Steven Mengere 'Steve Nyerere’ aliekuwa raisi wa Bongo Movie Unity alibandika andiko hili mtandaoni mara baada ya kuweka picha ya wawili hao hapo juu.

NANENEPA KIMASOGANGE" NISHA


Mwingizaji wa filamu mwenye vituko, Salma Jabu ‘Nisha’ alibandika picha yake matandaoni ikimuonyesha jinsi alivyo mnono kwa sasa na kuandika haya;
"Dah mbona km sijielewi au sio mm??? Ok nimekumbuka chips za mpemba zinafanya kazi dah!!!sa mbona nanenepa kimasogangee masogange mhhhh si kwa kibuno hiko loool.. niacheni nijiambie mwnyw maana mtakua hamnambii."

Usikose filamu mpya ya mkali huyu, inayokwenda kwajina la SHIDA amabayo siku ya kesho inaingia sokoni.

PICHA YA LEO, UWOYA NA TATOO KIFUANI.


Pata muda muda kuangalia picha ambayo mkali wa Bongo Movies, Irine Uwoya amei share katka Social Media.

JB ALIA NA JK, MAANA WATAKUFA MASKINI.


NGULI wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao, anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashungulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.
Nguli wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’.
JB alitoa ombi  kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale wanapopeleka filamu zao sokoni.
“Rais wetu alitoa kauli kuwa anawashungulikia wale wote wanaohusika na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie,” alisema JB.

TOP 10 YA WAREMBO WA AFRICA WANAOVUTIA ZAIDI KATIKA MOVIE INDUSTRY


Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku moja zikatimia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa  umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.
9. Omotola Jalade Ekeinde.
Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na mwananamuziki.
8. Chinyere Yvone Okoro
Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
7. Jackline Wolper.
Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali inayomfanya autunze urembo alionao.
6. Genevieve Nnaji.
Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna anavyouvaa uhusika.
5. Jackie Appiah Agyemang.
Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni, huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.
4. Nadia Buari.
 Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.
3. Ini Edo.
Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike kwenye filamu nyingi za Nigeria.
2. Stephanie Okereke Linus.
Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu nyingi.
1.Rita Dominic.
Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu. Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana wa kiurembo.
Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake

NATAFUTA MUME AMBAYE SIO STAA KAMA RAY" JOHARI


STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘Ray’ bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu. Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke.
Staa mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula ‘Johari’.
Kwanza sihitaji mwanaume wa kunioa awe staa hata siku moja, nataka tu awe wa kunijali na kunithamini na kingine awe mchapakazi kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtafutaji,” alisema Johari.
Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimap3nzi na nyota wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi map3nzi yao yalikuwa ni ya ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ na wala si ndoa.

TIKO WA BONGO MOVIE ASAKA NDOA


MSANII wa filamu Bongo, Tiko Hassan ‘Tiko’, amefunguka kuwa anashindwa kuolewa kutokana na kukosa mwanaume wa kufanya hivyo, ila yupo tayari kupokea barua ya uchumba kutoka kwa mwanaume yeyote atakayehitaji kufunga naye ndoa.
Msanii wa filamu Bongo, Tiko Hassan ‘Tiko’.
Akimwaga ubuyu na Uwazi, Tiko alisema bado hajapata yule ambaye anaweza kuwa mume wake hadi sasa japo amesubiri kwa kipindi kirefu.
“Akitokea mwanaume na kuja kutoa barua nyumbani hata leo, nipo tayari na naweza kuishi naye lakini haina maana kwamba kila mwanaume anaweza kuja kwetu na kufanya hivyo. Mwanaume ambaye atakuja anatakiwa awe anajitambua ili tuweze kujenga familia,” alisema Tiko.

AMANDA WA BONGO MOVIES ANENA MAZITO KUHUSIANA NA MAP3NZI



Stori: Gladness Mallya

MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi amefunguka na kueleza siri nzito kuwa hawapendi wanaume kutokana na kufiwa na mchumba wake muda mfupi baada ya kuzungumza naye miaka…iliyopita.
Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Amanda Poshi. Akipiga stori na gazeti hili, Amanda alisema stori ya mwanaume ambaye alikuwa ni mchanganyiko wa Mgiriki na Mbongo aliyejulikana kwa jina la Alan kila akiikumbuka huwa inamuumiza moyoni kwani ni mwanaume aliyekuwa na map3nzi ya dhati.

“Huwa naumia sana nikimkumbuka Alan mchumba ambaye alikuwa ameshajitambulisha kwetu lakini akafariki kwa ajali nusu saa baada ya kuzungumza naye kwenye simu akiwa Ugiriki huku akiniachia ujauzito wa miezi mitano lakini ilipofika miezi saba mtoto alifia tumboni. “Tangu hapo sipendi wanaume na sijawahi kumpata mwanaume mwenye upendo wa dhati kama huyo,” alisema Amanda.

AMZING PHOTOS OF KAJALA MASSANJA AND DAUGHTER, HOW LOVELY......!!!!


Cheki some of amazing photos za muigizaji nyota wa Bongo Movie, Kajala Massanja akiwa na Mwanae, aki show luv ile ile...... mama kijana, mtoto ndo usiseme...... Watch more pics below:-







RAY NA JOHARI HAWAKUWA WAP3NZI" CHUCHU HANS


Mrembo na muigizaji wa filamu Chuchu Hans ameyameha hayo kwenye alipokuwa akiohijwa kwenye kipidi cha Take One kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds TV.
“Ninachojua JOHARI hakuwahi kuwa na mahusiano yoyote ya kimap3nzi na RAY ila ni Partners in Business tofauti na watu wanavyofahamu"
Chuchu Hans alisisitiza kuwa bado yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji na muongozaji wa filamu, Vicent Kigosi ‘Ray’mbali na tetesi za zilizoenea kuwa wameteman.
Ray anadaiwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimap3nzi na Johari ambae kwa pamoja wanamiliki kampuni ya kutengeneza filamu ya RJ.




BATULI ALISIFIA JICHO LAKE, LINASEMA YA MOYONI ZAIDI YA MDOMO...


Urembo: Ni kweli macho ya naonge lakini hili la mwigizaji Batuli linaongea zaidi. Haya sio maneno yangu ni bali ni maneno yake mwenyewe alioyaandika kwenye ukurasa wake wa INSTAGRAM mara baada ya kutupia picha hiyo hapo juu akiwa amerembua.


“Look into my eyes and hear what I'm not saying, for my
eyes speak louder than my voice ever will.....”
Haya jamani wale mliosoma English Mediam, hebu malizieni hizo deshidesh...

SIKU 3 ZA SEGEREA ZILIVYOMTIA DOA MREMBO HUYU WA BONGO MOVIES


Mwigizaji wa toka kitambo, Davina Yahaya ‘Davina’, amesema kamwe hatokuja kusahau mateso aliyowahi kuyapata akiwa Gereza la Segerea ambapo alikaa kwa siku tatu.
Akipiga stori na GPL, Davina alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwaka 2012 ambapo ilikuwa ni tatizo la kifamilia lililosababisha kutupiwa huko japokuwa hakuweza kuliweka hadharani kwakuwa bado lipo mikononi mwa sheria.
“Huwa natokwa machozi na kamwe sitokuja kusahau mateso niliyoyapata Segerea. Nilikuwa kwa siku tatu lakini niliona kama mwezi, hali ya hewa, sehemu ya kulala zilikuwa mbaya sana, wingi wa watu na sikupata hata nafasi ya kulala zaidi ya kukesha nikilia,” alisema Davina.

AMANDA AJITAMBA KUJIUZA MAANA *PAPU*CHI* NI YAKE HAJA AZIMA KWA MTU


Mwigizaji wa filamu, Amamnda Poshi amewatolea uvivu wanaomponda kwa kuvaa nguo fupi huko Instagram. 

Amanda  amewataka  mashabiki  wake  kuachana  na  maisha  yake  binafsi  kwa  madai  kuwa  kama  maisha  yake  yanategemea  kujiuza  kingono  basi  wamwache  maana  anayoiuza  ni  Papu**chi  yake  mwenyewe  na  hajaazima  kwa  mtu.

Huu  ni  ujumbe  wake  alioundika: Instagrameee naipenda sanaaa..naipenda na watu wake nawapenda sanaaa coz ni sehem unayopangiwa uishi vipi,uvae vipi ,ulale wapi,uwe na bwana wa aina gani na ukikaa vibaya utapangiwa mpk chakula cha kutia tumboni tena kwa pesa yako...
  
Naomba ieleweke kila mtu anauhuru wake...kwangu me msinipangie mavazi wala jinsi ya kuishi,nikivaa nguo fupi ni mimi,niwe na miguu mibaya,mapaja mabaya ,sura mbaya haimuhusu mtu ....manina c mzae wenu!!!! mlikuwa mnasubiri mpk mama amanda azae ndio mkosoe mxiuuuuu....
  
Kuhusu nguo mtakosoa sana na makelele pigeni ila kuvaa vimini siachi maana hakuna anayenivisha wala kuninunulia...nanunua kwa pesa yng na kama mtu kuvaa nguo fupi anauza basi acheni kupiga kelele maana nauza papuchi yng sijaazima ya mtu.... 
  
"Niwatakie usiku mwema wote hahahaaaa nawapenda sana



MASTAA WA KI BONGO WENGI "WANAJIUZA"



Msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella’.

IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya mastaa wa kike Bongo Muvi wanaishi kwa kuuza miili yao.

Akizungumza na waandishi wetu, msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella’, alisema wasanii wengi wanaishi maisha ya thamani wakati kiuhalisia kazi yao haiwaingizii kipato kinachofanana na maisha ya thamani wanayoishi hivyo kuamua kujiuza.



“Filamu hazilipi, wengi tunajiuza. Bajeti yenyewe ya muvi ni ndogo, wasanii wengi wanataka kulipwa katika muvi moja, haiwezekani kumiliki vitu vya thamani ndiyo maana tunaamua kujiuza.
“Hakuna msanii anayeishi maisha ya kutegemea filamu, kwanza hazilipi kivile kama ambavyo wengi wanavyosema, ukweli ni kwamba wasanii tunajiuza ili tupate pesa ndiyo ituweke mjini tuendelee kung’aa,” alisema Bella.

Wakizungumza na waandishi wetu kwa masharti ya kutotajwa majina yao walikiri kuwa wasanii wengi wanajiuza kutokana na kutaka kuendana na hadhi ya umaarufu.



Mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’. 

“Ukweli ndiyo huo, hakuna anayeweza kuishi maisha ya kumiliki magari ya kifahari, nyumba kwa kazi ya sanaa ni uongo mtupu,” alisema mmoja wa wasanii hao.

Alipoulizwa kuhusiana na ishu ya kujiuza, mwigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ alisema: “Binafsi naishi maisha ya kawaida, najua wapo wanaojiuza, nawapa pole maana wanapenda maisha ya mteremko, mimi siyaungi mkono kabisa.”

Alipotafutwa mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’ naye alikiri: “Wasanii wengi Bongo wanategemea kuhongwa na mabwana tofauti ili wapate jeuri ya kujifanya wanazo, utakuta anatengeneza nywele za milioni mbili au kanunua nguo ya milioni kumi huo ni uongo tu, filamu hazilipi kiivyo wengi wanataka kuiga maisha ya wasanii wa nje.”

LULU NA MAONI YAKE KUHUSIANA NA FASHION


Kwa mtazamo wake Msanii Lulu Michael amedai kuna tofauti kati ya style na Fashio, kwake ameona Fashion ni kile tunachonunua na Style ni Kile tunachovaa. nahisi hapa kachemka sema kwa kuwa ni staa tuimezee.

KWA HILI MPENZ WA WOLPER ARINGE TU...


Ni jambo la kawaida kwa binadam kujiachia hasa pale tunapokuwa katika hali fulan ya raha ama kujawa na hisia nzuri za kimahaba. Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii wa Bongo Movie, Mrembo Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hlo ndio pozi analohusudu pindi anapokuwa ana chat na wake wa moyo.....

Je wewe ushawahi kujitathmin kuhusiana na pozi gani hukuhamasisha unapokuwa unawasiliana na mwenza wako...???

LUNGI ATOA ONYO KWA WANAOMNYEMELEA BWANA WAKE


Staa wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga amesema mwanaume aliyezaa naye (jina ni siri yake) anampenda sana na mwanamke asiyejipenda amshobokee aone kitakachompata.
Staa wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga.
Akipiga stori na Ijumaa Lungi amesema anajua kuwa wapo wanawake ambao wakiamua kutembea na waume za watu hawashindwi lakini akasema, kwa bwana wake aliyezaa naye akigundua kuna anayemnyemelea, atakufa naye.
“Nawataha-dharisha tu wasije kuthubutu kutoka na mwanaume ambaye ananipa jeuri hapa mjini kwani nitawafanyia kitu mbaya. Wanaonijua wananielewa na wanaujua moto wangu ninapoingiliwa kwenye anga zangu,” alisema Lungi.

MZAZI WA BINTI AANZISHA VARANGATI BAADA YA KUFUMANIWA MWANAE AKICHEZEWE KWENYE SCENE YA MAHABA


Baba mmoja ambaye jina halikupatikana mara ameshusha kichapo kwa wasanii ambao ni maprodyuza waliokuwa wakimchezesha mwanaye filamu bila ridhaa yake.
Baba huyo akizuiwa ili asiendelee kushusha kichapo hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilijiri juzikati, maeneo  ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar ambapo awali binti huyo ambaye ni msanii chipukizi wa kuigiza aitwaye Jeniffer alidaiwa kupigwa mkwara na baba yake kuwa asijishughulishe na masuala ya muvi na badala yake ajikite kwenye masomo yake kufuatia tasnia hiyo kuhusishwa na skendo za ng0no.
Ilidaiwa kwamba, Jeniffer alikaidi amri ya mzee wake huyo na kwenda kinyemela kurekodi vipande kadhaa vya muvi ya kikundi chao ambapo taarifa zilimfikia baba yake huyo na kuamua kutimba lokesheni.
Baba huyo akijiandaa kumvaa prodyuza huyo.
Ilisemekana kwamba, katika hali iliyompandisha zaidi hasira, mzee huyo alipofika maeneo hayo alimkuta mwanaye katikati ya ‘scene’ ya mahaba aliyokuwa akiigiza na msanii anayetamba kwenye Tamthiliya ya Siri ya Mtungi, Daudi Michael almaarufu Duma.
Baada kushuhudia bintiye ‘akigaragazwa’ kimahaba, mzazi huyo alimvaa msanii Duma na kumshutumu kumharibia binti yake ambapo alimpa kibano pamoja na maprodyusza wenzake kabla ya kuamuliwa na wasanii wengine waliokuwepo eneo hilo.
Watu waliokwepo kwenye sakata hilo wakiamulizia.
Ilidaiwa kwamba, alipoona amewakungung’uta vya kutosha, baba huyo aliondoka na bintiye akiahidi kwenda ‘kumsulubu’ nyumbani kwa kuwa amekuwa sikio la kufa.
Kwa upande wake, Duma alibaki na majeraha mgongoni ambayo hadi waandishi wetu wanafika eneo la tukio yalikuwa yakitoka damu.
Duma alipoulizwa kuhusiana na mzee huyo, alikana kumfahamu na kudai kuwa alipewa mamlaka ya kumtumia binti huyo kwenye muvi na kaka wa msichana huyo.
Baba huyo akiondoka na binti yake.
“Nilimuomba Jeniffer kwa kaka yake na alikubali nishuti naye, sasa sijui nitafanyaje maana tulishashuti scene kibao halafu Jeniffer kashindwa kumalizia,” alisema Duma.

ANTI "LULU" HOI HOSPITALI




Staa wa Filamu za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ yupo hoi kitandani baada ya kusumbuliwa na jino la juu ambalo anahofia kulitoa.

Akizungumza na Amani, Aunt Lulu alisema kuwa anajiona amekonda kwa maumivu ya jino tu na kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa marafiki zake anaogopa kwenda kuling’oa.
“Yaani nina siku tatu sili nakunywa tu, vile vitu vigumuvigumu kama kuku na nyama za kuchoma navisikia kwa wenzangu kwani vinanishinda, nikitaka kuangua kilio niviweke mdomoni,”  alisema Aunt Lulu.
Lulu alimalizia kwa kuwaomba mashabiki wake wamuombee kwani jino ni ugonjwa mdogo sana lakini kwake umekuwa ni mtihani mkubwa kwani kila akitaka kwenda kuling’oa anapatwa na hali ya woga.

"MASTAA WENGI WANAJIUZA MTANDAONI " ANTI LULU.


Bidada mwenye umbo matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ ameibuka na kueleza kwamba mastaa wamegundua njia mpya ya kujiuza ambayo ni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Aunt Lulu alisema mastaa wengi wa kike wanajiuza kwenye mitandao ambapo mapedeshee waliopo mikoa mbalimbali wakishaziona picha zao huwa wanawatafuta kwa udi na uvumba ambapo wanawapigia simu na kuwatumia fedha na tiketi za ndege ya kwenda na kurudi.

“Yaani mastaa wa kike hatulali unakuta pedeshee anakutumia tiketi ya ndege unamfuata mkoani ukienda usiku asubuhi umesharudi Dar unaendelea na mambo yako ndiyo maana unawaona wasanii wengi wa kike wana fedha lakini kazi wanazozifanya huzioni,” alisema Aunt Lulu

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga