MSANII wa filamu Bongo, Tiko Hassan ‘Tiko’, amefunguka kuwa anashindwa kuolewa kutokana na kukosa mwanaume wa kufanya hivyo, ila yupo tayari kupokea barua ya uchumba kutoka kwa mwanaume yeyote atakayehitaji kufunga naye ndoa.
“Akitokea mwanaume na kuja kutoa barua nyumbani hata leo, nipo tayari na naweza kuishi naye lakini haina maana kwamba kila mwanaume anaweza kuja kwetu na kufanya hivyo. Mwanaume ambaye atakuja anatakiwa awe anajitambua ili tuweze kujenga familia,” alisema Tiko.