STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘Ray’ bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu. Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke.
Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimap3nzi na nyota wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi map3nzi yao yalikuwa ni ya ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ na wala si ndoa.