Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

MAHABA YA BOB JUNIOR YAMBADILISHA MAVAZI MREMBO "SABBY ANGEL"



MSANII anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Filamu Bongo, Sarbrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa  mwanamuziki, Rummy Nanji ‘Bob Junior’ ambaye kwa hivi sasa ndiye mpenz wake amembadilisha mavazi yake aliyokuwa akivaa awali kabla hawajawa pamoja.
Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Filamu Bongo, Sarbrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi.
Akizungumza na Amani, Sabby alisema kuwa mpenzi wake huyo mara nyingi anapenda ajitande nguo na kuwa mtoto wa Kiislamu kama asipokuwa katika ishu za kurekodi kwani anaamini kuwa binti wa Kiislamu anapaswa kuvaa kiheshima.
Mtoto ‘Sabby Angel’ akiwa na Nanji ‘Bob Junior’.
“Nimekamatika sana, yale mavazi yangu ya awali nimeambiwa ‘stop,’ tukiwa katika mazingira ya kawaida ni lazima nijitande na nionekana haswa ni mtoto wa Kiislamu,” alisema  Sabby.

SABBY "ANGEL" NDIO USINGIZI WA BOB JUNIOR, AMFUNIKA MKE WA AWALI KWA MAHABA.



MSANII anayechipukia kwa kasi katika anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa kwa kipindi kifupi ambacho amezama kwenye penzi la staa wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, amempa mahaba mazito kiasi cha kumfanya asimkumbuke aliyekuwa mkewe.
Msanii wa filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi na 'Bob Junior' kimahaba.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Sabby alisema kuwa ameamua kuonyesha ufundi wake wote wa kimahabati kwa msanii huyo kwani ni mwanaume ambaye amemuona mwenye mapenzi ya dhati.
‘Sabby Angel’ akipozi.
“Sijawahi kukutana na mwanaume mwenye mapenzi kama huyu na mimi zawadi nitakayompa ni mapenzi mazito na nitamaliza ufundi wangu wote kwake na kamwe hatokumbuka kama aliwahi kuwa na mke kabla yangu,” alisema Sabby.Bob Junior aliwahi kumuoa mwigizaji, Halima Ally kisha wakamwagana baada ya kuzaa naye mtoto mmoja.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga