Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

VENGU WA ORIGINAL KOMEDY APATA AHUENI, KURUDI KWENYE FANI SOON......



MUNGU mkubwa! Vengu is back from hell (Vengu amerudi toka kuzimu). Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’ ameanza kurejea katika ‘fomu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu, Risasi Jumatano linathibitisha.
Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo (jina tunalo), Vengu ambaye kwa muda mrefu alipoteza kumbukumbu kiasi cha kushindwa kuwatambua watu, sasa amejaliwa kwani anaweza kuwafahamu watu mbalimbali wanaopata nafasi ya kwenda kumjulia hali, Kigamboni jijini Dar anakoishi.
AMEANZA KUTOA ‘HI’ KWA WATU
“Bado yupo chini ya uangalizi maalum wa kifamilia, ni watu wachache wanaruhusiwa kumuona, lakini sasa hivi huwezi kuamini, watu wanaofika kumtazama anawatambua na anawapa ‘hi’.
TATIZO USIRI
Kutokana na usiri wa hali ya msanii huyo unaofanywa na familia yake, kumekuwa na maneno chini kwa chini ikiwa ni pamoja na uzushi wa mara kwa mara kuwa, mchekeshaji huyo maarufu, amefariki dunia na kuzikwa kwa siri jambo ambalo si la kweli.
Hata hivyo, katika namna ya kusikitisha, ndugu huyo alisema kuwa kila Vengu anapomtambua mtu anayemtembelea amekuwa akimwaga machozi hali inayoonesha kuwa anarejesha nyuma kumbukumbu zake na kugundua amekuwa mbali naye kwa muda mrefu.
Mfano wa nyumba ya Vengu.
KUREJEA KWENYE FANI
Pia ndugu huyo alisema kwa hali ya Vengu sasa anaweza kurejea kwenye kazi zake za kuchekesha kama zamani zile.“Kwa jinsi ilivyo, Vengu atarejea hivi karibuni katika kazi yake ya kuburudisha akiwa sambamba na wenzake wa Orijino Komedi kwa sababu afya yake inaimarika sana,” alisema ndugu huyo huku akikataa katakata kutoa ramani ya nyumba anayoishi Vengu ili mapaparazi wetu wende wakamjulie hali.
APEWA NYUMBA
Kana kwamba haitoshi, wakati hali yake ikisemwa na ndugu inaendelea vizuri, kuna madai kwamba msanii huyo na familia yake wamepewa nyumba ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni 120, sawa na wasanii wenzake akina Wakuvanga kufuatia mkataba wa kundi hilo na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
“Ni kweli afya ya Vengu kwa sasa ipo vizuri, anajitambua. Pia amepewa nyumba, kubwa tu ipo kulekule Kigamboni anakoishi lakini bado hajahamia.”
KUMBUKUMBU
Vengu alianza kuugua kidogokidogo mwaka 2009, lakini Agosti, 2011 hali yake ilikuwa mbaya, akalazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kwenda kumjulia hali.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiaendelea kuuguzwa na familia yake huku taarifa zake zikiwa ngumu kupatikana mpaka hivi karibuni ambapo ndugu mmoja aliamua kuweka wazi hali ilivyo kwa sasa.
Ugonjwa wake mkubwa ulitajwa kushambulia sehemu ya kichwa, hasa kwenye ubongo

KUMBE SHERRY ALIMTAJA MAINDA KABLA SAFARI YAKE YA MWISHO....


MSANII aliyefariki dunia hivi karibuni mjini Morogoro, Sherry Magali, anadaiwa kuwa alikuwa akilitaja jina la Ruth Suka ‘Mainda’ kila mara hadi alipofikwa na umauti.
Marehemu Sherry Magali enzi za uhai wake.
Chanzo chetu makini kilichokuwa karibu na msanii huyo wa filamu, kinasema Sherry alianza kugoma kula akidai hadi amuone msanii mwenzake huyo ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam anakoishi.
Msanii wa 'Bongo Movie' Ruth Suka (Mainda) akiwa katika pozi.
Mpashaji huyo alisema hata siku aliyofariki pia alilitaja jina hilo, kitendo kilichowaumiza sana baadhi ya ndugu na marafiki. Mainda ambaye alikuwa ni rafiki wa marehemu, alikiri kusikia jambo hilo na anasikitika kwamba siku aliyopanga kwenda, ndiyo ambayo mwenzake alifariki.

Warembo wanavyojua kujiachia na Instagram



Instagram ni zaidi ya uionavyo, watu wanajua kula raha asikwambie Mtu jionee mwenyewe...maisha mazuri hadi unashawishika kutaka kujua zaidi wanafanya nini...ntajaribu kuwatafuta hawa watupe siri ya mafanikio yao.

 1. Vera Sidika anapenda clubs yaani mdada yeye ni full ku party. What I like from her she has a talent ni mchoraji balaa anaonekana msomi pia alisema karudi shule big up @queenveebossette naomba tuongee zaidi kuhusu vipaji vyako naamini watu watabaki vinywa wazi.. 

2. Starlisha huyu naye ni mrembo wa instagram yeye anapenda kula sehemu nzuri, kupiga picha akiendesha magari mazuri na selfie za kumwaga. Mungu ni mkubwa kapunguza mabifu, sikuhizi yeye ni mshauri na mhamasishaji wa masuala mbali mbali ya maendeleo, hii inampa heshima safi sana @chaggabarbie naomba nijue siri ya utulivu wako, inapendeza sana. 
3. Huddah kama hayuko airport, hotelini basi swimming pool @huddahthebosschick unapenda kuogelea we mtoto, umekaa kibiashara tu mara photo shoot, lebel yako ya mavazi iko hewan na mengine atleast unaonekana unafanya kazi. Hizo bikini ukiziweka sokoni utauza sana. Hongera 

4. Masogange, picha nyingi yuko kitandani, kama sio kitandani bafuni kama sio nje ya nyumba then anarudi kitandani anajipiga mapicha weee hadi analala. Hongera nawe @officialagnes Mungu kakupendelea sana. 

Kuna wengine humu nashindwa kuwaelezea kwakweli...sitaki kujua sana maisha binafsi ya mtu ila natamani kujifunza au tujifunze kupitia hao "mastaa" Hakuna asiyependa kupiga mapicha all the time kalala, anaogelea, kwenye mahoteli makubwa na maboti anaenjoy maisha kama mnaweza kupiga mapicha hayo jamani tuonesheni na kazi zenu nasi tutamani kufikia huko??..

MASTAA WA BONGO MOVIE WAMPONDA WEMA SEPETU BAADA YA KUNYANG'ANYWA KILA KITU NA MP#NZI WAKE KIGOGO WA SERIKALINI.


MASTAA wa kike Bongo wamecharuka na kutoa yao ya moyoni baada ya nyota mwenzao, Wema Sepetu kubwagwa na aliyekuwa mpenzi wake, anayetambulika kwa jina moja la Clement na kumnyang’anya vitu alivyompa kama zawadi wakati wa mapenzi yao.
Wema Sepetu.
Kuhusu Wema kuporwa ofisi yake ya Endless Fame Film Production, kupewa notisi ya nyumba aliyokuwa amepangiwa na kigogo huyo anayeelezwa yupo serikalini na kunyang’anywa magari siyo stori kabisa mjini.
Risasi Mchanganyiko lilifanya mahojiano na mastaa hao wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu na kuwahoji kuhusu kitendo alichofanyiwa mwenzao ambapo walifunguka bila wasiwasi wowote.
USENGENYAJI
Wakali hao, waliopata kuzungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi wamemponda Wema kwa kutokuwa makini wakati akiwa kwenye uhusiano na kigogo huyo kwa kutaka kukabidhiwa hati za vitu alivyopewa.
Wa kwanza kuzungumza ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye alisema: “Mimi namshukuru Mungu kwa sababu sijapangiwa nyumba na mwanaume.  Naishi maisha yangu simpo ya furaha na amani, sipendi kuigiza maisha. Hao wasanii wanaopenda mambo makubwa wakati hawana uwezo,  nawashauri wafanye kazi, filamu zinalipa sana. Wasipende vitu vya haraka, maana siku zote vizuri huja taratibu.”
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
“Mastaa tusijiachie sana kwa wanaume, kama ukipewa gari, upewe na kadi... tusidanganyike na tusipende kuhongwa, tutafute vya kwetu. Kama mtu anakupenda na anakusaidia kwa mapenzi mema, sawa mheshimu.”
WASTARA JUMA
“Inabidi tujitambue jamani, maana kuna watu wanatembea na mastaa makusudi ili wajulikane au kwa manufaa yao wenyewe. Tuache kuishi kwa kutegemea migongo ya wengine. Wengi hawana mapenzi ya kweli. Hata kama mmeachana, sasa kuna sababu gani ya kumnyang’anya mtu vitu ulivyompa?”
NURU NASSOR ‘NORA’
“Mimi najisikia vibaya sana... kama mtu unajiamini una kipaji, kwa nini usifanye kazi?  Mastaa tuache kujitangaza, kwa sababu tunatumika kama vyombo vya starehe tu.  Tutafute ndoa, tusitumie ustaa kufanya ufuska kwa sababu mali zinapita na mwisho wa siku tunaharibu maisha yetu.”
TAMRINA POSH ‘AMANDA’
“Utapeli ni mwingi, haya mambo ya kupewa vitu siyo vizuri kabisa, tuache.  Wanawake tuna akili fupi sana na tunajisahau tunapokuwa na wanaume wakati wenyewe wana kitu moyoni mwao, akishapata anachotaka anaanza matatizo.



“Bora nitembelee taksi au Bajaj kuliko kudhalilishwa... wanawake ni wajinga na huwa tunajidanganya kwa vitu visivyo vyetu, mwisho wa siku tunaumbuka. Tuache sifa za kijinga.”

FAHAMU KIUNDANI MAFANIKIO YA LADY JAY DEE, MPAKA KUWEZA KUMILIKI GARI LA KIPEKEE BONGO.


Mwaka 2013, vuguvugu la Anaconda lilimsaidia Lady Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Hadi sasa muimbaji huyo ana zaidi ya likes laki mbili kwenye Facebook na followers zaidi ya 60,000 kwenye Twitter.

Jaydee akiwa na gari yake mpya, Range Rover Evoque
Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo, album yake Nothing But The Truth ilifanya vizuri na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya album zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye santurui take hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki aliyekuwa na show nyingi zaidi mwaka jana. Lady Jaydee alitumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako aliiingiza si chini ya shilingi milioni 25.
Mwaka jana pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za album yake kama njugu pamoja na t-shirt za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka jana, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya. Na sasa Lady Jaydee amekuwa msanii wa Tanzania anayemiliki gari aghali zaidi, Range Rover Evoque.
land-rover-range-rover-evoque-1306223771-19
“Hakupenda kudisclose mambo ya bei wala wapi alikoinunua,” mume na meneja wa Lady Jaydee, Gadner G Habash ameiambia Bongo5.
“Lakini tunashukuru Mungu kwa baraka zake na nguvu ya mashabiki wake amefikia hapo. Hiyo ni gari aina ya Range Rover Evoque. Gari hizi mara nyingi hapa Tanzania kuna wakala wake kampuni inaitwa CMC Moters, ni moja kati ya magari latest sana,” amesema Gadner.
jide
Gadner amezitaja sababu za mafanikio ya Jaydee ni pamoja na ‘karama na fadhila ya mwenyezi Mungu, nguvu anayoipata kutoka kw mashabiki wa muziki nchini.

“Wamekuwa wakimwamini, wamekuwa wakimsupport na kwa jinsi hiyo ndio maana amekuwa anapata mafanikio. Sababu ya tatu ni ile commitment yak wake yeye mwenye kama msanii. Jaydee ni mtu ambaye ana bidii sana kwenye kazi yake na anapenda sana muziki. Jambo hili linafanya siku zote awe makini na umakini ule unampelekea awe na mafanikio kusema ukweli. Kitu kingine ni kwamba ni mtu ambaye anathamini kesho yaani kama leo tumefanya vizuri, je kesho itakuaje! Huwa anafikiria sana kutowaangusha mashabiki wa muziki wanaomsupport.”
Gadner amesema pamoja na kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner amefafanua.
Akiongelea ushiriki wa Jaydee kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, Gadner amesema Jide amejiongezea connection kubwa na amejifunza mengi.
“Pamoja na kuestablish mawasiliano lakini kumekuwa na kujifunza kwa malegend kama Salif Keita na zaidi ya hapo kumekuwa na kama aina flani ya miradi ya kufanya kazi pamoja na wasanii waliofika pale. Mzee Salif Keita amemkubalia Jaydee wakati wowote atakapokuwa tayari aende Mali wakafanye wimbo pamoja. Hali kadhalika Octopizzo kutoka Kenya tayari wameweka kwenye line wimbo wa kufanya pamoja na Jaydee na wasanii wengine wa Nigeria akiwemo Waje.
Gadner amesema kwakuwa kufanya kazi na wasanii wa nje kunahitaji maandalizi ya kutosha, muda muafaka ukifika Jaydee ataanza kuifutilia miradi hiyo.
Gadner ambaye ni mtangazaji wa Times FM, ameongeza kuwa kwa mwaka 2014 Lady Jaydee atasikika kwenye kazi alizoshirikishwa ukiwemo wimbo wa Juma Nature, One, Songa na Nikki Mbishi, huku pia yeye akiachia wimbo mpya uliotayarishwa na Bob Junior na kwamba Historia unaopatikana kwenye Nothing But The Truth ni wimbo wa mwisho kutoka kwenye album hiyo.
Amesema video ya Historia imefanywa na kampuni ya Ogopa na kwa sasa ipo kwenye hatua ya editing.


Kuhusu wimbo mpya, Gadner amesema video yake itaongozwa na muongozaji Mtanzania aishiye Marekani, Hefemi.
“Nafikiri Jaydee alikuwa anataka afanye kitu cha tofauti na ndio maana akaamua amchukue director ambaye yuko nje ya Tanzania ili atupe picha na idea tofauti.”

Mmh, Angalia 10 Hot Photos za Super Model Mika Shay



Msichana huyo ambaye ni Model ana Mvuto wa Ndani na nje, ni Mwanamke ambaye binafsi naimani kila mwanaume ana wish awe mke au awe mtu wake angalia hizo Photos halafu uniambie unaonaje. 
Mika Shay eewMika Shay treMika Shay 54Mika Shay r4Mika Shay tttMika Shay 55Mika Shay 5Mika ShayMika Shay
PHOTOSHOW- Model Mika Shay
Model Mika Shay

Nollywood wazidi kutoa picha za Map3nz! Hadharani, Jionee hapa



Miongoni mwa Movies ambazo wahusika wake wamefanya kweli na kwenda mbali zaid ya uigizaji ni hii inayojulikana kwa jina la "Pleasure and Crime" hapa hata Bongo Movies Hawagusi Mziki Huu.
Angalia Video hapa chini:-

WEMA AWATIBUA FANS WAKE NA VIVAZI VYAKE VYA UTATA



BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ameendelea ‘kutibua’ hali ya hewa kwa kukiuka maadili ambapo kwa mara nyingine tena ametupia picha mtandaoni zikimuonesha akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi baadhi ya sehemu nyeti za mwili wake.
Wema Sepetu.
Picha hiyo iliyopo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii inamuonesha Wema akiwa amevaa kiblauzi chenye matundu kiasi cha kuifanya sidiria aliyovaa ionekane huku sehemu nyingine zikiwa wazi.
Wakiizungumzia picha hiyo ambayo Wema anaonekana akiwa na rafiki yake, Kajala Masanja, baadhi ya wadau wamesema msanii huyo anaonekana kujisikia raha sana sehemu zake kuwa wazi.



“Mh! Huyu Wema na hivi vivazi vyake vya nusu utupu hajambo, sijui anajisikiaje kuvaa vile…hata kama atasema ni kutokana na hali ya joto lakini hii sasa imezidi, huko ni kuwatega wanaume,” aliandika mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaidi.


GPL

Wanaume wa Umri sawa nami ni Watoto, Hawaniwezi, Afunguka Msanii wa Movie.


Msanii wa Nolly Wood ambaye ana Mvuto wa Kipekee Kiumbo na Kimapenzi, Uche Jombo,  amesema ya kwamba Yeye si Mungu hivyo hana uwezo wa kuchunga hisia za Mwenza wake ingawa kwa upande wake hakuna nafasi ya usaliti.

Uche aliendelea kufunga alipokuwa akihojiwa na Television Moja kuhusu Movie yake mpya iitwayo
 "Un Conditional" na kusema ya kwamba kamwe hajawahi kutembea na wavulana wadogo kuliko umri wake Pia wanaume wa umri wake anawaona kama watoto, hawana jipya.

Gumzo kuhusu Sakata la Mzee Majuto Kuoa kwa Siri Dar!!!!

-->


Chande Abdallah na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, kuna taarifa kwamba gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ almaarufu mzee Majuto amefunga ndoa ya siri ndani ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Tukio hilo limetokea Julai 8, mwaka huu pande za Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo mzee Majuto alifunga ndoa na msichana mbichi aitwaye Rehema Omary.
Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.
Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.
Muoaji akaongozana na wakwe na mashehe kwenda Msikiti wa Aqswa uliopo jirani ambapo ndoa hiyo ilifungwa kisha wakarudi nyumbani ambako cherekochereko ziliendelea.
Paparazi wetu alifanikiwa kujipenyeza na kuonekana kama mmoja wa ndugu na kushuhudia mzee Majuto akikabidhiwa mkewe.
Baada ya robo saa, mzee Majuto na mkewe walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuingia kwenye gari hilo aina ya Noah.
Paparazi wetu alipojaribu ‘kufotoa’ picha kadhaa, alisababisha kuzuka kwa  kizaazaa kwa wanandugu waliomlazimisha kuzifuta picha hizo ambapo alitii.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu walijaribu kuzungumza na mzee Majuto kwa simu lakini kazi haikuwa nyepesi kwani simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Alilipopigiwa simu mpambe wa bwana harusi, Barafu, alisema hana la kusema na kusisitiza atafutwe mzee Majuto.
Mwandishi wetu alirudi Mbagala kwa mama wa biharusi ambaye alikuwa mkali na kusema kuwa atafutwe mzee Majuto.
Siku hiyohiyo mzee Majuto alipokea simu na kuulizwa kama ni kweli amefunga ndoa na msichana aitwaye Rehema.
Katika hali ya kushangaza, mzee Majuto alicheka sana na kudai kwamba utafiti wake umekakilika. Alipohojiwa ni utafiti gani alisema:
“Nilikuwa nafanya utafiti wa kutaka kuigiza filamu ya ndoa ya siri ndiyo maana nikaenda kule Mbagala lakini sasa nimeamini kwamba hakuna ndoa ya siri,” alisema mzee huyo huku akikwepa kukubali.
Habari zinasema kwamba mzee Majuto anakwepa kukubali kwamba amefunga ndoa kwa kumhofia mkewe wa kwanza ambaye amemuacha jijini Tanga.

Source: GPL

Eniola Auliza Mashabiki kuhusu kuwa Dada yake Rick Ross!!


Yule mwanamke mnene na anayekula kushinda wanawake wa Nigeria, Eniola Badmus ameandika katika page yake ya Instagram ikiwauliza wadau ya kwamba vipi kila mtu anamfananisha na Mwanamuziki kutoka Marekani, Rapper Rick Ross, yawezekana akawa dadake? Angalia picha mwenyewe kisha toa tathmini yako.

Bow Wow Avunja Ukimya, Amla "DENDA" Tyra Banks Live Katika TV Show Interview.



Ikiaminika na Wengi wa Raia kutoka Marekani kuhusu kutamani na jinsi ambavyo wengi wa wanaume wanatamani wapate nafasi ya kuwakumbatia na hasa Kuwabusu Walimbwende Kama Tyra Banks, Juz Mwanamuzi Bow Wow aliukata Mzizi wa Fitina kwa Upande wake kwani ali Wish Kumbusu Super Model huyo na akapewa nafasi hiyo akiwa kama Mgeni mualikwa wakati Tyra Akirusha Kipindi cha BET's 106 & Park Music Video Show.

Bow Wow akamkamata kisawasawa Model huyo na kuanza kujimwaya mwaya nae Huku Kipindi kikiwa kinarushwa Moja kwa Moja Hewani.

Kajala Atimkia South Africa, Wadau Wamohofia na Madawa, Mwenyewe Asema ni kupunguza Stress Tu!!!


Imelda Mtema
MWIGIZAJI Bongo, Kajala Masanja ambaye miezi michache iliyopita alichomoka nyuma ya nondo za Segerea kwa dhamana, ametimkia nchini Afrika Kusini kupunguza mawazo.
Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, Kajala alitupia picha zake mbalimbali katika mtandao wa Instagram zikimuonyesha akiwa nchini humo na kusindikiza na ujumbe wa maandishi uliosomeka kuwa amekwenda kwa ajili ya kubadilisha hali ya hewa kwani toka akumbwe na matatizo, hajapata mtoko wa kupumzisha akili.
“Nimekuja kubadilisha hali ya hewa  maana nimetoka kwenye matatizo, sijapata kabisa muda mzuri wa kuipumzisha akili yangu hivyo nimeona bora nije huku kupumzika kidogo kisha nitarejea nyumbani,” alisema Kajala.

Source: GPL

Muigizaji wa Kike anayelipwa Zaidi Holly Wood.



Kwa mujibu wa tathimini iliyotolewa na Forbes, Angelina Jolie amefikisha kiasi cha $33 Milioni kwa kipindi cha Mwaka Moja kati ya June 2012 na June 2013.

Kupanda huko kwa Jolie kumemshusha Kristen Stewart ambaye alikuwa namba moja, lakini kutokana na Gharama kubwa za Bajeti za Movie zake kama Twilight na Snow White.

Nafasi ya Pili inashikiliwa na Jennifer Lawrence ambaye ana $ 22 Milioni wakati Kristen akishika nafasi ya tatu na $20 Milioni

Justin Bieber Awatemea Mate Mashabiki walikuwa wamejazana kumshangaa!!!


Kweli majuu hapaishiwi vituko, Mkali wa Pop Kijana mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amefanya Kufuru ya aina yake baada ya kuwatemea mate mamia ya mashabiki waliokuwa wamejazana chini katika ghoroma moja alipokuwa amekwenda kwa rafiki zake Alhamis ya Tarehe 25 July. Angalia Picha zaidi Chini..

Agness Masogange Amponza Madee South Africa



Kwenye Exclusive interview na millardayo , Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana (Akina Masogange )  waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.


Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.


Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.


Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.


Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.


Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.

Source: Milard Ayo 
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga