Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

LULU ALITOKA KIVINGINE SIKU YA WAPENDANAO



Mara kadhaa tume kuwa tukiwaona  baadhi ya ndungu zetu ambao Lugha ya malkia inawapiga chenga wamekuwa wakivaa nguo zenye maandishi ambayo huwa hayafai lakini hawa mara nyingi huwa hawajui maana ya kile ambacho kimeandikwa.
Sote tunatambua kuwa watu wenye uelewa kama wa mrembo huyu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hawezi kuvaa ngue yenye maandishi akiwa ajui maana yake au hakubaliani na kile kilichoandikwa. Sasa je mtoto lulu ni kweli  anamaanisha hiki kilichoandikwa hadi kupiga nacho picha na kutupia mtandaoni. Au labda ni dili
amepata la kutangaza kinywaji.
Kama sio,ndio tuseme kweli mrembo huyu anapenda kilaji kiasi kwamba haitaji kupendwa na mtu yoyote?
Hebu tuambie wewe umemuelewaje hapa bidada huyu.

PAMOJA NA KUCHANGIWA KUJENGEWA NYUMBA NA BWANA'KE, MAMA AMKANA MCHUMBA WA LULU.


Kufuatia kauli yake ya hivi karibuni kuwa nyumba anayomiliki ilitokana na mchango wa bwana’ke (hakumtaja jina), mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ameibuka na kumkataa mwanaume huyo.


Mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.
Kwa mujibu wa Lulu, nyumba hiyo iliyopo Kimara jijini Dar ameijenga kwa kusaidiana na bwana’ke kwa mtindo wa pasu kwa pasu (kuchangia nusu kwa nusu).Alisema kuwa anamshukuru Mungu kwani hadi hapo ilipofikia ikiwa inakaribia kumalizika ameijenga kwa nguvu zake na mwanaume wake huyo.

“Yeah! Nimejenga kwa msaada wa mwanaume wangu, tunasaidiana nusu kwa nusu,” alinukuliwa Lulu.
Pamoja na mbwembwe zote hizo za staa huyo kwa jamaa yake huyo, mama mzazi wa Lulu ameliambia Amani kwamba hamtambui mwanaume huyo kwani hajawahi kwenda kujitambulisha kwake pamoja na kwamba kahusika kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.
Alifunguka: “Sijawahi kutambulishwa na Lulu kama ana mchumba.
“Kwa hiyo awe amemsaidia au hajamsaidia, mimi simtambui.
“Ingekuwa Lulu amewahi kumtambulisha kwangu kuwa huyo ndiye mchumba wake hapo sawa lakini hakuna kitu kama hicho.

“Halafu naomba utambue kwamba Lulu hawezi kumtambulisha bwana’ke au boy friend wake kwangu, siyo heshima labda awe mchumba. Hapo kidogo afadhali lakini mtu tu mtu, hakuna kitu kama hicho.
Kabla ya Lulu kueleza ukweli juu ya ujenzi wa nyumba hiyo, awali kulikuwa na madai kwamba alihongwa na mheshimiwa mmoja (jina tunalo) huku wote wakikanusha kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo, kitendo cha Lulu kumiliki mjengo huo kimempa heshima kubwa tofauti na mastaa wenzake wa kike ambao wamekuwa wakiishia kupangiwa nyumba na kuhongwa magari yasiyo na kadi kisha kunyang’anywa na kurudia maisha ya kawaida uswahilini.




LULU HATUMII NGUVU KATIKA MAPENZ ILI AJIANDAE NA LEBA



MASTAA wana mambo! Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kwenye mapenzi kwa sababu yanapoteza muda bila sababu za msingi bora nguvu zake azitunze hadi pale atakapokuwa akijifungua.
Mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Akimwaga cheche mbele ya mwanahabari wetu, Lulu alisema siku hizi wanaume wengi wanawafanya wasichana watumie nguvu kutetea penzi kutokana na migogoro isiyokuwa na msingi.
“Bora nguvu zangu nizihifadhi za kuendea leba kuliko kuzipoteza katika mapenzi kwani hayo mambo yamepitwa na wakati kabisa,” alisema Lulu.

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga