Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

BAADA KUKOSA MUME, MISS DODOMA AAMUA KUOKOKA


Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans amemrudia Mungu kwa maana ya kuokoka kwa kile alichodai kutotimia kwa malengo aliyojiwekea.Akizungumza na mwanahabari wetu, Eva alisema tangu akiwa mdogo, alijiwekea kiapo kuwa endapo atashindwa kumpata mume mwema, basi atafanya kazi ya kumtumikia Mungu.
Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans akiwa kanisani.
“Nakumbuka mapito yangu yote tangu nikiwa mdogo mpaka nikaingia kwenye masuala ya urembo nilijiwekea nadhiri ikifika muda mambo yangu hayajakamilika, itanibidi nimrudie Mungu wangu.
“Baada ya kupitia urembo nilichumbiwa, hapohapo nikaanza kuhudhuria mikutano mbalimbali ya neno la Mungu, siku moja Nabii akitoa neno, nilimsikia akisema kuna binti mmoja hapa anataka kuolewa apite mbele haraka sana, basi nikapita mbele na nilipofika pale alianza kuniombea na baadaye alianza kuniuliza maswali.
“Akaniambia mwanaume anayetaka kunioa hana sifa za kuwa mume bora na kama nabisha nimchunguze, basi nikamchunguza na kugundua kuwa hakuwa na sifa.“Basi nilivyojua tu nikaamua nisitishe mipango ya ndoa zikiwa zimesalia wiki mbili tu ili ndoa ifungwe, nashukuru Mungu nilieleweka, na kuanzia hapo nikaamua kuokoka kabisa, ninaomba sana Mwenyezi Mungu aniletee mume mwema,” alisema mrembo huyo.
Eva alifunguka kuwa katika mashindano ya urembo kuna uchafu mwingi hivyo akawashauri wasichana walioko huko kumrudia Mungu.

HALI BADO TETE KWA ALIYEKUWA MISS TANZANIA 2014


 Hatima ya kashfa ya kudanganya umri inayomkabili aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2014, Sitti Mtemvu bado ipo kizani baada ya polisi kuikana kauli ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).
Rita, kwa upande wao ilieleza wiki moja iliyopita kuwa imekabidhi polisi vielelezo kuhusu uchunguzi wa kashfa hiyo kwa lengo la kuchukua hatua.
Jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikana kupokea taarifa za vielelezo hivyo vilivyotumiwa kuombea cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu.
Wiki mbili zilizopita, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ilijivua lawama katika kashfa hiyo na kuiachia Rita.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kova alisema, “Jeshi la Polisi halijapokea vielelezo vyovyote kutoka Rita, wamepeleka wapi? Iwapo waliviwasilisha katika kituo chochote cha polisi watoe taarifa iliyo sahihi, iwapo vielelezo hivyo vitatufikia tutachukua hatua stahiki,” alisema Kova.
Kwa upande wao, Rita waliahidi kuwasilisha vielelezo hivyo wiki hii na kwamba vilicheleweshwa kutokana na kukamilisha upekuzi wa taarifa za kuombea cheti pamoja na cheti cha awali kilichokuwa kikitumiwa na Sitti Mtemvu.
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Rita, Emmy Harrison alisema jana kuwa idara yake imekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na vielelezo hivyo vitakabidhiwa rasmi polisi.
“Haya ni masuala ya kisheria, hivyo sisi tumeshakamilisha kile tulichotakiwa kukifanya na mchakato huu bado unaendelea, tupo katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kuripoti polisi, wiki hii vielelezo vya Sitti vitapelekwa kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Harrison.

MISS TANZANIA KUTOPOKONYWA ZAWADI BAADA YA KUJIVUA TAJI

Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga amesema miongoni mwa maswali aliyokutana nayo kwa wingi jana kwenye ‘Kikaangoni’ ya EATV, ni pamoja na swala la Sitti Mtemvu kama atanyang’anywa zawadi alizopewa ili akabidhiwe aliyevishwa taji hilo baada ya yeye kujivua.“Kwanza hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania mtu kujivua taji, na kwenye kanuni zetu haikuelezwa wazi wazi kwamba mtu akivua taji tunachukua zawadi tunamkabidhi mtu mwingine ama hivyo,” Lundenga ameiambia E-Newz ya EATV.Lundenga amesema kuwa Sitti hatanyang’anywa zawadi kwasababu hakuvuliwa taji bali alijivua mwenyewe.

“lakini bado tuna majadiliano na wadau wetu masponsors tuangalie namna ya kufanya, kama kuna zawadi zimebaki atapewa lakini zawadi ambazo amepewa nafikiri hataweza kurudisha kwasababu hakuvuliwa, kama tungemvua kwa makosa angeweza kurudisha lakini hatujamvua kajivua mwenyewe”.

Zawadi iliyotolewa mwaka huu kwa mshindi wa Miss Tanzania 2014 ni shilingi milioni 18

LUNDENGA AKANA MAPENZ NA SITTI MTEMVU





Mkurugenzi wa Lino Agency akichat Live na mashabiki wa EATV kupitia ukurasa wa facebook wa EATV

Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mahusiano ya kimapenz na aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu.Lundenga amefunguka hayo leo alipokuwa akichata Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana mpka saa nane mchana.

Mbali na mahusiano Watu wengi walitaka kujua ni sifa zipi zilizompelekea mrembo Sitti Mtevu kutwaa taji hilo kama si upendeleo kutoka katika kamati na crew inayohusika kuandaa mashindano hayo kwani watu wengi wamekuwa wakisema kuwa mrembo huyo alikuwa hastahili kushinda taji hilo ukilinganisha na warembo wengine ambao walikuwa wakichuana nae,kufuatia hali Ludenga ikabidi aweke wazi sifa tano amabzo zinamfanya mtu kushinda taji la Miss Tanzania kuwa ni lazima awe na sura nzuri, umbo zuri, mvuto, haiba, ufahamu wa kutosha wa mambo mbali mbali.

SITI HANA SIFA YA KUWA MISS TEMEKE


Kutokana na maamuzi ambayo Sitti Mtevu aliamua kujivua taji la Miss Tanzania 2014 hivyo mrembo huyo amejifutia sifa zake zote alizopata katika kusaka taji la Miss Tanzania hivyo si Miss Chang'ombe wala si Miss Temeke tena.

Hashim Lundenga amesema kuwa kitendo cha Sitti kujivua taji hivyo automaticaly amevua mataji yake yote aliyopata katika ngazi ya wilaya mkoa na hata Taifa kama ambavyo ilivyotangazwa.

"Hashim Lundenga: Automatimacally anakuwa amejivua na mataji mengine pia...."

Kufuatia sakata la Mrembo Sitti Mtevu kudanganya UMMA juu ya umri wake na kumgharimu kulivua taji hilo la Miss Tanzania 2014.Ludenga amesema kuwa hali ya udanganyifu wa umri wa warembo hao huwa ni suala la kawaida na lipo kila mwaka ila kwa kuwa huwa wako makini ndiyo maana wangundua hivyo haoni sababu ya yeye na kampuni yake kuwajibika kisa Sitti Mtevu alidanganya umri.

"Hashim Lundenga: sio sahihi, tupo makini na ndio maana tumegundua, fahamu ya kwamba kila mwaka washiriki wengi tu hutudanganya kuhusu umri wao na ndio maana tupo makini...... tuwajibike kwa kosa gani?????"

NIPO TAYARI KUKABIDHI KIJITI KWA MWINGINE


Kufuatia kuzuka kwa kashfa mbalimbali zinazohushisha mashindano ya Miss Tanzania na waandaaji wake mashabiki wa Eatv walitaka kujua kama Mkurugenzi huyo wa Lino Agency Hashim Lundenga yupo tayari kuachia nafasi hiyo ili watu wengine waweze kuendeleza pale wao walipohishia lakini Ludenga aliweka wazi kuwa yeye kama Mkurugenzi yupo tayari kuchagua mtu mwingine ili asimamie nafasi yake lakini si kuwaachia watu wengine kuendesha shindano hilo.

"Hashim Lundenga :Lino International Agency ni Kampuni ya mtu binafsi na inayo Directors wake, hivyo tunaweza kuteua Mkurugenzi mwingine wa kufanya kazi hiyo........"

MISS TANZANIA HAIWEZI KUFUTWA


Kutokana na baadhi ya watu kutooana umuhimu wa uwepo wa mashindano ya Miss Tanzania na kuyahusisha na kumomonyoka kwa maadili hususani kwa warembo wa Tanzania watu wamependekeza mashindano hayo yafutwe kwani yamekuwa hayana tija na hayana haki kwani kumekuwa na upendeleo na udanganyifu na vitendo vya rushwa ambavyo hupelekea wasichana wengi kuvunja utu wao kwa sababu ya kutaka kushinda au kufikia hatua fulani katika mashindano hayo.

"Hashim Lundenga:Sitty bado ni msichana mrembo na ataendelea kuwa mrembo....haya mashindano hayawezi kufutwa kwa sababu wananchi wanaelewa faida zake, wewe usiyejua faida zake, baki hivyo hivyo..."

MISS TANZANIA HAKUNA FAIDA YOYOTE


Hashim Lundenga ameweka wazi kuwa katika mashindano hayo hakuna faida yoyote anayopata zaidi ya yeye mwenyewe kufahamika na kutembea nchi nyingi duniani,watu walitaka kujua kwanini miaka yoye amekuwa aking'ang'ana yeye tu katika kuandaa na kusimamia mashindano hayo na je anafanya kwa masilahi ya nani na hayo ndiyo yalikuwa majibu ya Lundenga

"Hashim Lundenga hakuna faida yeyote, zaidi ya kufahamika, kutembea nchi nyingi duniani, n.k."

KASHFA YA NGONO KWANGU FITINA TU


Hashim Lundenga amekana leo wakati akichat Live na mashabiki wa ukurawa wa EATV kuwa hana kashfa ya kuomba ngono au kuwa lazimisha warembo hao kutoka na yeye kingono ili waweze kushinda au kushiriki mashindano hayo,Ludenga anasema hizo ni fitina tu za watu fulani wenye lengo la kumchafua na kuchafua mashindano hayo.

"Hashim Lundenga hakuna kashfa kama hiyo..........hiyo ni fitna.............."

Lakini pia Lundenga aliwaambia watanzania kuwa kutokana na Sitti kujivua taji na kumpa nafasi mshindi wa pili kuchukua taji hilo hivyo wasitegemee tena sherehe za kumkabidhi taji hilo Miss Tanzania namba mbili kwani shehere watafanya wazazi wake pamoja na wakala wake wa mkoa alipotokea

"Hashim Lundenga hakuna sherehe yeyote, sherehe huandaliwa na wazazi wake na wakala wake wa mkoa alipotokea"

Hashim Lundenga alimaliza kwa kusema kuwa tunaoomba radhi sana kwa wale wote ambao hatukuweza kujibu maswali yenu yote kutoka na ufinyu wa mud

MISS TANZANIA MPYA NAYE UTATA MTUPU



MISS Tanzania mpya wa 2014, Lilian Kamazima, amesema alihisi ushindi tangu alipoingia katika mashindano hayo, lakini alipokosa taji hakuhuzunika bali alikubali matokeo.
Lakini zengwe jipya limeibuliwa jana na kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Lilian aliyepewa taji hilo baada ya Sitti Mtemvu ambaye ni mshindi wa awali kujivua taji kutokana tuhuma za kudanganya umri, si raia wa Tanzania bali ni Mnyarwanda.
Hashim Lundenga ambaye ni Mkurugenzu wa Miss Tanzania, amekanusha vilivyo na kusisitiza kuwa ni uzushi kwa sababu wao wanaangalia vyeti vya kuzaliwa ambavyo vinaonyesha uraia wa mshiriki.
Hayo yameibuka siku mbili tangu Lilian kukabidhiwa taji la Miss Tanzania 2014, lililokuwa likishikiliwa na Sitti Mtemvu aliyeamua kulivua baada ya kukumbwa na kashfa mbalimbali tangu kutawazwa kwake Oktoba 11.
Lilian ambaye awali alikamata nafasi ya pili, alisema: “Sikuwa na kinyongo ukizingatia urembo ni mambo mengi si sura, ngozi, mwonekano pekee bali unajumuisha mambo mengi, ndiyo maana kipindi cha usahili huwa kirefu. Binafsi niliamini kwamba (Sitti) alistahili hasa kutokana na kuwa na vigezo vingi vinavyoonekana kwa macho hata tulipokuwa kambini, nilikubali matokeo,” alisema Lilian.
Lilian alisema kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa matokeo Oktoba 11, anaamini kilikuwa kigumu kwa Sitti, pia kwake hasa ukizingatia tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili mrembo huyo aliyetokea katika Kanda ya Temeke.
“Nina maono ya mbali na ninatamani miaka mitano ijayo niione Tanzania iliyokua hasa katika nyanja ya elimu, napenda kuona namba ya wanafunzi wanaofaulu ikiwa sawa vijijini na mijini ili kuwa na taifa lenye watu werevu na wenye maendeleo, hivyo nitajitahidi kutumia nafasi yangu kusongesha gurudumu hili,” alisema.
Mrembo huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda kwa shughuli za masuala ya mitindo, alisema anafurahia kupata nafasi hiyo na anawaahidi Watanzania kuwa atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuhakikisha anatimiza malengo ya waandaaji wa mashindano hayo. Lilian Kamazima ana miaka 18, alishiriki akitokea Mkoa wa Arusha.


HATIMAYE SITTI MTEMVU AJIVUA TAJI LA MISS TANZANIA 2014



Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, baada ya kuandamwa na skendo za muda mrefu kutokana na ushindi wa utata wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amejivua taji hilo leo, mshindi wa pili, Lillian Kamazima amrithi, Lundenga athibitisha.

SITTI MTEMVU ATOWEKA KIAINA MJINI



WAKATI suala la kudaiwa kudanganya umri likiwa bado ‘bichii’, taarifa zinadai kuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ametoweka na hajulikani alipo, Risasi Mchanganyiko limechimbua stori kamili.
Mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Shughuli ya kumsaka mrembo huyo ili kujua undani wa sakata lake ilianzia Temeke ambako ilielezwa kuwa ndiko anakoishi.
Mapaparazi wetu walipofika katika nyumba waliyoelekezwa, walikuta imebadilishwa na kuwa Ofisi ya Vikoba ambapo mmoja wa wahudumu wa ofisi hiyo kwa sharti la kutoanika jina lake gazetini, aliwataka waandishi wetu kwenda Mbezi-Makonde akidai ndiko anakoishi kwa sasa.
“Hapa ilikuwa nyumba ya zamani lakini kwa sasa ni ofisi na Sitti hakai hapa, kama mnamtaka nendeni Mbezi-Makonde huko nasikia ndiko anakoishi,” alisema mtumishi huyo.
Mapaparazi wetu hawakuchoka, walifunga safari hadi Mbezi-Makonde ambapo walikuta nyumba yenye maduka yaliyoandikwa Mtemvu Foundation, wakaenda moja kwa moja katika saluni mojawapo iliyokuwa na bango lililosomeka Malisa huku likiwa na picha ya Sitti sambamba na namba za simu.
Sitti Mtemvu wakati wa kutwaa taji la Miss Tanzania 2014.
Dada mmoja aliyeonekana kufanana na Sitti alizidi kutibua hali ya hewa baada ya kusema Sitti amesafiri nje ya nchi pasipo kufafanua nchi gani.“Sitti amesafiri nje ya nchi, ila kama mnamtaka nafikiri nitawapa namba zake akirudi kati ya Jumatatu au Jumatano ya wiki ijayo (wiki hii),” alisema dada huyo pasipo kutaja jina lake.
Mmoja wa majirani wa mrembo huyo alihoji inawezekanaje mrembo huyo akasafiri nje ya nchi wakati suala lake la umri halijapata ufumbuzi?“Mh! Ataondokaje wakati bado ana majanga ya umri?” alihoji jirani huyo.
Aidha, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia hapo, Jumapili iliyopita walitia timu Buza Kipera katika Kanisa la The Revelation Church la Nabii Yaspi Bendera ambalo ilielezwa kuwa Sitti anaabudu, ili kujiridhisha kama yupo, lakini pia hakuonekana huku waumini wakidai hawajamuona kwa siku za karibuni.Nabii Yaspi Bendera wa Kanisa la The Revelation Church.
“Hatumuoni siku hizi, ila alikuwa anakuja katika ibada ya peke yake kwa nabii saa kumi lakini siku za karibuni hatumuoni,” alisema muumini mmoja.Katika ibada inayoendeshwa kanisani hapo ambayo mapaparazi wetu walizama ‘kiintelijensia’, Nabii Yaspi alisikika akimkingia kifua Sitti kuwa alistahili ushindi na kumtabiria kufika mbali na hata kuwa Miss World huku akiwaonya wanaomfuatilia mrembo huyo.
“Mara ya kwanza nilimtabiria Sitti kushinda u-miss Tanzania na kweli akashinda, sasa wanatokea watu wakidai mara ana hipsi kubwa, ooh kadanganya umri, huu wote ni upepo tu na utapita.“Kama Sitti hatakengeuka kwenye imani yake atafika mbali zaidi na kushinda hata Miss World. Wale wote watakaoendelea kumfuatilia wataparalaizi,” alisema Nabii Yaspi.
Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), walisema bado wanalifanyia uchunguzi suala la Ritta kudaiwa kufoji cheti cha kuzaliwa kutokana na baadhi ya nyaraka zake kuonesha amezaliwa mwaka 1989 huku yeye akidai amezaliwa 1991.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akitafakari jambo.
Wakati RITA na BASATA wakiwa hawajatoa tamko lolote kufuatia uchunguzi waliodai wataufanya, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara ili azungumzie sakata hilo.
“Waziri ni mtu mkubwa sana kuzungumzia suala kama hilo, watafute wasaidizi wangu pale wizarani watakuambia kinachoendelea. Naweza kutoa tamko halafu nikaonekana mtu wa ajabu, kumbe watu wanaendelea kulifanyia kazi, nenda kamuone Mkurugenzi wa Utamaduni atakusaidia,” alisema Waziri huyo alipozungumza nasi kwa njia ya simu.

UTATA WA UMRI WA MISS TANZANIA NA MADUDU YA RITA.


Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), bila shaka mko vizuri mnaendelea kusimamia jukumu zito katika taifa letu.Usajili, Ufilisi na Udhamini siyo kazi ndogo. Ni kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu maana matokeo ya ufanisi wenu ndiyo majibu ya shughuli nyingi katika nchi.
Watu wakitaka kusafiri, kutambulika katika maeneo mbalimbali nyinyi lazima mhusike kutatua.
Mkitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea na majukumu yangu kama kawaida.  Nimewakumbuka leo kupitia barua hii ili niweze kuwafikishia yaliyoko katika akili yangu ndogo.
Madhumuni ya barua hii kwanza kabisa ni kutaka kuwauliza, hivi mmewahi kuwaza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa watu kufanya madudu ya kufoji vyeti kama anavyodaiwa kufanya mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu?Kwa kuanzia eneo hilo, ni vyema basi chombo chenu kikafanya tathmini upya katika kuhakiki taarifa mbalimbali na kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti mtu kufanya udanganyifu wa aina yoyote.
Msisubiri hadi yatokee ya kutokea ndiyo muanze kuchukua hatua.
Kupitia suala la Sitti ni dhahiri inaonesha kuna walakini kwenye ofisi yenu. Haiwezekani nyaraka nyingine za mtu huyohuyo mmoja zioneshe kwamba amezaliwa mwaka 1989 huku mwenyewe akidai kuwa amezaliwa mwaka 1991.
Kinachonisikitisha zaidi mhusika anadai eti cheti chake cha kuzaliwa kilipotea na akadai kuwa mmempatia kingine kipya Septemba 9, mwaka huu.Alipoulizwa kwamba alitoa taarifa katika kituo gani cha polisi juu ya upotevu wa cheti chake hakuwa na jibu la kueleweka, mlimpaje?
Wakati umri wa mrembo huyo ukiendelea kuwa gumzo kwa takriban mwezi mzima, RITA mliendelea kuziba mdomo katika kung’amua umri halisi wa binti huyo licha ya wadau mbalimbali kuhoji juu ya hilo. Mtendaji Mkuu wa RITA, Jumamosi iliyopita alikaririwa katika chombo cha habari akisema bado wanaendelea kumchunguza miss huyo. Hadi lini?
Labda sina uzoefu juu ya mambo ya uchunguzi lakini kweli mfumo mlionao si rafiki kiasi cha suala hilo kuchunguzwa kwa zaidi ya wiki tatu? Nafikiri kuna haja ya kwenda mbele zaidi ya hapo. Dunia ya leo kila kitu kinakwenda katika mfumo ‘data base’ kwenye kompyuta.
Kwa nchi za wenzetu ni rahisi tu mtu kupata taarifa zake, tena hakuna kificho ndiyo maana utata wa Sitti ulipokuwa ukiendelea, watu ‘wali-google’ tu na kupata taarifa zote za Sitti kule Texas, Marekani na kila kitu kikawekwa hadharani. Kuanzia leseni ya udereva hadi hati ya kusafiria.
Ni wakati sasa umefika tubadilike, tutengeneze mfumo wa kuweka wazi data. Isichukue muda mrefu kubaini taarifa za mtu hususan katika suala la utaifa kama la Miss Tanzania ambaye anatakiwa akaiwakilishe nchi katika mashindano ya urembo ya dunia.

MOTO WAMUWAKIA MISS TANZANIA 2014



WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu, taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo.
FikraPevu imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ambaye ni baba yake.
Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.
FikraPevu imefahamishwa kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18.
Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho.
Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko, ameiambia FikraPevu leo Alhamisi Oktoba 31, 2014 kwamba kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wa kina kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa.
Unaweza soma  
Baada ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa chini ya kiapo.

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga