Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

JOYCE KIRIA AKWAA DENI LA MIL 500 BAADA YA KUTOA SIRI YA MBUNGE WA ZANZIBAR


Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.

Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi

KIFO CHA MAMA NTILIE CHASABABISHA VURUGU IRINGA, KITUO CHA POLISI CHACHOMWA MOTO.




Habari kutoka Iringa zinasema kuwa kituo cha polisi cha Ilula mkoani Iringa kimechomwa moto na wananchi wenye hasira kufuatia polisi kumuua mwanamke mmoja mfanyabiashara ya mama ntilie wakati wa msako maalum ulioendeshwa na jeshi la polisi dhidi ya wafanyabiashara na watu wanaokunywa pombe mida ya kazi.
Inasemekana wakati wa purukushani za kukimbia ndipo polisi mmoja alimchota mtama huyo mama wakati anakimbia na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki dunia hapo hapo.
 
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.

 
Muonekano wa mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya mji huo.


 
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.
 
 
 
 



MKUU WA KITUO CHA POLISI JELA MIAKA 30 KWA UBAKAJI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

MWALIMU MBARONI KWA KUMTUMIKISHA BINTI WA MIAKA 12KUMUUZIA MAYAI NA SOSEJI


MATUKIO ya mateso, unyanyasaji na utumwa kwa watoto yanashika kasi nchini! Safari hii mwalimu wa shule moja ya msingi iliyopo Mburahati jijini Dar aliyetajwa kwa jina moja la Lucy ametia aibu baada ya kutiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar akituhumiwa kumtumikisha mtoto mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Sakina kwa kumuuzisha mayai ya kuchemsha na soseji.

Mwalimu huyo akijitetea juu ya sakata hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilichukua nafasi maeneo ya Kashuda Bar, Magomeni hivi karibuni baada ya wakazi wa eneo hilo kuhamaki kumuona binti huyo akitembeza mayai na soseji mtaani wakati umri wake ni mdogo kinyume na sheria za ajira.
RAIA WAMZUNGUKA
Ilisemekana kwamba, baada ya kukerwa na kitendo hicho huku Sakina akionekana hana furaha, raia hao wenye hasira kali walimhoji ambapo alimtaja mwalimu huyo kuwa ndiye bosi wake aliyemchukua kutoka Tanga kwa ajili ya kufanya kazi za ndani (hausigeli).
AFUATWA SHULENI
Ilidaiwa kwamba, wakifuatana na mtoto huyo, wakazi hao walifunga safari hadi shuleni kwa mwalimu huyo Mburahati ambapo wanahabari wetu walitonywa na kutia timu hadi kwa mkuu wa shule hiyo, Kibassa ambaye alikiri kuchukizwa na kitendo cha mfanyakazi wake kumwajiri mtoto wa miaka 12 kumtumikisha kazi akiwa ni mwajiri wa serikali.
Mwananfunzi Sakina anayedaiwa kuuzishwa mayai muda wa shule.
“Kimsingi nimesikitishwa kwa sababu Lucy ni mwajiriwa wa serikali, hapaswi kufanya jambo baya kama hili. Kwa umri wake alipaswa awe darasani,” alisema Kibassa.
MWALIMU AJITETEA
Kwa upande wake, Lucy alijitetea kuwa binti huyo aliletewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Kizito aliyemuagiza mfanyakazi wa ndani, lakini baada ya kufika binti huyo alimkataa na kudai bado mdogo asingeweza kufanya kazi za ndani.
Mwalimu huyo alisema alikuwa akimsubiri binti mwingine mkubwa aletewe na Kizito ili amrudishe Sakina kwao na kudai kuwa hata biashara ya mayai hakumtuma yeye bali alimtuma John (kijana wake wa kazi) ila inawezekana Sakina alijiingiza kujisaidia na ugumu wa maisha.

Mwalimu huyo akiwekwa kikao.
BINTI ASIMULIA
Akiwa shuleni hapo, mbele ya bosi wake, Sakina alifunguka kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo na kufanya kazi za ndani kwa Lucy huku akisimulia kunusurika kubakwa na kupitia mateso mengine kama kunyimwa chakula na kulazimika kutembeza mayai na soseji mchana kutwa.
“Nafanya kazi za ndani na kutembeza mayai, kuna kaka mmoja nilimwomba msaada ili nirudi nyumbani, akanilazimisha tufanye map3nzi ndipo anisaidie, nilipokataa akaniacha,” alisema Sakina.
Hata hivyo, mwalimu huyo alitolewa shuleni hapo chini ya ulinzi mkali kisha kufikishwa Polisi Magomeni katika dawati la jinsia kwa hatua zaidi.

VITA YA U-FIRST LADY IMEANZA, MITANDAO YA KIJAMII YATUMIKA KATIKA KAMPENI


TAYARI imebainika kwamba, baadhi ya viongozi walioonesha nia ya kugombea urais mwaka huu wameanza kupigiwa debe na wake zao ndani ya mitandao ya kijamii ili waume hao watakapoibuka na ushindi wapate nafasi ya ‘u–First Lady’, Risasi Jumamosi linakupa zaidi!
Mama Salma Kikwete.
Taarifa zilizotua juu ya dawati la gazeti hili juzi zilisema kuwa, vita ni nzito kwani baadhi ya wake wa wagombea nao wapo ndani ya mkakati wa kukusanya watu wa kuwaunga mkono waume zao katika kinyang’anyiro hicho kitakachochukua nafasi Oktoba, mwaka huu.
Wakati vita hiyo ikiwa imepamba moto, mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan Hussein naye ameibuka kwenye Risasi Jumamosi na kuanika utabiri mzito juu ya wasifu wa mtu atakayeshinda urais huo.
HALI ILIVYO SASA
Habari zinadai kuwa, baadhi ya wake wa viongozi hao nao wamekuwa wakipita chini kwa chini kukusanya na kuweka sawa makundi ya kisiasa tayari kwa kampeni za kuwaingiza ikulu waume zao.
ISHU NI KUMRITHI MAMA SALAMA KIKWETE
“Kila mke wa mgombea anafanya kampeni za chini kwa chini. Unajua wenyewe kila mmoja anafahamu kwamba ‘mzee’ akiingia ikulu yeye atakuwa First Lady kumrithi wa sasa (mama Salma Kikwete), ndiyo maana siku hizi karibu wake wa wagombea wote wana safari za mikoani kupanga timu ushindi,” kilisema chanzo kimoja.

Mke wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.
FARAJA KOTA YUKO WAZI ZAIDI
Miss Tanzania 2004, Faraja Kota ambaye ni mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyetangaza nia, amekuwa akitupia maneno yenye kumpigia kampeni mumewe huyo kwenye Instagram na mitandao mingine ya kijamii.
KWENDA NAYE KANISANI
Desemba mwaka jana, Faraja aliongozana na mumewe huyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwenda kwenye Kanisa la FPCT, Ilongelo na baadaye kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, Singida ambako mumewe alitangaza rasmi nia yake ya kugombea urais.
MAMA PINDA
Tunu Pinda ni mke wa Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda. Yeye aliwahi kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema alishtushwa kusikia habari kwamba, mumewe ametangaza nia ya kugombea urais 2015.
Mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Alisema alipomuuliza mumewe alimwambia hajaita vyombo vya habari kusema hivyo lakini muda ukifika atafanya hivyo. Mama Tunu akasema na yeye anakubaliana na maneno ya mumewe kwamba muda ukifika atangaze kugombea urais.“Kwa hiyo kama alivyosema na iwe hivyo kama Bwana Mungu aishivyo, nasema amina. Kwa sababu muda bado haujafika, utakapofika tutajua,” alisema mama Pinda.
YA MTABIRI SASA
Kuhusu utabiri wa Maalim Hassan, amesema mwaka huu, Tanzania itampata rais wa aina yake kuliko miaka yote iliyopita tangu uhuru (Desemba 9,1961).Akizungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita, ofisini kwake, Magomeni, Dar, Maalim Hassan alisema kuwa, rais atakayepatikana mwaka huu atakuwa mtu aliyechanganya dini.
Alisema mtu huyo, kama baba yake atakuwa Muislam basi mama atakuwa Mkristo. Kama mama Muislam, baba itakuwa kinyume cha hapo.
Mke waNaibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Yusuf Makamba.
TOFAUTI HATA KWA MKE, MUME
Maalim Hassan akaenda mbele zaidi kwa kusema: “Kama wazazi wake wote watakuwa dini moja, basi yeye (mgombea) atakuwa na imani tofauti na mke wake au mume wake (kama kutakuwa na mgombea mwanamke). “Mgombea anaweza kuwa Muislam, kama ni mwanaume basi mke wake atakuwa Muislam. Vivyo hivyo kwa mgombea mwanamke,” alisema Maalim Hassan.
KWA HARAKAHARAKA
Kauli ya Maalim Hassan ina ishara ya kumgusa moja kwa moja, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Yusuf Makamba ambaye mama yake mzazi ni Mkristo huku baba yake, mzee Yusuf Makamba akiamini katika Uislam.
WANAOTAJWA KUWANIA URAIS MWAKA HUU
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitangaza nia hiyo usiku Agosti 22, mwaka jana Ikulu Ndogo ya Jiji la Mwanza.

Margreth Sita.
January Makamba alitangaza nia ya kuwania nafasi hiyo Julai 2, mwaka jana alipokuwa Uingereza katika mkutano wa sekta ya mawasiliano. Wengine ni Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Andrea Kigwangallah, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba (CCM), Waziri Nyalandu (CCM), Mawaziri Wakuu Wastaafu, Frederick Tuluwai Sumaye na Edward Ngoyai Lowassa (wote CCM).
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camillus Membe (CCM), Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Masatu Wassira na Mbunge wa Sengerema, William Mganga Ngeleja (CCM). Waziri wa Uchukuzi, Samuel John Sitta naye amekuwa akitajwa kujitosa kwenye kijiti cha urais.
Kutoka vyama vya upinzani, ambaye ameshatangazwa na chama chake ni Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba. Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Peter Slaa yeye amekuwa akigombea kwa chama hicho kwa miaka kumi iliyopita. Lakini kuna tetesi kuwa, huenda Chadema ikamsimisha mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Haikaeli Mbowe.

DALALI WA KUWAUZA NA KUWAUA ALBINO APATA STAHIKI YAKE, AUAWA KIKATILI NA WANANCHI.


Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba, kata ya Kazunzu, wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya Bulyaheke, wamempiga kwa marungu, mawe na mapanga na kisha kumchoma moto mtu ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu kuwa wakala wa kuteka watoto wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana na waganga wa kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri.
Mbali ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto nyumba 13 zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao.
Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Richard Mangalamu baba wa mwanafunzi aliyetekwa, Winfrida (11) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Kazunzu, alisema mtuhumiwa alimwachia mwanafunzi huyo kutokana na kumkuta ana chale mgongoni na kifuani akidai amepoteza ubora.


Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Enock Mabula, kwa nyakati tofauti walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Naye Diwani wa Bulyaheke, Bagadi Nyuki, akiwa eneo la tukio, alisema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kudaiwa kuwa juzi alimteka mwanafunzi wa kike anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kazunzu na kumvutia vichakani na kisha kumvua nguo na kumpapasa.


Inadaiwa kuwa alimuachia huru baada ya kugundua kuwa hakuwa na sifa zinazohitajika na mganga na mwanafunzi huyo alipofika nyumbani aliwaeleza wazazi wake na ndipo wakishirikiana na wanakijiji wenzao walianza kumsaka mtuhumiwa na kufanikiwa kumtambua.


Inadaiwa baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo alikiri na kujitambulisha alikuwa ametoka kijiji cha Katoro, mkoani Geita na alikwenda Sengerema kwa kazi ya uwakala wa kuteka watoto.


Diwani huyo alisema marehemu aliomba apelekwe kijiji jirani cha Bulyaheke umbali wa kilometa sita kutoka Kazunzu kwa mwenyeji wake na mdau mwenzake, Sato, lakini wapofika walikuta amekwisha kutoroka.


Wakati huohuo, mwili wa mtoto Yohana Bahati aliyeuawa kwa kukatwa miguu na mikono, mwili wake utazikwa kesho katika kijiji cha Kataro, mkoani Geita.
CHANZO NIPASHE

BREAKING NEWS :MEZ B AFARIKI DUNIA


Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kurudishwa nyumbani na mama yake amefariki Dunia. Mez B alikuwa akiuguliwa na homa ya mapafu [Pneumonia] na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa siku ya tatu toka anatumia dawa hizo. 



Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe drip ila hali yake ikawa mbaya zaidi, wakati wanampeleka hospitalini alifia walipofika mapokezi. Jirana amelezea haya. 

Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen

HALI YA KIKONGWE ALICHAPWA AKIHUSISHWA NA USHIRIKINA BADO NI MBAYA


KIKONGWE Hilda Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Kikongwe akiwa hoi baada ya kupigwa mawe kutokana na imani za kishirikina.
Kikongwe huyo na Maurus Zenda (46) anayedaiwa kuwa ni mwanaye kiukoo, kwa pamoja walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na baadhi ya ndugu zake kwa kuhisiwa kuhusika katika upotevu wa mtoto Adamu Mselewa (4).
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa.
“Bado hali ni mbaya, bibi bado analalamika maumivu, tunaendelea na matibabu huku tukisubiri madaktari watatueleza nini kuhusu maendeleo yake, ikishindikana hapa tutamhamisha hospitali, afadhali kidogo Maurus,” alisema mwanafamilia huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mtoto wa kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mihayo Msekhela,  waliwakamata watuhumiwa 10 kutokana na tukio hilo, ambao ni Ambros Mselewa (24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda (45), Lameck Zenda (22),  Pautas Komba (24), Fredy Mende (24), Gerord Ngonyani (27), Odilo Mwingira (21), Shadrack Ngonyani (22), Hilda Zenda(36) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Muunganozomba.
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Ambros Mselewa akiwa pamoja na watu wengine walipoanza kuwashambulia watu hao wakimtaka kijana wao aliyepotea kimauzauza tangu Februari 3, mwaka huu.

VIDEO: DULLY SYKES AKIONGEO KUHUSIANA NA MSIBA WA BABA YAKE


FULL STORY YA MAPIGANO YA AL SHABAB NA VIKOSI VYA ULINZI VYA TANZANIA HUKO TANGA



Na Mwandishi Wetu, Tanga
NI kama kumekucha! Siku chache tu baada ya Gazeti la Ijumaa (ndugu na hili) kuandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; Kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini...NI HUYU, kundi jingine limeibuka na kuandika mkanda wa video wakizungumzia uhalifu.
Moja ya kikosi cha kigaida cha Al Shabaab.
Cha ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko kwenye Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya polisi, askari wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi likiwa limepiga makazi ndani ya mapango ya kihistoria ya  Amboni, Uwazi lina full story.
Katika mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.
MASHUHUDA WA MAPIGANO
Kabla Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye makazi yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na wahalifu yalitokea.
Mzee Ibrahimu Ally, yeye anasema: “Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi nilikuwa nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi kama mara mbili hivi.
“Mke wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi. Nilimwambia funga mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio ya risasi ikawa inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
“Ilifika mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi. Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa kweli. Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi haitajirudia tena.” 
Kundi la wahalifu wanaodaiwa kujificha na kushambulia Polisi katika mapango ya Amboni.
WAZIKIMBIA NYUMBA
Mwanahawa Mudale yeye alisema: “Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta) ikitembea angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa askari wetu.”
SIKU MBILI HAKUNA KULALA
Baadhi ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.
“Mimi na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi tu. Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la mapango. Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
“Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu,” alisema Simeon Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.
INAVYODAIWA
Habari zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga damu nchi jirani ya Kenya.
Moja ya Zana ya kivita ya Polisi ikiwa kazini kubambana na matukio ya uhalifu.
Wale jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje wafanye uhalifu baadaye.
“Sasa wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za kivita, wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na wao waje Tanga kujificha kwenye mapango.
“Lengo lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze. Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze kutoka kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja jamaa yao mmoja akakamatwa kwa uhalifu.
“Yule jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano makali kama yale,” alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
WANACHOAMINI WANANCHI, TOFAUTI NA POLISI
Uwazi lilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Tanga ambapo karibu wote walikuwa na mtazamo mmoja tu.
“Kutuambia wale ni majambazi si sawasawa. Majambazi wetu tunawajua, polisi wanawatosha sana, sasa hawa wametokea wapi mpaka JWTZ washirikishwe?” alihoji Paulina Mathias, mkazi wa Chumbageni, Tanga.
Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja.
Kusema ukweli serikali ituambie moja. Lakini wale si majambazi. Kwanza mpaka leo hii (juzi) hawajamkamata hata mmoja zaidi ya kujeruhi askari wetu na kumuua mmoja. Wale ni magaidi, lazima tuwe makini sana,” alisema Ally, mkazi wa Duga Maforoni, Tanga.
KUHUSU VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.
Watu hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara wakidai jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa.
KAULI YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya Amboni, Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku akisisitiza:
“Askari walifika mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano,  askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.      
GPL

NYOKA WA KICHAWI ANAVYOMTESA KONDO, AOTA MAGAMBA NA VIDOLE KUKATIKA


KWELI duniani hujafa hujaumbika! Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Kondo Athuman, mkazi wa Pugu Mnadani, Dar es Salaam amejikuta akiishi kwenye mazingira magumu kutokana na magamba kumtoka mwilini na kukatika vidole baada ya kumuua nyoka. 
Kondo Athuman akionyesha mguu unaotoka magamba.
CHANZO CHAKE
Akisimulia kwa huzuni, Kondo alisema mwaka 2006 alisafiri na mkewe kwenda mkoani Morogoro ambapo walipata shamba na kuendesha shughuli za kilimo cha mahindi na ufuta.
Alisema siku moja akiwa ametoka shambani alijipumzisha nyumbani kwake lakini ile anaingia ndani akamuona nyoka mkubwa na alijitahidi kumuua lakini kabla ya kumuua akakimbia, akashangaa kumuona wa pili akiingia na kufanikiwa kumuua.
ALIMUUA NYOKA, AKAMFUKIA, ASUBUHI AKAKUTA MTI
Akifafanua zaidi Kondo alisema baada ya kumuua nyoka wa  pili akiwa na mkewe waliendelea kumsaka yule wa kwanza ambaye aliingia chini ya kabati na kufanikiwa kumkata kichwa.
Baada ya kuwaua nyoka hao aliwatoa nje na kuchimba shimo kisha kuwafukia lakini cha ajabu alipoamka asubuhi na kwenda kuangalia alipowafukia, alikuta shimo likiwa wazi huku kukiwa kumepandwa mti.
KUISHIWA NGUVU NA KUTOKWA MAGAMBA
“Mara baada ya kuwaua wale nyoka nilianza kusikia baridi na kuishiwa nguvu  ambapo zilipita siku tatu nikaanza kutokwa magamba yanayofanana na wale nyoka huku nikitokwa na vidonda vikubwa mguuni na vidoleni kisha mikono ikawa inagoma kukunjuka.
VIDOLE VIKAANZA KUKATIKA
“Niliendelea kuumwa mpaka vidole vingine vikakatika kutokana na vidonda. Kweli nateseka ambapo baada ya kuzidiwa tuliamua kurudi nyumbani Dar ambapo nilienda katika hospitali mbalimbali na kupimwa vipimo vyote ambapo nilionekana sina ugonjwa wa ukoma wala mwingine wowote.
“Nikaanza kutafuta dawa za kienyeji kwa waganga. Mganga mmoja alinieleza kwamba wale nyoka hawakuwa wa kawaida bali walitumwa na yote hayo yalitokana na wivu kwani wazee wa pale Morogoro walikasirika walipoona tunawapita kimaendeleo kwa kuwa nilikuwa na bidii ya kufanya kazi na kuvuma mavuno mengi,” alisema Kondo.

WAFANYA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA WAZIDI KUKAMATWA


WATU wawili raia wa kigeni wanashikiliwa na polisi mkoani Lindi baada ya kukamatwa wakiwa na kilo 40 za madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye thamani ya shilingi bilioni 2.4, tukio lililotokea Februari 7, mwaka huu.

Miongoni mwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema watu hao, Ture Ally (55) raia wa Uganda na Sano Sadick Abobakary (53) wa Guinea Bissau, walikamatwa katika kizuizi cha Nangurukuru wakitokea Msumbiji kuelekea jijini Dar es Salaam.
“Polisi walikuwa wameweka mtego baada ya kupewa taarifa na raia wema, dawa hizo zilikuwa zimehifadhiwa katika paketi 40 zilizokuwa na uzito wa kilo moja kila moja na walikuwa na gari lenye namba za usajili UAU 789 na kesi yao ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Lindi.
Wakati huo huo, Februari 12, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, saa 7 usiku, polisi wa kitengo cha madawa ya kulevya, walimkamata msichana aliyetambuliwa kwa jina la Munira Mohamed (32) (pichani) mkazi Mombasa nchini Kenya akiwa na kilo1000 za Heroine.
Binti huyo ambaye bado hajafikishwa mahakamani, alikamatwa akiwa njiani kuelekea Nairobi na Mombasa na Kamanda wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa amewataka wananchi kuzidisha ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu mtu yeyote wanayemhisi kujihusisha na biashara hiyo haramu.
GPL.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014 NA QT HAYA HAPA

MAMA KANUMBA ANA LAANA, NDO MAANA ANAFILISIKA


   Stori: Laurent Samatta
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amemchana mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kuwa anateswa na laana na ndiyo maana hafanikiwi.

Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba. Mzee huyo alisema mama Kanumba ameshindwa kufanikiwa katika mambo mengi likiwemo suala la kuendeleza ofisi ya marehemu kutokana na kushindwa kumshirikisha yeye kama baba na ndiyo maana amepata laana.“Tatizo ni papara ya mwezangu ya kutaka mali ndiyo mambo yanayotokea na kamwe hataweza kufanikiwa kwa sababu baraka za mtoto zinatoka kwa mama na baba na hiyo laana itazidi kummaliza sababu hakunishirikisha,” alisema. 
Mama Kanumba Flora Mtegoa. Alipotafutwa mama Kanumba kuhusiana tuhuma hizo, alisema:
“Huyo mzee yeye ndiyo ana laana, nimeshamzoea, hana jipya amekalia majungu. Mimi sina laana, nakaa kwenye nyumba ya maana na si kama yeye anaeishi kwenye nyumba ya udongo.

BABA AMBAKA BINTI YAKE WA MIAKA 12 KWA WIKI 2 MFULULIZO



Stori: Hamida Hassan na Gladness  
BINTI mwenye umri wa miaka 12 aliyejitambulisha kwa jina moja la Irine, mkazi wa Mbagala-Charambe, Dar amesimulia tukio la kusikitisha akidai kubakwa na baba yake mzazi kwa muda wa takribani miezi miwili.
Akilisimulia Risasi Jumamosi mkasa huo wa kusikitisha hivi karibuni nyumbani kwao maeneo hayo, binti huyo alisema kuwa baba yake aliyemtaja kwa jina moja la Israel alikuwa akimfanyia unyama huo mara tatu kwa siku (dozi) pale mama yake anapokuwa hayupo nyumbani. 
“Baba amekuwa akinibaka wakati wa alfajiri kwa zaidi ya miezi miwili sasa hasa mama anapoamka na kwenda kazini na usiku tulipokuwa tukilala wakati mama hajarudi, wakati mwingine ilikuwa ni wakati mama akiwa anaoga bafuni,”
alisema Irine. Binti huyo aliendelea kusimulia kwamba baba yake huyo alikuwa akimwingilia kwa kumlazimisha na pale alipokuwa akikataa alikuwa akimpiga vibao na wakati mwingine waya wa umeme.
“Nilipokuwa nikimuuliza baba kwa nini ananifanyia unyama huo aliniambia hana kazi ndiyo maana ananifanyia hivyo na alikuwa akipenda kuniuliza kama nafurahia au nasikia raha pale tunapokuwa kwenye tendo, nikijaribu kulia ananipiga na kuniuliza nataka watu wamsikie hivyo navumilia maumivu,” alisema Irine kwa uchungu. 
MAMA MZAZI AFUNGUKA 
Akizungumzia mkasa huo, mama mzazi wa Irine alifunguka kwa uchungu na kusema kuwa amekaa na mwanaume huyo kwa muda wa miaka 12 lakini hajawahi kumuonesha tabia hiyo.“Ninachojua baba yake ni mkorofi kwani huwa ananipiga mara kwa mara na amekuwa hapendi kufanya kazi, nilikuwa nikimuhudumia kwa kila kitu kuanzia chakula hadi malazi,” alisema.
Kamanda Kihenya. Mama Irine alisema habari za kuwa anatembea na mwanaye alianza kuambiwa na mtoto mwenyewe lakini hakutilia maanani kwa sababu alipombana alikataa.“Wikiendi iliyopita niliambiwa na jirani yangu kuwa nifuatilie nyendo za mtoto kwani amekuwa akilia sana muda ninapokuwa sipo nyumbani, nilipomuuliza mwanangu akafunguka kila kitu,” alisema na kuongeza: 
“Baada ya kuniambia, nilimbana mume wangu akawa hana jibu na nilipomlazimisha tukampime mtoto alikataa na kusema niende mwenyewe.“Nilikwenda kumpima na kugundua kuwa ameshaharibiwa vibaya sehemu za siri ndipo nikaenda polisi Mbagala-Kizuiani na kufungua jalada la kesi namba MB/RB/1171/15 –UBAKAJI.” 
Aliongeza kuwa alipomaliza kufungua kesi alipanga na askari baba Irine akamatwe na ndipo akarudi nyumbani bila kumweleza mumewe lakini alikuta tayari ametonywa na watoto wake.
“Nahisi mtoto wangu wa kiume ndiye alimtonya mume wangu kwani tuliporudi hatukumkuta, hata hivyo polisi wanamsaka ili wamfikishwe kwenye vyombo vya sheria.


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga