KIKONGWE Hilda Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa.
“Bado hali ni mbaya, bibi bado analalamika maumivu, tunaendelea na matibabu huku tukisubiri madaktari watatueleza nini kuhusu maendeleo yake, ikishindikana hapa tutamhamisha hospitali, afadhali kidogo Maurus,” alisema mwanafamilia huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Ambros Mselewa akiwa pamoja na watu wengine walipoanza kuwashambulia watu hao wakimtaka kijana wao aliyepotea kimauzauza tangu Februari 3, mwaka huu.