Wiki hii kupitia ukurasa huu tunaye mwanadada anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa filamu anayefahamika sana kwa jina la Sandra lakini jina lake halisi ni Salama Salmini.Ni mama wa watoto wawili na anaishi na mume wake. Mwandishi Wetu Mayasa Mariwata hivi karibuni alimbana kwa maswali 10 na bila hiyana alitoa ushirikiano katika kuyajibu, shuka naye…
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo,Salama Salmini 'Sandra'.
TQ: Ni kitu gani kilichokufanya udumu kwenye ndoa yako mpaka sasa jambo ambalo wasanii wengi linawashinda?Sandra: Unajua mwanamke mjinga anaivunja ndoa yake mwenyewe, mimi siyo mjinga hivyo nailinda kwa kadiri ninavyoweza. Uvumilivu, kupendana kwa dhati na kuheshimiana ndiyo siri kubwa.TQ: Unapokuwa nyumbani kwako huwa unapendelea kuvaa mavazi ya aina gani, hususan ukiwa chumbani na mumeo?Sandra: Nikiwa nyumbani kwa kuwa naishi na wanangu huwa napenda kujifunga kanga na kuvaa madira lakini nikiwa chumbani, huko ni full kujiachia.
TQ: Inadaiwa wewe ni kati ya mastaa wasiopenda kufanya kazi za nyumbani na mara nyingi unamuachia majukumu hausigeli ikiwemo kumpikia mumeo, hili likoje?
Sandra: Sipendi kabisa mume wangu apikiwe chakula na hausigeli, mimi ni mwanamke ninayejua majukumu yangu, kwa hiyo hausigeli huwa ananisaidia tu.
TQ: Hivi siku ikitokea umemfumania mumeo utafanyaje?
Sandra: Kwa kweli naomba Mungu hilo lisitokee maana sijui maumivu nitakayoyapata, kwanza nitamsamehe sababu nampenda sana mume wangu.
TQ: Umeshawahi kuchepuka? Kuwa mkweli Sandra.
Sandra: Sijawahi kufanya hicho kitu wala sifikirii. Nifuate nini wakati kila kitu nakipata kwa mume wangu jamani? Sina tamaa za kijinga mimi.TQ: Hili la wasanii kuibiana mabwana halikutii hofu?
Sandra: Mimi sihofii hilo kabisa maana najiamini mno, kama mtu ni mal@ya, mal@ya tu hata umchunge vipi akiwataka atatembea nao.
TQ: Ni sehemu gani ambayo inakupa mzuka zaidi kwenye jumba la mah@ba?
Sandra: Ninapokuwa hayo maeneo kila kona ya mwili wangu huwa imejaa msisimko, ila napendelea zaidi ‘rom@nce’.TQ: Siku za wikiendi unapendelea kufanya nini?
Sandra: Napenda kutoka na familia yangu kwenda ufukweni kuogelea na kubadilishana mawazo na mume wangu.
TQ: Utapenda watoto wako warithi fani yako ya uigizaji?
Sandra: Sifikirii wanangu waje kuwa wasanii, kikubwa nawaombea mafanikio wawe watu bora zaidi kwenye taifa.TQ: Hivi baada ya kuolewa kwenda viwanja ndo’ basi?
Sandra: Naiheshimu sana ndoa yangu, sioni sababu ya kwenda kukesha klabu, huwa napenda kutulia chumbani na mume wangu na kutazama muvi.
GPL.