Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ameeleza kushangazwa kwake na taarifa zinazozidi kuenea kuwa amejifungua, jambo ambalo anadai eti siyo kweli.
“Mimi sina mtoto mdogo, mwanangu ni yule mnayemjua, hao wanaosema nimezaa mbona wananizalisha?” alihoji Snura ambaye baada ya muda mrefu kupotea, juzikati aliibukia kwenye Ukumbi wa Escape One ulipo Msasani, jijini Dar.