MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ambaye sasa anatamba na wimbo wake wa Tucheze amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa tangu atengane na mzazi mwenziye, Rose Ndauka bado hajatokea wa kumtetemesha.
Rose Ndauka.
“Unajua mambo yanapotokea lazima kukubaliana nayo na huwezi kulazimisha. Tangu uhusiano wetu usambaratike, hajatokea kama Rose,” alisema Malick.