Safari ya Ommy Dimpoz kuelekea Vegas, Marekani kwa ajili ya kupiga show imeishia airport ya marekani, baada y akuzuiliwa kuingia Marekani na kurudishwa na ndege inayofata.Habari zilizotufikia ni kuwa Dimpoz amerudishwa na kukataliwa kuingia ndani ya Marekani kwa kushindwa kufata msharti ya visa, ambapo visa aliyosafiria ilikuwa sio visa inayomruhusu kufanya show, na hivyo kumtilia shaka.
Baada ya kuongea na meneja wake Mubenga amesema, yeye mwenyewe hajui kinachoendelea na alijaribu kumtafuta bila mafanikio na sio kawaida ya Ommy kutokumjulisha kama amefika katika safari zake.


Ila leo asubuhi kwenye majira ya saa tatu amenicheki kuwa yupo njiani anarudi, anaingia leo usiku kwahiyo mpaka kesho mtakuwa na majibu, hajanieleza kwanini, aaaah mi nnachojua yeye anavisa ya marekani ya mwaka mmoja ya kufanya kazi" amesema Mubenga.