Issa mnally/Mchanganyiko
Baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna maeneo jijini Mwanza yanatisha kwa biashara ya ngono, Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivi karibuni imetua na kufanikiwa kufumua dangaro maarufu.
Makahaba hao wakiwa katika mawindo yao ya kila siku. Awali, dawati la OFM lilipokea sms kutoka kwa msomaji wake aliyeomba hifadhi ya jina lake iliyosomeka hivi: “Jamani nyie tunawaaminia kwa kufichua maovu, tumeona kazi nyingi nzuri mlizofanya Dar sasa tunaomba mje huku Mwanza maana kuna maeneo kama vile Liberty, Market Street, Deluxe na Villa Park, Kirumba yanatisha kwa uchangudoa.”
Baada ya kupokea meseji hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita kamanda wa OFM akiwa na wenzake walitingia jijini humo na katika zungukazunguka yao, walifanikiwa kunasa eneo maalum linalosifika kwa biashara hiyo haramu.
Ilikuwaje?
...Wakisubilia wateja.Mishale ya saa 8 usiku mapaparazi wetu walitonywa juu wa kuwepo mabinti waliojikusanya katika maeneo ya Liberty (Mwanza mjini) huku wakitumia nyumba moja iliyopo karibu na hapo kufanyia ufuska wao.
Bila kuchelewa, timu ya OFM ilifika na kuwakuta mabinti hao wakiwemo wake za watu wakiwa wamevaa kihasara ikionekana wazi walikuwa ‘sokoni’.
Kufuatia hali hiyo, maparazi wetu walianza kuwafotoa picha kitendo kilichowafanya watimue mbio kuelekea kusikojulikana.
Kamanda wa OFM akitua jijini Mwanza. Hata hivyo, baada ya timuatimua hiyo, inadaiwa wengi waligundua kuwa OFM wako Mwanza na wengi waliokuwa wakifanya ufuska eneo hilo walihama wakihofia kunaswa.
Uchunguzi uliofanwa na gazeti hili umebaini kuwa, kama ilivyo maeneo mengine, Mwanza pia wapo wake za watu na wanafunzi ambao nyakati za usiku huingia viwanja na kujiuza ili kupata pesa za kujikimu.OFM inaahidi kuendelea kufichua maovu mkoani humu ili kuhakikisha maadili yanachukua mkondo wake.