Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » KWA NINI MAKAMUZI YA MWANA FA JMOSI YALIFANA HUKO TANGA


Tunajua kuhusu umahiri wake kwenye uandishi wa mashairi pamoja na kumiliki stage, amedumu kwenye game tangu siku ya kwanza na bado anabakia kuwa bora kila siku ndio maana siku ya Jumamosi Oktoba 31, rapa mkongwe, Hamis Corleone Mwinjuma a.k.a Mwana FA aliacha historia ya aina yake Tanga kwenye ile show ya nguvu iliyoandaliwa na Vodacom.
Kabla ya kufanya show hiyo iliyopewa jina la ‘Mcheza Kwao Hutuzwa’ iliyofanyika katika ukumbi wa La Casachika, taarifa kutoka kwenye blog ya Issa Michuzi zimesema Mwana FA alitembelea kituo cha yatima cha Diana kilichopo Tanga na kukabidhi zawadi ya jezi kwa niaba ya kampuni simu ya Vodacom Tanzania.
Mwana FA Tanga
Mwana FA akikabidhi zawadi ya Jezi kwa Niaba ya kampuni ya Vodacom Tanzania kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Diana, Tanga.
Mbali na hilo, msanii huyo alikabidhi zawadi kwa mshindi wa simu ya Vodafone Smart alipotembelea duka la Vodacom lililopo barabara ya tatu, Tanga.
Mwana FA II
Mwana FA akipiga ‘Selfie’ na mshindi wa Vodafone Smart, Kika Martin Joseph baada ya kumkabidhi zawadi ya simu hiyo kwa niaba ya kampuni ya Vodacom Tanzania.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga