Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » » CHRISS BROWN AFUNGUKA UHUSIANO WAKE ULIOVUNJIKA KWA RIHANNA



Baada ya ukimya wa kama miaka 5 hivi, Chris Brown ameamua kuzungumzia yote yanayomhusu ikiwemo mahusiano yake na Rihanna.
Chris amesema kila kitu ni kama ilikuwa ‘mistake’, na hana haja ya kuwa na majuto kwa kuwa tayari walirekebisha tofauti zao na kwa sasa ‘pepo’ alilonalo ni pepo la kuogopa kushindwa.
Akizungumzia kuhusu yeye na Rihanna, amesema “..naamini ilikuwa ni makosa ambayo siwezi kuyarudia.. nikiangalia nilikuwa nna umri wa kama miaka 17 au 18.. sasa nna 25.. najikuta bado natumikia adhabu ya kufanya huduma za kijamii na natakiwa kuonana na jaji kila baada ya mwezi mmoja na nusu kutokana na tatizo lile..”
Chris Brown na Rihanna walikaa kwenye headlines ambapo imesemekana walijaribu kama kuufufua uhusiano wao, ambapo Chris anasema alihitaji kumuonyesha Rihanna kwamba anaweza kubadilika na kuwa mwanaume ambaye Rihanna anamuhitaji.
Baada ya Chris kumuona Rihanna kwenye show ya Oprah akizungumzia kwa hisia kuhusu Chris, na kusema upo uwezekano wakawa marafiki, Chris aliona namna ambavyo Rihanna anamjali, kitu ambacho hakuwahi kukiona kwa kipindi kirefu, lakini kizaazaa kikawa pale Rihanna alipoanza ‘kutoka’ na Drake ambapo Chris alihisi kuwa Rihanna anafanya hivyo kumuumiza japo yeye hana uadui na yoyote kati yao.
Chris & Drake
“.. Namna ninavyofanya.. Iko wazi.. Hii ni game, sisi ni vijana.. tunafanya hivi ni kwa sababu ya umri. Nadhani tukifikia miaka 30, tutakuwa tumepevuka na malengo yetu hayatokuwa upande huo tena..”
“..Tumalizane na masuala ya ugomvi, itaonyesha namna gani tumekua na tumepevuka..”-Chris Brown

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga