Papa Misifa ( wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Cassim Mganga
Meneja wa  zamani wa Diamond Platnumz, Msafiri Misifa maarufu kama Papa Misifa,  amesema wasanii wengi wanashindwa kuendelea kutokana na kushindwa  kuhifadhi wanachokipata.
Papa  Misifa aliyewahi pia kuwa meneja wa Dully Sykes na Cassim Mganga,  ameiambia Bongo5 kuwa Diamond ni msanii pekee aliyeweza kufuata mafunzo  yake na ndio maana anaendelea kufanikiwa mpaka sasa.
“Tatizo  kubwa wasanii sana wanapopata riziki wanashindwa kujipangilia. Na  mafunzo mengi niliyompa Diamond ndo maana mpaka leo anajua kujipangilia  mpaka pale alipofika. Wasanii wanashindwa kupangilia pesa zao. Tatizo  wanapopata pesa wanabadilika. Ukitaka kujua tabia ya mwanadamu ngoja  apate pesa ndo utajua tabia yake,” amesisitiza.
“Wasanii  wengi hawalengi kufanya vitu vya maendeleo, wanalenga kufanya starehe  kwenye baa. Ndio maana watu wanasema wanamuziki wa zamani wamefulia ni  kweli kwa sababu hawakujipanga. Hawakutambua kesho yao, wewe unafikiri  kwanini Diamond anaiogopa kesho yake? Ni kutokana na maisha yalivyo  ukipata nafasi itumie ipasavyo.”
