Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » JOKATE ALAMBA SHAVU


Baada ya Salama Jabir kupata shavu la kuwa na show kwenye kituo cha runinga cha Maisha Magic, sasa ni zamu ya Jokate Mwegelo. Mtangazaji huyo anatarajiwa kuongeza show yake ya tatu katika TV (baada ya The One Show ya TV1 na Top 10 Most ya Channel O), itakayoanza kuonekana kupitia Maisha Magic, December mwaka huu.

Jokate atashirikiana na mtangazaji maarufu wa Uganda, Gaetano Kagwa kuendesha kipindi hicho kiitwacho Beat the Challenge.
Beat the Challenge ni kipindi kitachokuwa kikihusisha mashindano ya familia 12 (baba, mama na watoto wao wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 17) wataokuwa wakihusika kwenye kazi mbalimbali na kuulizwa maswali kuhusu uelewa wa masuala mbalimbali.

Show hiyo itaanza kuonekana kupitia Maisha Magic (DSTV CHANNEL 161(, Jumamosi ya December 13, saa 2 na nusu usiku. Usaili utafanyika Nairobi November 22, Supersport Studios, Tanzania ni siku hiyo hiyo New Africa Hotel Dar es Salaam na Kampala utafanyika Silver Springs Hotel Kampala,kuanzia saa tatu asubuhi.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga