Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » » BLUE "KAMA SIO NGOMA YA "PESA" GAME INGEKUWA BASI


Akizungumza kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, rapper huyo alidai kuwa kama ngoma yake ‘Pesa’ ingebuma, angeachana kabisa na muziki na kuzamia Ulaya.
“Pesa kama Pesa ilikuwa ni project yangu ya mwisho,” alisema Kabayser. “Nilikuwa nimeshakata tamaa. Vitu vingi vilikuwa vinanisumbua, nilikuwa naplan kidogo niwakimbie watanzania nikatulie Uingereza. Nyumba yangu ilikuwa ipo kwenye finishing na itahitajika kama milioni 25 nimalize au 30 labda, nitaipata wapi hiyo hela, ikiwa mimi kazi yangu ni muziki? Ndioa Mungu akanisaidia nikatoa lile jiwe Pesa. Kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu ikawa ni balaa,” aliongeza.
“Sasa baada ya kupata ile pesa ikabidi nichague nimalizie nyumba yangu au nitoe video watu wanijue kama huyu ni Mr Blue! Kwahiyo hela yangu yote nawashukuru Serengeti Fiesta naomba niseme wazi kabisa ni watu ambao wamenisaidia hilo tatizo. Kwasababu hela hiyo yote niliipata kwenye Fiesta.”
Kuhusu video ya Pesa, Blue alidai kuwa Adam Juma alishoot video ya Pesa bure, bila kumpa chochote.
“Adam Juma from nowhere, ni mtu ambaye sikuwahi kufikiria nitafanya naye video. Nilishajaribu kutaka kufanya naye lakini mipango ikawa haikamiliki. Alinipigia simu mwenyewe namshukuru sana Adam Juma na Mungu akusaidie kwa kunipa video bure kabisa! Yaani video kila kitu bureee kabisa. Mimi nasema kuishi na watu kwa upendo ndo zimefanya hivyo ninaweza kusema ni zawadi.”
Credit: Bongo5.com

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga