MWANAMUZIKI Winfrida Josephat ‘Rachel’ juzikati aliwashangaza watu baada ya kudai kwamba siku hiyo baada ya shoo yao akiwa na Kundi la Kigoma All Stars mjini Nairobi alikuwa akitafuta bwana wa kumpa kampani usiku bila mafanikio.
Mtandao mmoja wa Kenya wa Standard Digital News uliandika kuwa, siku hiyo baada ya shoo akiwa anazungumza na mapaparazi wa huko binti huyo alisema alikuwa akitaka mtu wa ‘kujivinjari naye’ lakini akafedheheka kwa kumkosa yule wa kumpa furaha ya kimahaba.
Ijumaa lilimtafuta Rachel kupitia simu yake ya mkononi kuzungumzia hilo na alipopatikana alisema:
“Mimi kuongea hivyo si kitu cha ajabu kiasi cha kuifanya mitandao ya Kenya inicharukie. Kwani kuna ubaya gani kusema natafuta mtu wa kuniridhisha? Ile ni mbinu tu ya kuwateka mashabiki.”
“Mimi kuongea hivyo si kitu cha ajabu kiasi cha kuifanya mitandao ya Kenya inicharukie. Kwani kuna ubaya gani kusema natafuta mtu wa kuniridhisha? Ile ni mbinu tu ya kuwateka mashabiki.”