UCHUMBA wa muda mrefu kati ya msanii wa filamu za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ na Saguda George ‘Polite’ umeanza kusengenywa na baadhi ya wadau wakidai umekuwa wa muda mrefu bila kuwepo kwa dalili yoyote ya kuoana.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mmoja wa rafiki wa Recho ambaye pia ni msanii wa filamu (jina tunalo) alisema wasanii wenzake wamekuwa wakiusimanga uchumba huo uliodumu kwa takribani miaka mitano sasa, huku wengi wakidai ni wa Kichina.
“Kwa kweli uchumba huo unasengenywa sana hadi wakati mwingine wanakosa amani wenyewe,” alisema rafiki huyo.
Mwandishi wetu alimtafuta Recho kwa njia ya simu ambapo alikiri kusikia maneno hayo na kudai kuwa watasema sana na kamwe hawezi kuvunjika moyo, huku akiamini ipo siku ataitwa mke.