HAYO NDIO MAMBO YA MISS JELA HUKO BRAZIL, WAREMBO WAKALI NDANI YA ULINZI MKALI
HAYA ni mashindano ya urembo yanayofanyika kila mwaka katika moja ya gereza la wafungwa huko nchini Brazil, waliyoanzisha mashindano haya wanasema wanawapa haki wafungwa nao wajisikie kama binadamu na si kama wanyama kwani muda mwingi wanakuwa wanafanya kazi kwahiyo inakuwa sio mbaya kuwapa muda kidogo wajifurahishe katika mioyo yao na sio muda wote waonekane watumwa wa kazi. Mshindi wa taji hilo anapewa uangalizi na zawazi za kutosha kutoka kwa waandaaji wa shindano hilo.