Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

JOYCE KIRIA AKWAA DENI LA MIL 500 BAADA YA KUTOA SIRI YA MBUNGE WA ZANZIBAR


Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.

Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi

MAKAH@BA MWANZA WAVAMIWA NA OFM WAKIWA WANAJIUZA


Issa mnally/Mchanganyiko
Baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna maeneo jijini Mwanza yanatisha kwa biashara ya ngono, Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivi karibuni imetua na kufanikiwa kufumua dangaro maarufu.

Makahaba hao wakiwa katika mawindo yao ya kila siku. Awali, dawati la OFM lilipokea sms kutoka kwa msomaji wake aliyeomba hifadhi ya jina lake iliyosomeka hivi: “Jamani nyie tunawaaminia kwa kufichua maovu, tumeona kazi nyingi nzuri mlizofanya Dar sasa tunaomba mje huku Mwanza maana kuna maeneo kama vile Liberty, Market Street, Deluxe na Villa Park, Kirumba yanatisha kwa uchangudoa.” 
Baada ya kupokea meseji hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita kamanda wa OFM akiwa na wenzake walitingia jijini humo na katika zungukazunguka yao, walifanikiwa kunasa eneo maalum linalosifika kwa biashara hiyo haramu.
Ilikuwaje?
...Wakisubilia wateja.Mishale ya saa 8 usiku mapaparazi wetu walitonywa juu wa kuwepo mabinti waliojikusanya katika maeneo ya Liberty (Mwanza mjini) huku wakitumia nyumba moja iliyopo karibu na hapo kufanyia ufuska wao. 
Bila kuchelewa, timu ya OFM ilifika na kuwakuta mabinti hao wakiwemo wake za watu wakiwa wamevaa kihasara ikionekana wazi walikuwa ‘sokoni’.
Kufuatia hali hiyo, maparazi wetu walianza kuwafotoa picha kitendo kilichowafanya watimue mbio kuelekea kusikojulikana.
Kamanda wa OFM akitua jijini Mwanza. Hata hivyo, baada ya timuatimua hiyo, inadaiwa wengi waligundua kuwa OFM wako Mwanza na wengi waliokuwa wakifanya ufuska eneo hilo walihama wakihofia kunaswa. 
Uchunguzi uliofanwa na gazeti hili umebaini kuwa, kama ilivyo maeneo mengine, Mwanza pia wapo wake za watu na wanafunzi ambao nyakati za usiku huingia viwanja na kujiuza ili kupata pesa za kujikimu.OFM inaahidi kuendelea kufichua maovu mkoani humu ili kuhakikisha maadili yanachukua mkondo wake.


HEBU MUONE LADY JAY DEE ENZI ZA KU RAP


Kweli maisha ni safari ndefu, mkali Jide wa enzi hizoo, kipindi anachana, alikuwa bonge la msela. cheki picha kali nyingine hapo chini.

SHILOLE AWAWAKIA WALIOMPONDA KWA KUWA KICHWA WAZI MSIBANI KWA MEZ B



Nawaangalia tu wote mnaonisnich kama ww unajiua ni snich jitoe tu coz hata mm sina time na ww! Tusilazimishane kuwa kama ww mm ni mm na ww ni ww so naona au coz mm ni shilole nisingeenda msiban pia mngechamba oooh wasanii hamjaliani sasa mm nimekwenda lakin bado oooh nywele
 sijafunika! Plzzz tusiingiliane mbona hamna jema nyinyi loh! Mnikome nafanya kile ambacho naweza kufanya kwa wakati huo so tuheshimiane (tusi) tena nyie ambao mnasema ooooooo hujafunga kitamba kichwani hata misiban hamjaww kwenda 

HATIMAYE MILLARD AYO AMILIKI STUDIO YAKE YA RADIO


Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini
hii na baadae watu wangu francis_ayo na abdul8819 wa pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa. 

HAYA SASA, HIZO NDO SIFA ZA MWANAUME ANAEMTAKA JAY DEE


SIFA ZA MWANAUME AMTAKAE LADY JAYDEE KWA SASA Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa? JIBU :Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona ),Asiwe
tegemezi.Hata kama sio tajiri lakini asinitegemee.Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar,Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale.Nikikohoa tu awepo hapo Kwa mtazamo wako unaweza kupata Mwamke au Mwanaume asiye na mapungufu?

BARUA YA JACK AKIWA GEREZANI, ALIA NA USALITI WA P3NZI LAKE KWA JUX, DIAMOND NA ZARI NA SKENDO ZA MASTAA WA BONGO



Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.

Modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’.
BARUA KUTOKA CHINA
Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani map3nzi hayachagui hasa kama ana furaha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike map3nzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika Jack.
DIAMOND, ZARI
Mbali na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo alionesha kushtushwa na p3nzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh! Wala hawatadumu maana map3nzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond Platnumz) atahamia South.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakiwa kwenye pozi.
KAJALA Vs WEMA
Pia video queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan (ya Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la Wema na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies walishazoeleka kugombana na kupatana.
Bifu hilo ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK) huku akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa wako hivyo kila muda, kawaida yao.”
JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malov3e na s3xy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.
Juma Khalid ‘Jux’, akiwa na mp3nzi wake Vanessa Mdee.
“Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack.
Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapema hivyo hatakaa jela miaka yote sita.

BAADA KUKOSA MUME, MISS DODOMA AAMUA KUOKOKA


Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans amemrudia Mungu kwa maana ya kuokoka kwa kile alichodai kutotimia kwa malengo aliyojiwekea.Akizungumza na mwanahabari wetu, Eva alisema tangu akiwa mdogo, alijiwekea kiapo kuwa endapo atashindwa kumpata mume mwema, basi atafanya kazi ya kumtumikia Mungu.
Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans akiwa kanisani.
“Nakumbuka mapito yangu yote tangu nikiwa mdogo mpaka nikaingia kwenye masuala ya urembo nilijiwekea nadhiri ikifika muda mambo yangu hayajakamilika, itanibidi nimrudie Mungu wangu.
“Baada ya kupitia urembo nilichumbiwa, hapohapo nikaanza kuhudhuria mikutano mbalimbali ya neno la Mungu, siku moja Nabii akitoa neno, nilimsikia akisema kuna binti mmoja hapa anataka kuolewa apite mbele haraka sana, basi nikapita mbele na nilipofika pale alianza kuniombea na baadaye alianza kuniuliza maswali.
“Akaniambia mwanaume anayetaka kunioa hana sifa za kuwa mume bora na kama nabisha nimchunguze, basi nikamchunguza na kugundua kuwa hakuwa na sifa.“Basi nilivyojua tu nikaamua nisitishe mipango ya ndoa zikiwa zimesalia wiki mbili tu ili ndoa ifungwe, nashukuru Mungu nilieleweka, na kuanzia hapo nikaamua kuokoka kabisa, ninaomba sana Mwenyezi Mungu aniletee mume mwema,” alisema mrembo huyo.
Eva alifunguka kuwa katika mashindano ya urembo kuna uchafu mwingi hivyo akawashauri wasichana walioko huko kumrudia Mungu.
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga