Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

Majanga ONA Majanga!!!! Mpaka Kieleweke Leo!!


Kama kawaida, Cheka Upate Afya, leo nakuletea Picha niliyoipata katika mtandao wa kijamii huku ikiwa Commented ya Kwamba Mpare Utamjua Tu!!!! Walionaje hili?

Ajali!!!!Akuta Panya Ndani ya Wali Rost Nyama Aliouagiza.


Hali ya Sitofahamu imejitokeza katika Mgahawa mmoja huko Africa Magharibu baada ya Mteja aliyekuwa ameagiza Wali Rost nyama ya kukaanga kukutana na "KAPANYA" Kadogo kameiva ndani ya chakula alichokiagiza.

Mteja huyo alikumbwa na bumbuwazi na hasa ukizingatia alikuwa ameshakula chakula hicho kwa zaidi ya Asilimia 90.

Za mwizi, 40.!!! Kibaka achezea kipigo huko Kawe, ni baada ya kuruka geti.


Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.…
Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.
Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi waliochoshwa na wizi.
...Akiendelea kusulubiwa kabla ya kupelekwa polisi.
Baada ya kulainika akawa anapelekwa polisi.
Kutokana na kipigo jamaa huyo alianguka hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa.

MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Source:GPL

Ndege Abadilika na kuwa Binadamu baada ya Kudondoka Chini Mchana Kweupee!!!

-->

Walioshuhudia tukio hilo wamesema ilikuwa kama sinema au mchezo wa kuigiza kwani walikuwa ndege watatu wanapaa angani, ghafla mmoja akadondoka na akatumbukia katika ki mfereji cha maji, hapo ndipo alipojaza watu kwani alibadilika kutoka kuwa ndege na kuwa binadamu.

Ilibidi polisi waingilie kati na kumchukua mwanamke huyo ambaye alijieleza ya kwamba anatokea Ikole na Ni Mkazi wa Jimbo hilo la Ekiti Huko Nigeria.

Polisi hawaamini uchawi, sijui suala la mwanamke huyo watalishughulikiaje!!!!

Angalia Jinsi Bongo Movie Wanavyopondwa na Kutathminiwa hapa



UTAJUAJE NI BONGO MOVIE? 

1.Jini akifika barabarani
anaangalia
pande zote ndo avuke barabara. 

2. Matajiri majumba yao yana askari
badala ya electric
fence &
gates.
3.Trailer inachukua
dakika 40.
4.Part2 ya movie ukiiona
mwanzo unajua part1
ilikuwaje.
5.Madem wanaamka wanamake ups
usoni na hereni kabisa.
6.Wakifika hotelini imezoeleka ni juice
inaagizwa au wine
isiyofunguliwa.
7.Nusu saa mtu anatembea,anafanya
mazoezi,anakimbizwa au ananunua vitu.
8.Wimbo wa malavidavi
unaimba
mpaka unaisha.
9.Mtu yupo
village,life gumu ana wave kichwani.
10.Wote wanaouwawa kwa risasi
hupigwa kifuani au
tumboni sio kichwani.
11.Jambazi
lazima awe anavaa miwani nyeusi,koti
kubwa na mvuta sigara mwenye sauti
nene na sura ya kutisha
12Tajiri anakuja kumpenda maskini.
13. Jina La Movie La Kingereza, Ndani
Mazungumzo Ni Kwa Kiswahili.
14.Editor Roy Kijusi, Camera man
Inosenti Kijusi, graphic designer Roy
Kijusi, Location manager Happy Kijusi,
Mavazi Suzy Kijusi.
15.Movie inapart1 na part2,lakn
ukiangalia unagundua ni disc.1 na disc.2
16.movie inaitwa life is harder (mfano)
afu kwenye kava watu wameweka
mapozi ya mamodo na warembo."


Hii nimeikuta face book, huku ikipata Comment zaidi ya 30, Likes ndo Usiseme, Vipi ndugu Msomaji wangu, unalionaje hili?

Nabii Achezea Kipacho, Baada ya Kutuhumiwa kuwa na Uhusiano na Mume wa Mtu, Mchungaji.

-->
Nabii Juliana Aliyechezea Kichapo

Stori:Gladness Mallya na Sanchawa
MWANAMKE anayejulikana kwa jina la Nabii Juliana wa Kanisa la Miracle Assemblies of God, amepigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuingilia ndoa ya Mchungaji Richard Kiondo.

Nabii Juliana Aliyechezea Kichapo
Tukio hilo la aina yake ambalo lilikusanya umati wa watu, lilitokea hivi karibuni maeneo ya Ukonga Mazizini, jijini Dar ambapo nabii huyo alipigwa hadi kuchaniwa nguo.
Akielezea mkasa huo, mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo, Christina Kiondo alisema baba yake alikuwa akishirikiana kwa huduma ya kanisa na Nabii Juliana lakini katika ushirika huo anaamini wawili hao walikuwa na uhusiano usiofaa.
Alisema kisa cha nabii huyo kupigwa, hivi karibuni mwanamke mmoja alikwenda nyumbani kwa Mchungaji Kiondo na kuwaeleza watoto hao kwamba anamdai baba yao shilingi 40,000, kitu ambacho kiliwashitua sana kwa kuwa baba yao anaishi kwa nabii na pia hawakujua fedha hizo alikopa kwa ajili ya familia gani.
Mtoto mkubwa wa mchungaji huyo, alimtuma mdogo wake nyumbani kwa nabii huyo kwa lengo la kwenda kumuita baba yao ili aje kuzungumza na mwanamke huyo.
Ilidaiwa kuwa, mtoto huyo alipofika alikutana na nabii na kumwambia amemfuata baba yake lakini alimfukuza.
“Baadaye alikuja hapa nyumbani na kuanzisha varangati kitu ambacho hakikukubalika kwa majirani kwani tangu siku nyingi wanajua uhusiano wake wa baba.
“Majirani walitoka kwa wingi baada ya kumsikia nabii akitufanyia fujo, walianza kumshushia kipigo mpaka alipokuja kuokolewa na mjumbe wa eneo hili na kupelekwa polisi,” alisema Christina.
Akizungumza na mapaparazi wetu, mjumbe wa eneo hilo Joseph John ‘Mzee Kasheshe’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Kwa upande wake, mke halali wa mchungaji huo ambaye yuko Mbagala kwa matibabu, alisema alizipata taarifa za nabii huyo kupigwa.
Aliongeza kuwa tangu zamani mama huyo alikuwa akienda na mumewe nyumbani hapo akidhani kuwa wote ni watumishi wa Mungu hivyo hakuwahi kuwatilia shaka hadi baadaye sana aliponyetishiwa na watu.
Kufuatia kipigo hicho, Nabii Juliana alipofika polisi alitoa malalamiko yake na kufungua kesi yenye kumbukumbu: MAZ/RB/2246/2013 KUHARIBU MALI.

Source: GPL.

Mwanafunzi Ashikiwa Uchawi, Akutwa na zana kibao za uchawi huku akiwa na Nguo ya Ndani Tu!!!


Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa
AMINI usiamini, duniani kuna uchawi! Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Pasco (21) ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Samaritan iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara amekutwa getini kwa kaka’ke, Edward Raphael akiwa amefungwa kamba na matunguri.
Denti akiwa amaefungwa kamba
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni huko Yombo-Buza jijini Dar na kuibua sekeseke la aina yake kutokana na mazagazaga ya kichawi aliyokutwa nayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Pasco alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni huku akiwa na nguo ya ndani pekee.
Habari zilieleza kuwa pia kijana huyo alikuwa amepakwa unga na kuandikwa maandishi ya Kiarabu mwilini huku kiunoni akiwa na shanga, hali iliyowashangaza wengi.
Polisi akiwa eneo la tukio
Akizungumza na wanahabari wetu juu ya tukio hilo, kaka wa kijana huyo alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, wiki mbili zilizopita ambapo aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake lakini alipofungua geti alishangaa kumuona mtu akiwa amelala akiwa hajitambui.
Alisema baada ya tukio hilo, alirudi ndani haraka na kumwita mpangaji wake ili akashuhudie alichokiona.

Mazagazaga aliyo kutwa nayo
Alisimulia kuwa baada ya mpangaji huyo kuamka, waliamua kwenda polisi lakini wakiwa huko, mkewe aliamua kwenda kumchunguza mtu huyo kwa makini usoni ambapo aligundua kuwa ni shemeji yake, jambo ambalo lilizidi kuwachanganya watu.
Alisema aliporudi alikuta umati mkubwa wa watu umemzunguka Pasco.
Wakazi wa eneo hilo wakishangaa

Kaka mtu alisema kuwa alitimba na askari ambao walimfungua kamba na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza lakini wakiwa njiani, kijana huyo alikuwa akiongea maneno ya ajabu kama vile mtu mwenye majini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina la Mube, Joseph Paja alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema naye alikuwa miongoni mwa mashuhuda.
Alisema kuwa alipofika, alikuta kijana huyo aliyewahi kuishi mtaani hapo kwa kipindi kirefu akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hali ambayo ilimshangaza kila mtu.
Mchungaji wa Kanisa la Church of World, Steven Paul ambaye naye alishuhudia tukio hilo, alisema kuwa baada ya ndugu kuamua kumpeleka polisi aliambatana nao hadi kituoni lakini walipofika, askari walimtema kwa kigezo kuwa hakuwa na kesi ya kufunguliwa, wakashauri apelekwe hospitali.
Ilielezwa kuwa zoezi la kumpeleka hospitali lilifanyika lakini walipofika huko, madaktari walimkataa kwa kigezo kuwa hawakuona ugonjwa wowote, jambo lililosababisha hofu kutanda.
Akizungumza na waandishi wetu, mchungaji huyo alisema kutokana na kote huko kushindikana, aliamua kumchukua kijana huyo na kuishi naye nyumbani kwake kwa lengo la kumfanyia maombi.
Baada ya kumchukua, alianza dozi ya maombezi ya nguvu ambapo hivi sasa anaendelea vizuri.
Katika mahojiano na waandishi wetu, Pasco alisema hajui kilichotokea hadi akajikuta amefika Dar, tena getini kwa kaka yake akiwa uchi.
Alisimulia kuwa siku hiyo, alienda benki kutuma ada ya shule na baada ya hapo, alirudi nyumbani kwa bibi yake na kumkuta akiandaa ugali ambapo alikula kidogo kwani alikuwa akihisi maumivu makali ya kichwa.
Baada ya kushindwa kula vizuri, bibi yake alimtaka ale chungwa ambapo alichukua moja na kwenda nalo chumbani, akachukua panga kisha kulikata vipande viwili lakini alipoanza kula, kabla ya kumaliza kipande kimoja alihisi usingizi mzito ambapo alikuja kushtukia akiwa sehemu tofauti yaani getini kwa kaka yake akiwa amezingirwa na watu kibao.
Alieleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na mauzauza ya kichawi ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kaka yake amhamishie Rorya mkoani Mara ambako alienda kuanza kidato cha pili wakati huku Dar alikuwa ameshafika kidato cha nne.

Chanzo: GPL

Cheka Upate Afya, Waionaje Tathmini hii ya Elimu ya Bongo?!!!

-->

Hapo Vipi Mjomba? Kwa Hali hii Tutafika Kweli?!!!!!!!!!!

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga