Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » Amuua Kijana wa miaka 17, sababu ya sauti kubwa ya muziki katika gari lake.

Michael Dunn

Michael Dunn, 45, mkazi wa Florida, yupo mahabusu bila dhamana kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua Jordan Davis,17 baada ya kupishana kauli chanzo kikiwa ni sauti ya muziki kuwa ya juu sana.

Siku ya tukio(jana) Jordani na wenzake watau walikuwa katika gari alilokuwa anaendesha Jordani, walipoingia kituo cha kuweka mafuta walimkuta Michael akiwa na Mpenzi wake nao wanaweka mafuta, kwa vile gari lao lilikuwa na mziki mkubwa Michael alishuka na kuwafuata akiwataka wapunguze sauti, hata hivyo mambo yalikuwa kinyume kwani sauti haikupunguzwa na mabishano yakaanza.

Dunn alitoa bastola na kuanza kulipiga gari hilo na ndipo risasi mbili zilipomuingia kijana huyo. Dunn anakabiliwa na shitaka la mauaji na jaribio la kutaka kuua wale watatu walionusurika. Bado yupo mahabusu mpaka mwezi wa 9 kesi itakaposomwa tena.

Mwanasheria wake amemtetea kwa kusema eti ameua bila ya kukusudia baada ya kuitoa ile bastola aliingia uoga na hivyo akajikuta anipiga tu, ingawa wengi walikataa hilo kwani inaonesha ni jinsi gani anatafuta pa kutokea kama Zimmerman aliyemuua Trayvon Martin.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga