Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » » Askari Polisi Asimulia jinsi Wanajeshi wa JWTZ walivyouawa huko Darfur


Majeruhi wakiwa wodini huko Sudan

 Wakati Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa bado halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko Sudan, askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio hilo.
Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.
Gazeti hili limepata majina ya askari hao waliofariki kutoka vyanzo tofauti lakini limeshindwa kuwataja leo kwa kuwa JWTZ kupitia kwa msemaji wake, Kanali Kapambala Mgawe limesisitiza kuwa haliwezi kutangaza majina hayo hadi litakapowasiliana na jamaa za askari waliofariki.

Tukio lilivyotokea
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.
“Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena katika doria waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki, waliyafuatilia, walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,” alisema askari huyo na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban kilometa 70 kutoka katika kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la kusini na hiyo kambi ya Korabeche inaongozwa na jeshi letu.”

Akizungumzia kazi ambazo polisi wanazifanya huko, alisema hawaruhusiwi kushika silaha, bali kuwashirikisha wananchi katika masuala ya amani.
“Sisi majukumu yetu ni kuungana na jamii na kuwafundisha masuala mbalimbali, hivyo sisi tunawasiliana moja kwa moja na wananchi waliopoteza makazi kisha tunaandaa taarifa. Haturuhusiwi kushika silaha, wanajeshi wao wanatulinda na kusimamia usalama na kutusindikiza wakati wa doria,” alisema.
“Huku hali ya usalama haitabiriki. Mpaka sokoni tunakwenda chini ya ulinzi.”

Kauli ya JWTZ
Akizungumza kwa simu jana, Kanali Mgawe alikanusha uvumi wa majina yaliyosambaa mitandaoni huku akisema kwa utaratibu uliopo, jeshi haliwezi kutangaza majina hayo hadi ndugu watakapotaarifiwa. “Hayo majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alidai Kanali Mgawe.
Hata hivyo, alisema Tanzania imewasilisha maombi ya kubadilisha kanuni za kulinda amani ikitaka kuruhusiwa kujihami kwa silaha za moto pale wanajeshi wake wanaposhambuliwa kwa kutumia kanuni namba saba ya Sheria za Majeshi ya Kulinda Amani.

Source: Mwananchi.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga