Ulimwengu utakuwa unaadhimisha Miaka 95 ya kuzaliwa kwa shujaa wa Africa ya Kusini Mzee Nelson Mandela wakati mwenyewe akiwa hospitalini akipigania uhai wake kwa msaada wa mashine.
Watu wakujitolea watatumia dakika 67 kesho kama ishara ya kumbukumbu ya matukio yaliyofanikishwa nae katika jamii za mia moja tofauti ndani ya miaka yake 67 ya mapinduzi ya kisiasa.
Mnamo mwaka 2010, umoja wa mataifa ulipitisha Mandela kupewa Tuzo ya amani ya Nobel huku akiiadhimisha sambamba na siku yake ya kuzaliwa.
Miongoni mwa matukio yanayotarajiwa kufanyika ni kwa watoto shule zote nchini Africa ya kusini kuanza masomo yao baada ya kuimba nyimbo maalumu za Siku ya kuzaliwa kwa ajili ya Mzee Mandela.