Usingizi ni dawa ambayo inaweza kukutibu bila wewe kujua, kwa hiyo inafaa uitumie mara nyingi Ni wengi katika jamii ambao hawafahamu umuhimu wa kupata muda mzuri wa kulala katika maisha yao. Pia, wengi hawatambui jinsi ukosefu wa usingizi wa kutosha ulivyo na athari kwao na kuwa kulala kwa muda mfupi kunapunguza kichochezi dume kiitwacho testosterone Mwonekano wa mwanamume yeyote duniani na kupata sifa ya kuitwa mwanamume husababishwa na kichochezi hiki testosterone.
Kichochezi hiki kiletacho tabia na maumbile ya kiume na kumpa mtu sifa ya kuitwa mwanamume kinaweza kuathiriwa na ukosefu wa usingizi wa kutosha. Kichochezi hiki kinazalishwa katika sehemu za uzazi za mwanamume katika korodani na hutiririshwa kutoka korodani na kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili kupitia njia ya damu. Homoni hii ndiyo inayotoa maumbile na kazi za kimwili kwa wanaume na hufanya maumbile ya kiume kuwa na misuli iliyo kakamavu, mifupa imara, kuota ndevu, kupata ndevu za kifua, kuongezeka maumbile ya viungo vya uzazi, kuwa na sauti nzito, kumfanya mtu apate hamu ya kujamiiana, kuwa na mikono iliyojitokeza kwa nje, kutembea kibabe. Pia, kichochezi hiki hasa kwa wanaume hutokea kuwa na upara kichwani. Nini athari ya kupungua kichochezihiki Wanaume wengi wanapofikia umri wa miaka 30 au zaidi, wengi wao hudhani kuwa kupungua kwa uwezo wao wa kujamiiana kunasababishwa na umri mkubwa, kumbe sivyo.
Hilo si sahihi, bali ni kupungua kwa kichochezi hiki cha testosterone. Moja ya athari ya kupungua kwa kichochezi hiki ni kupungua kwa nguvu za kiume na kutofika kileleni, kukosa mwamko wa kujamiiana, kupata ugumba kwa wale walio katika umri wa uzazi. Mambo haya yakitokea humwathiri mhusika kisaikolojia na kumfanya kuwa na sonono (depression), kuwa na tabia za ukali, msongo wa mawazo, unyongofu, kujitenga na jamii kwa kule kuhofia kunyanyapaliwa, misuli ya mwili kupungua uzito na uimara, huwa katika hatari ya kupata maradhi ya moyo.
zaidi kutoka (chanzo)
Mwananchi.