-->
Kichanga Hicho |
Oyinlola Rotimi, 22, ni mwanafunzi katika chuo cha Ukandarasi cha Obafemi Awolowo, mwanafunzi wa Mwaka wa pili amekubwa na mkasa wa aina yake baada ya kujifunguamtoto wake wa kwanza chooni.
Siku ya tukio, mwanafunzi huyo alikuwa akijiskia kutapika na kuhara tangu asubuhi na ilipofika jioni alipata kichefuchefu na ndipo alipoenda chooni akahisi maumivu makali ya tumbo huku akihisi kutokwa na kitu tumboni ilibidi achuchumae chini na ndipo alipoona damu zikimtoka na dalili ya mtoto kuja.
Alichanganyikiwa na kuanza kupiga kelele akiomba msaada kwani ilikuwa ni miujiza kwake, hakkutegemea kujifungua kipindi kile. Oyinlola alipata msaada wa kuzalishwa kutoka kwa wafanyakazi wa usafi wawili wliowahi kusikia kilio chake ambao ni Bi. Grace Shipebi na Bi. Cecilia Ologbenla.
Habari zilizagaa katika vyombo kadhaa vya habari huku wengi wakitafsiri tukio hilo kama jaribio la mauaji na kwamba binti huyo alikuwa anataka kumuua mtoto huyo. Ilibidi binti huyo aelezee kwa kina kuhusu mkasa mzima na pia mwanafunzi mwenzie ambaye anaishi nae chumba kimoja alisema ya kwamba, rafiki yake hakuwa na mpango wa kumuua mtoto wake na kwamba alishakubali kuzaa na kumlea mtoto huyo.
"Binafsi sikuwa naujua uchungu wa uzazi upoje, na ndio mara yangu ya kwanza kukutana na jambo hilo, siwezi kumuua mwanangu mwenyewe niliyembeba tumboni kwa miezi tisa kwa shida zote" Alisema Onyinlola.
Oyinlola na mwanawe akiwa na furaha |