Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » » Ng0n0Zembe Sehemu za Kazi, Wanawake wapo Hatarini kupata Maambukizi zaidi.



Kwa miaka mitatu iliyopita, Rehema Nduguru (50) anayeishi Mkoa wa Njombe alikuwa katika mazingira hatarishi ya kupata magonjwa ya ngono ikiwamo Ukimwi kutokana na kazi yake ya uhudumu wa baa.
Akitoa maelezo yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Rehema anasema kutokana na kazi hiyo alikuwa akilazimika kufanya ng0no zembe ili kujiongezea kipato. Hata hivyo, anashukuru Mungu hakupata maambukizi ya Ukimwi.
“Wakati tukifanya kazi hiyo, mimi na wenzangu tulikuwa tukifanya ng0no zembe, hasa na madereva wa magari ya mizigo yanayoegeshwa karibu na baa tulizokuwa tukifanyia kazi,” alisema Rehema.
Hata hivyo, Rehema sasa ameachana na kazi hiyo na amepata msaada kutoka Shirika la Kazi duniani (ILO).
“ILO walikuja Njombe na kutushauri tuunde vikundi ambapo tulipewa fedha zilizotuwezesha kufanya kazi zenye staha. Sasa ninauza nguo sokoni na ninapata fedha za kutosha kutokana na biashara hiyo. Tumeanzisha ushirika wa kuweka na kukopa (Saccos) ambayo inatuwezesha kujiendeleza kiuchumi,” anasema.
Kwa upande wake Mwajuma Sabuni anayefanya kazi katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam (jina linahifadhiwa) analalamikia unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa waajiri wao.
“Nimefanya kazi katika kiwanda hiki kwa miaka saba sasa. Kwa miaka miwili ya awali nilifanya kazi kama kibarua, lakini baadaye nikaingizwa kwenye mkataba wa kazi na kuanza kukatwa mafao ya uzeeni na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), bila kupewa kadi ya uanachama na mwajiri wangu. Hadi sasa sijui hatima ya pensheni yangu,” anasema na kuongeza:
“Kwa jumla hali ya ajira katika kiwanda hiki ni ngumu hasa sisi wafanyakazi wa kike kwani rushwa ya ng0no iko nje nje. Wasimamizi wa vitengo ndiyo wahusika na ukiwakataa ajira yako inakuwa hatarini. Licha ya kuwepo kwa Chama cha Wafanyakazi (Tuico) kinachojua kero zote hizi, bado hazijashughulikiwa. Naiomba Serikali iingilie katika kwa kuchunguza madai haya kwani tunanyanyasika mno.”
Maelezo ya wanawake hawa yanawakilisha kilio cha wafanyakazi wengi wanaonyanyaswa kijinsia kutokana na kazi zao. Wengi hulazimika kujiingiza kwenye ngono zisizo salama, hivyo kuhatarisha maisha yao hasa kwa kupata ugonjwa wa Ukimwi.
Katika mkutano wa wadau wa kupambana na ugonjwa wa Ukimwi, hasa maeneo ya kazi uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, wadau wanasema kuwa wanawake na wasichana wako kwenye hatari zaidi ya kuathirika na ugonjwa huo na kwamba hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa ili kukabilia na tatizo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Fatma Mrisho anasema kuwa makundi ya wanawake walijitokeza kuomba msaada ili kujikwamua kimaisha na kujilinda.
“Hatari ya wanawake hawa kuathirika na Ukimwi ni kubwa mno. Ni changamoto kubwa inayohitaji jitihada za kila mmoja wetu,” anasema Dk Mrisho.
Chanzo: Mwananchi(Web)

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga