Stori: Brighton Masalu na Issa Mnally
AISEEE! Yameshuhudiwa matukio mengi ya kamatakamata ya dadapoa kwa mwaka 2013 lakini hili ni funga mwaka.
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers kwa kolabo na polisi, safari hii imefumua madanguro mengi yaliyojificha vichochoroni na kwenye nyumba za kulala wageni na kuibuka na mambo mengi ya kushangaza.

Ukiachilia mbali sehemu za madanguro hayo, OFM ilitonywa kuwepo kwa baadhi ya gesti zinazotumiwa na wanawake hao kama madanguro kwa kuingiza na kubadili wanaume asubuhi, mchana na usiku.
Katika upelelezi wetu, baadhi ya wanawake walionaswa kwenye sekeseke hilo, ni wachumba na wake za watu.
Baadhi ya watu waliokuwa karibu na maeneo hayo, walisema imekuwa ni kero kwao kwani uwepo wa wanawake hao maeneo hayo huleta picha mbaya kwa jamii hasa watoto.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyuso za huzuni, baadhi ya wanawake walionaswa walikiri kuwa wachumba na wake za watu ila kutokana na ugumu wa maisha wanalazimika kujiingiza kwenye biashara hiyo.
Wengine walisema si wake za watu lakini wapo maeneo hayo kusaka fedha za kujinasua na ukata kutokana na ukosefu wa ajira hasa kuelekea kwenye kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
Waandishi wetu waliendelea na upekuzi kwa kuwapeleleza wanaume wateja walionaswa nao kwa kuwauliza kulikoni wafanye hivyo wakati mitaani kumejaa wanawake wengi wastaarabu ambapo walifunguka kuwa chanzo ni matatizo ya kindoa.
Hata hivyo, jeshi la polisi kupitia Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Buguruni (OCD), Lucy Kakuru alisisitiza kuwa wataendelea kupambana na biashara hiyo haramu hadi suala hilo liishe maeneo hayo.