JANGA la kusafirisha madawa ya kulevya Bongo limezidi kuwa zito kufuatia takwimu za hivi karibuni kuonesha kwamba, idadi ya wanawake kujihusisha na shughuli hiyo inazidi kupanda.
Akizungumza na Uwazi juzi, Kamanda wa Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alisema wanawake wamekuwa ni janga kwa kuwa wanaongoza kwa kukamatwa kutokana na kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ‘unga’.
NZOWA AANIKA MAMBO
Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Kamanda Nzowa alisema inasikitisha, inashangaza kwani kwa kipindi kifupi cha kuanzia Desemba 11, 2013 mpaka Januari 6, 2014 watuhumiwa watano walikamatwa na unga, kati yao wanawake walikuwa wanne.

“Hata mwaka jana mpaka Juni, wengi wa watuhumiwa tuliowakamata ni wanawake ukilinganisha na wanaume, hii ni mbinu inayotumiwa na wasafirishaji wa mihadarati kwa kuwatumia wanawake,” alisema Nzowa.
ANAJUA KITAKACHOENDELEA
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Tunajua, wahusika wakiona wanawake wanadhibitiwa sana watabadilisha na kutumia wanaume kusafirisha madawa hayo, hii hali inatisha lakini tumeigundua.”
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Tunajua, wahusika wakiona wanawake wanadhibitiwa sana watabadilisha na kutumia wanaume kusafirisha madawa hayo, hii hali inatisha lakini tumeigundua.”
UWANJA WA NDEGE DAR UPENYO?
Nzowa alisema kuwa, watuhumiwa wote hao walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar wakiwa wamepakia kete za madawa hayo tumboni wakiyasafirisha kwenda nje ya nchi.

KUPANDA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE
Kamanda huyo aliongeza kwamba wanawake watatu walikamatwa Desemba 11, mwaka jana uwanjani hapo wakiwa na madawa tumboni wakielekea nchini China.
Kamanda huyo aliongeza kwamba wanawake watatu walikamatwa Desemba 11, mwaka jana uwanjani hapo wakiwa na madawa tumboni wakielekea nchini China.
Aliwataja wanawake hao kwa ni, Mariam Hamad (29), mkazi wa Tabata- Kimanga, Dar. Alikutwa na pipi zenye uzito wa gramu 670. Hadija )Abdu (30, mkazi wa Magomeni, Dar alikutwa na kete zenye uzito wa gramu 1,227.
Wengine ni Sabrina Salum (34), mkazi wa Kiwalani, Dar. Alikutwa na unga wenye uzito wa gramu 310 na Salama Omar (miaka haikutajwa), mkazi wa Tabata, Dar alikutwa na madawa yenye uzito wa gramu 1,975. Alikamatwa Januari 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imeelezwa kuwa, wanawake wengi wamekuwa wakitumika kusafirisha unga kutokana na tabia iliyokuwepo huko nyuma kwamba, walikuwa wakiaminika na hawakuwa wakikaguliwa kwa undani walipokuwa wakipita viwanjani.
NZOWA ATAHADHARISHA
“Nawatahadharisha wale wote, wakiwemo wanawake wenye nia au wanaofanya biashara hii haramu kuacha kwa sababu vyombo vya dola vitawakamata,” alisema Nzowa.
“Nawatahadharisha wale wote, wakiwemo wanawake wenye nia au wanaofanya biashara hii haramu kuacha kwa sababu vyombo vya dola vitawakamata,” alisema Nzowa.
WANAOGOPWA VIWANJA VYA NDEGE
Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipohojiwa na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema wanawaogopa sana wanawake wanaosafiri siku hizi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipohojiwa na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema wanawaogopa sana wanawake wanaosafiri siku hizi.
“Hivi sasa tunawaogopa sana wanawake wanaosafiri kwa ndege kuliko wanaume kwa sababu wanaweza kukuingiza katika matatizo ikiwa watapenya na madawa ya kulevya na kukamatwa hapa Dar au huko nje ya nchi,” alisema mfanyakazi mmoja.
Alifafanua kwamba, kutokana na hilo wamekuwa wakiwapekua wanawake kila sehemu za miili yao hata sehemu nyeti ikibidi ili kuhakikisha hawapiti na madawa hayo uwanjani hapo.
WANAWAKE HAO WAPO MASTAA
Hivi karibuni baadhi ya mastaa Bongo wamenaswa kwa kujihusisha na biashara hiyo. Baadhi yao walikutwa na hatia na kuhukumiwa, wengine kesi zao zinaendelea.
Hivi karibuni baadhi ya mastaa Bongo wamenaswa kwa kujihusisha na biashara hiyo. Baadhi yao walikutwa na hatia na kuhukumiwa, wengine kesi zao zinaendelea.
Wasanii hao ni Jacqueline Patrick (alikamatwa Macau-China), Saada Kilongo (JNIA-Dar), Agnes Gerald ‘Masogange (Afrika Kusini) na Melisa Edward (Afrika Kusini). Pia yumo Mbongo aliyenaswa Misri aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma huku Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ akitumikia kifungo cha miaka mitano China.
JK AKASIRIKA, AWAONYA WASANII
Akizungumza katika mkutano mmoja na wasaniiwa Rais Tanzania, Jakaya Kikwete ‘JK’ alionesha hasira zake za wazi kwa wasanii wanaotumika kubeba unga kwenda nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano mmoja na wasaniiwa Rais Tanzania, Jakaya Kikwete ‘JK’ alionesha hasira zake za wazi kwa wasanii wanaotumika kubeba unga kwenda nje ya nchi.
JK aliwaonya wasanii wenye tabia hiyo na wale ambao wapo katika ushawishi wa kujiingiza kwenye biashara hiyo inayopigwa vita kwa sasa duniani kote kuacha kufanya hivyo.