MSANII nyota wa filamu Irene Paul, amesema kwamba haoni mwanamke mwenye uwezo wa kumuibia bwanaake, ingawa hataki kumtaja hadharani kwakuwa alishaapa kutoyaanika maisha yake binafsi hata kabla hajawa staa.
Irene alizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni ambapo alisema kwamba mashabiki wake wanatakiwa kujua kwamba ana mp#nzi . "Mtu anataka niweke hadharani bwana wangu wakimjua watapata nini??
Hakuna anayeweza kumchukua mp#nzi wangu hilo najua lakini maisha yangu ya sanaa tofauti na yale binafsi hivyo mashabiki wangu naomba wafahamu hilo", alisema.Hata hivyo alisema kwamba amekuwa mtu wa kuheshimu mambo yake ya ndani kwani ndiyo yanaweza kuharibu kila kitu endapo atafanya matangazo kama wengine wanavyofanya.