Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » HUU NDIO MTAZAMO WA MBUNGE WA NCCR MAGAUZE, MOSES MACHALI KUHUSIANA NA SAKATA LA ZITTO NA CHADEMA

                                                         

                                                                    Moses Machali
Kuna watu wanazungumzia nidhamu na kwamba ili mtu uweze kufanikiwa maisha ni lazima uwe na nidhamu. Nami nakubaliana na kauli hiyo, lakini tunapaswa kujiuliza ni nidhamu ya aina gani? Inawezekana mtu akasema ZITTO hana nidhamu kwa chama chake lakini ikawa ni kinyume chake. Hii ni kwa sababu hana nguvu za kufanya maamuzi ndani ya chama na kwa hiyo akawa anatakiwa kutii mambo ambayo yako kinyume cha utaratibu wa chama chake lakini kwa kuwa yanatolewa na kusimamiwa na watu wenye nguvu basi akipinga anaonekana hana nidhamu. Binafsi niseme moja tu kwamba, wakati mwingine sisi wanasiasa tunakurupuka na kukosea. Katika sakata la zitto na CDM nadhani pande zote zinaweza kuwa na makosa kwa kuwa hadi mambo yamefikia hapo yalipofika ni kwa sababu kumekosekana collective responsibilty na imekosekana pia nidhamu ya kiuongozi inavyoonekana kwa kuwa hata akina Mbowe; Dr. SLAA na wengine siyo malaika wakati mwingine nao hukosea tena sana.

Na kwa hiyo napingana na wale wote wanaosema mkosefu ni Zitto tu la hasha ni uonevu kwa upande mmoja. Lakini pia napingana na wale wote wanaosema Zitto anaonewa tu la hasha inawezekana kweli kukawa kuna makosa tofauti na historia tunayoifahamu wachache. Ngoja niwakumbushe kidogo wana jamvi: Mwaka 2009 wakati wa uchaguzi ndani ya CDM uliibuka mgogoro kati kundi la Mbowe na kundi la Zitto ambapo wazee wa chama wakamtaka Zitto aache kugombea uenyekiti wa chama kwa kuwa yeye ni kijana bado ana muda mwingi na kwamba anaweza kugombea wakati mwingine na kwa hiyo amwachie mbowe kwanza akiongoze chama. Finally Zitto alijiondoa kwa shingo upande yaani pasipo kupenda na wafuasi wengine wa Zitto wakakutana na majanga mazito ndani ya CDM na wakaamua kuondoka CDM wakaitwa majina ya kwamba wao ni sisimizi nk; wakati mwingine wakaitwa Wasaliti na watu wenye njaa nk.

Waliopatwa na kadhia hiyo baadhi ni hawa wafuatao: mhe. david KAFULILA(MB), MARTINE DANDA kutoka Iringa. Wengine ni akina Mhe. Mkosamali(mb) pamoja nami Machali(mb) na baadaye kabisa waliondoka akina Mama Msole nwengineo. Wapo wadau wasemao kwamba huenda mgogoro uliopo hivi sasa unatokana na kile kilichotokea 2009 kwa kuwa CDM walipaswa kufanya uchaguzi lakini wakaahirisha kwa kile kinachosema kwamba watamwambia nini Mhe. Zitto mwaka huu katika kugombea Uenyekiti wa chama kama ilivyo dhamira yake ya siku nyingi ya kukiongoza CDM. INASEMEKANA kwamba baadhi ya viongozi wa CDM wenye nguvu ndani ya chama wametafakari ni namna gani Zitto hapenyi katika kinyanganyiro cha uchaguzi ikaonekana ni ngumu sana na kwamba inabidi kuangalia namna ya kufanya na huenda ndiyo haya tunayoyaona sasa. Aidha Ikumbukwe kuwa kuna nyakati vyombo vya habari vilimnukuu Mhe. Mbowe akisema kwamba Dr. Slaa ndiye atakaechukua fomu za kugombea Urais na kwamba yeye hatagombea tena(Mbowe), Lakini Zitto amekuwa akitangaza nia ya kugombea Urais anakutana na vikwazo au mikwara mingi kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa CDM. Na baadhi ya vyombo vya habari vilipata kumnukuu Mzee Mtei akimshauri Mhe. Zitto kuachana na masuala ya kutangaza nia ya kuombea urais kwamba ni kusababisha fujo au vurugu ndani ya CDM na kwamba atulie hadi wakati ukifika.

Tujiulize mimi na wewe, inakuaje Zitto akitangaza nia iwe kosa lakini Mbowe akitangaza nia iwe ni sawa wakati kwa mujibu wa katiba ya CDM kuna mamlaka inayotakiwa kumtangaza mgombea urais ni nani lakini pia sidhani kama kuna mahala katiba ya CDM inakataza Mwanachama wake kutangaza nia ya kugombea nafasi fulani kama vile urais. Kama kuna kipengele hicho CDM wanapaswa kukionesha ili kuondoa mashaka yaliyopo juu ya kwamba wanamuonea Mhe. Zitto. Hata hivyo wapo wanachama wengi wametangaza nia kugombea Ubunge ndani ya CDM mwaka 2015 kama ilivyokuwa kwetu sisi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; tulitangaza nia sana tu; wote akina Wenje, akina HAINESS KIWIA na wengine na hawakuelezwa kwamba wanaleta fujo ndani ya CDM. dugu zangu ndiyo maana ninakuwa na mashaka wakati mwingine kwa kusema kwamba huenda kweli Mhe. Zitto akawa anaonewa kama anavyosema, mtazamo huu unatokana na records hizo za nyuma. CDM wajitokeze kufafanua hoja hizo ili nasi makomredi wao kimkakakti tuweze ku clear dout. Inawezekana baadhi wakaja na maneno maneno yaliyozoeleka kwamba nimetumwa na Zitto nk. La hasha ni utashi wangu tu kutokana na uzoefu wangu katika siasa za CDM na sasa niko NCCR-Mageuzi. Uzoefu wangu usibezwe kwa kuwa ninayo

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga