MKESHA wa Mwaka Mpya (2014) ulikuwa ni kilio, huzuni na majonzi kwa wakazi wa Pugu Kwamustafa, Ilala jijini Dar es Salaam kufuatia Meja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Rashid Musa (43) kudaiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi hadi kufa madenti wawili na wengine watatu kujeruhiwa wakati wakisherehekea mwaka.
Madenti waliouawa ni Ibrahim Mohamed (16), wa kidato cha tatu na Abubakar Hassan (14), wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Kinyamwezi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, siku ya tukio, Meja Rashid wa Kikosi cha Jeshi Land Force Kibaha, alidaiwa kuwamiminia risasi vijana hao waliokuwa wakishangilia kuuona mwaka mpya wakati walipokuwa wakivuka barabara.

Ibrahim Mohamed enzi za uhai wake.
SHUHUDA NZITO
Kufuatia tukio hilo la kuhuzunisha, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi liliwatafuta mashuhuda wa tukio hilo na kuzungumza nao wanachokijua.

“Kwa jina naitwa Rashid Juma nina miaka kumi na tatu, nakumbuka siku hiyo tulikuwa watoto wa kike na wa kiume, wengi wenye umri kati ya miaka nane hadi kumi na saba, tulikuwa kama themanini hivi, ilipofika saa sita kamili usiku tuliingia mitaani kushangilia kwa kuuona mwaka mpya.
“Si mara ya kwanza sisi watoto wa mtaa huu kusherehekea mwaka mpya, kila mara tunafanyaga hivyo na kurudi majumbani salama, lakini nashangaa safari hii kipindi hiki hili balaa limetoka wapi?
“Ilipofika saa sita na dakika tano tukiwa tunaendelea kusherehekea huku tukivuka barabara, tulipishana na gari la mwanajeshi huyo, hatukumtukana wala, ghafla tulisikia mlio wa risasi, paa! Paa! Papapa!
“Kabla hatujakaa sawa tulimwona mwenzetu (Abubakar) yupo chini huku akilia kwa uchungu akihitaji msaada, kabla hatujakaa sawa tena risasi ziliendelea kusikika, wengine wakiwa wamedondoka chini.

Mimi na wenzangu wengine tulikimbia, tulijua ni majambazi,” alisema shuhuda huyo, akaendelea:
“Baada ya kutawanyika, tuliliona gari likiondoka katika eneo la tukio, tukapiga kelele, ndipo wazazi wetu wakatoka nje na kuliona lile gari. Wengine walilitambua kwa vile yule mwanajeshi anaishi karibu na maeneo haya, amekuwa akipita na gari lake hilo mara kwa mara.

“Hata hivyo, yule mwanajeshi hakusimama, nasikia alikwenda hadi kwake, tulirudi na kuwaangalia waliopigwa risasi ndipo tuligundua kuwa wenzetu wawili walikufa na wengine walijeruhiwa.
MAJERUHI AZUNGUMZA
Naye mmoja wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Agustina Pius alipohojiwa na Uwazi alisema siku ya tukio alikuwa nje ya nyumba yake akiongea kwa simu na ndugu zake wa mikoani akiwapongeza kwa kuuona mwaka mpya.

“Ghafla nikasikia milio ya risasi barabarani huku watoto waliokuwa wakisherehekea wakipiga kelele za kusema tunakufa…tunakufa,” alisema majeruhi huyo.
Aliendelea kusema kwamba kufuatia hali hiyo, aliweka simu kwenye mfuko wa suruali na kuingia ndani, lakini ghafla alisikia kitu kimepiga simu yake na kulipuka.

Aliitoa mfukoni ikiwa inawaka moto na kuitupa chini, alipojikagua ndipo aligundua anatokwa na damu nyingi kwenye paja, alipoangalia chini aliona risasi.
“Niliwaambia watu wa jirani yangu ambapo walinikimbiza Hospitali ya Amana kwa matibabu,” alisema.

BABA MZAZI WA MAREHEMU
Naye baba mzazi wa marehemu Abubakar, mzee Hassan alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema ni tukio la ajabu sana kwake kwani watoto hao kila mwaka katika kuukaribisha mwaka mpya hutoka nje kuushangilia, anashangaa kusikia wameuawa kwa risasi.

KAMANDA MINANGI
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimfuata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Afande Marietha Minangi Komba na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alikiri kulipokea, akasema:

“Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba meja huyo alifyatua risasi hewani kwa kudhani kuwa wale vijana walikuwa wahalifu, hivyo alikuwa akijihami.
“Kwa sasa tunamshikilia (meja). Wakati wa kukamatwa kwake bastola yake ilikuwa na risasi kumi, tano zilitumika katika eneo la tukio. Jeshi langu linaendelea na uchunguzi na sheria itachukua mkondo wake,” alisema kamanda huyo.
WALIOJERUHIWA
Waliojeruhiwa katika sakata hilo ni Lugano Wanga (17), Kasim Abdul (16) na Agustina Pius (28) ambao walikimbizwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na kuruhusiwa.

GPL.