Feature

Udaku wa Africa

Habari za Kimataifa

Habari za Kitaifa

Mapenzi

Michezo na Burudani

Udaku wa Ulaya

» » MKE ATOWEKA KIMIUJIZA, USHIRIKINA WATAJWA



Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni imani za kishirikina, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Merry Patrick  au Mama Jack, mkazi wa Magole B Ilala jijini Dar es Salaam, ametoweka kimiujiza nyumbani kwake usiku wa manane wiki iliyopita.
Merry Patrick  au Mama Jack aliyetoweka kimiujiza
Chacha Muhochi, mume wa mwanamke huyo, aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio, saa tisa usiku akiwa nje ya nyumba akilinda mifugo yake, aLimwacha mkewe amelala ndani, ghafla alisikia sauti ya mtoto wake wa mwisho akilia, hali iliyomfanya akimbilie ndani kutazama kilichotokea.
Baada ya kuingia ndani, alishangaa kutomuona mkewe kitandani kwani mtoto alikuwa peke yake. Alipojaribu kuchunguza, mlangoni mwa nyumba yake, aliona damu. Aliingia katika vyumba vyake vyote pasipo kumuona mkewe huyo, ambaye pia alikuwa ni mwanakwaya wa SDA.
“Sikujua nini kilimkuta mke wangu, nilihangaika kila kona sikumuona, nikaona niende kwa mjumbe na kutoa taarifa polisi, hadi ninavyozungumza na wewe bado hajaonekana,” alisema Chacha na kuonesha hati ya Polisi (RB) STK/RB/23241/2013.
Lakini katika hali ya kushangaza, baadhi ya majirani na waimba kwaya wenzake, wanadai mwanamke huyo huwa anaonekana nyakati za usiku na kwamba simu yake ikipigwa inaita bila kupokelewa, lakini baadaye hutuma ujumbe usioeleweka.
Mmoja wa waimba kwaya ambaye pia ni jirani na mama Jack, alisema wamekuwa wakikesha katika kufanya maombi kila siku, lakini wamekuwa wakishangazwa na ujumbe wanaopata wanapojaribu kupiga simu ambayo huwa haipokelewi.
“Tuache kwanza, kwa sasa ana majukumu, yuko bize, ila mchawi wenu hataki akae hapa, anaweza kuja muda wowote, yuko bomba kinoma,”  huu ni mmoja wa ujumbe unaotajwa kuandikwa kupitia simu ya mwanamke huyo anayedaiwa kutoweka kimiujiza.
Mwanakwaya mmoja alidai siku moja wakiwa katika maombezi, ujumbe mwingine kutoka simu ya mwenzao huyo uliingia katika simu ya wanamaombi hao na uliosomeka hivi; “Wachawi wakubwa mkiongozwa na huyo aliyejuu, ng’ombe wakubwa nyie, pigeni magoti chini.”



Mjumbe wa shina namba saba Bi. Fatuma Juma alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la aina yake ambalo limewatia hofu kubwa wakazi wa eneo hilo.

About Unknown

Habari karibu katika Blog hii, Tafadhali Like Page Yetu na Toa Maoni yako kuhusiana na kile unachokiona humu.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Majanga