MWANDISHI HUYU MAHIRI KUTOKA KENYA AJITANGAZA HADHARANI KWAMBA NI "SHOGA"
Hii inamfanya Binyavanga kuwa mmoja wa wafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.
Matendo ya kimap#nzi kwa watu wa jinsia moja hayakubaliwi nchini Kenya, na nchi nyinginezo za Afrika.
Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliyowiana na siku ya kuzaliwa kwake.Ana umri wa miaka 43.
Hii inakujia wakati ambapo kuna mjadala mkali nchini Kenya na katika baadhi ya mataifa ya Afrika kuhusiana na suala la haki za wap#nzi wa jinsia moja.
Hivi karibuni, Nigeria ilipitisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa makundi ya watu wanaoshiriki map#nzi ya jinsia moja, ilhali Rais wa Uganda alikataa kuhalalisha mswada kama huo uliopitishwa bungeni.
Uamuzi wa Binyavanga kujitokeza hadharani umepokelewa kwa hisia mbali mbali nchini Kenya. Kunao waliompongeza ingawa baadhi wanahisi kuwa huenda jamii ikamnyanyapaa.
Binyavanga aliwahi kushinda tuzo la mwanadishi bora zaidi Afrika la Caine mwaka 2002.
Watu wanaoshiriki map#nzi ya jinsia moja nchini Kenya wanaweza kuadhibiwa kifungo cha miaka kumi jela ikiwa watapatikana na hatia.