Ni mara chache kusikia video flani ya bongofleva haichezwi kwenye vituo vya TV kwa sababu ya wamiliki wa vituo hivyo kuona haina maadili hivyo haiwezi kuruhusiwa kuonyeshwa kwa mamilioni ya Watanzania.
Video ya Jux toka mwaka 2013 mwishonimwishoni stori zilikua zinazunguka kwamba hii video imefungiwa kwenye vituo vya TV za bongo sababu picha zinazoonekana ndani yake zimezidisha kuvuka mipaka ya kimaadili.
Kwa sababu taarifa hizi ‘inadaiwa’ hazikutokea BASATA, wengi walisubiria Jux mwenyewe akirudi Tanzania atasema nini kuhusu hii ishu manake labda ni vituo vya TV vyenyewe ndio vimeamua kuisimamisha bila agilo la BASATA hivyo kama ni TV zenyewe basi vingekua vimemwambia.
Anachosema ni hiki >>> ‘Mimi nilikua China ndio B12 akaniambia video yako imefungiwa, nilivyorudi Tanzania BASATA tulipoulizia wakasema hawana hizo taarifa na ni lazima wapitiwe kwanza wao kwenye ishu kama hii… na lazima wakichukua hatua wanatoa taarifa kwa muhusika, wakasema kuna vitu viwili inawezekana kuna michezo imechezwa’
Swali : Toka umerudi bongo umeshawahi kuiona hii video ikichezwa kwenye TV?
Jux : ‘hapana ila kuna watu waliniambia wameshawahi kuiona EATV, pia mimi sio mtazamaji wa TV sana’
Angalia Video hapo chini:-