Waziri mkuu wa Latvia ajiuzulu kutokana na maafa yaliyoikumba Taifa hilo
Waziri mkuu wa Latvia, Valdis Dombrovskis, ametangaza kujiuzuru wadhifa wake mara baada ya kujiona kisiasa kuwa anahusika na kuanguka kwa paa la supermarket ambalo lilisababisha vifo vya watu 54 na kujeruhi wengine 40 wiki iliyopita, hivyo ana kila sababu ya kuwajibika kutokana na tukio hilo, Associated Press imetaarifu.
Paa la Supermarket ya Maxima iliyopo ndani ya Riga lilianguka siku ya Alhamisi Novemba 21 likiuwa watu kadhaa wakiwamo wakowaji watatu na wengine 39 wakiwa wameumia vibaya sana.
Kuanguka kwa paa la supermarket hiyo ni janga kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa nchi hiyo ya Latvia toka mwaka 1950.
Nasi tujifunze kuwajibika....
Dc.